Kibaka Anapojisaidia Kwenye Nyumba Aliyoingia Kuiba.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibaka Anapojisaidia Kwenye Nyumba Aliyoingia Kuiba..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 29, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wednesday, November 25, 2009 4:35 PM
  Hivi inakuwaje pale unapoamka usiku kwenda kujisaidia Toilet na kumkuta mwizi aliyezamia nyumbani kwako kwa nia ya kuiba akiendelea kujisaidia na kukutaka usubiri amalize haja zake? Mwizi mmoja nchini Mexico alitiwa mbaroni katika eneo la tukio baada ya kujipa mapumziko ya kukusanya mali na kwenda kujisaidia kwenye choo cha nyumba aliyoingia kuiba.

  Kwa mujibu wa taarifa ya polisi katika mji wa Puebla, kibaka huyo alizamia kwenye nyumba moja katika mji huo kwa nia ya kuiba.

  Lakini akiwa katikati ya shughuli yake ya wizi, alijisikia haja kubwa na kwenda kujisaidia kwenye choo cha nyumba aliyokuwa akiiba huku wakazi wa nyumba hiyo wakiwa wamelala.

  Bahati mbaya kwa kibaka huyo, mwenye nyumba naye aliamka usiku huo kwenda Toilet na kushangaa kuona mlango umefungwa huku akisikia kelele zikitoka Toilet humo.

  Alipojaribu kuufungua mlango huo kibaka huyo alijibu "Kuna mtu subiri kidogo".

  Mwenye nyumba alikifunga choo hicho kwa nje na kuita polisi na kibaka huyo alitiwa mbaroni baada ya kutolewa toka kwenye choo hicho.

  Kibaka huyo amefunguliwa mashtaka ya kuvunja na kuzamia nyumba za watu na kufanya wizi.

  Mwenye nyumba naye amesema hataki kukitumia tena choo hicho na ameongeza kuwa ataita mafundi waje wakiondoe choo hicho cha kukalia na kuweka choo kipya.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3612110&&Cat=2
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  inategemea.......kama panga ninalo mkononi ndo wasaa mzuri wa kumkata mguu mmoja
   
Loading...