Kibaka Ajaribu Kuchomoka na Zawadi za Harusi ya Mtoto wa Sumaye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibaka Ajaribu Kuchomoka na Zawadi za Harusi ya Mtoto wa Sumaye

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, May 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,185
  Likes Received: 3,114
  Trophy Points: 280
  Kibaka Ajaribu Kuchomoka na Zawadi za Harusi ya Mtoto wa Sumaye
  [​IMG]
  Wananchi wenye hasira wakijaribu kumuadhibu kibaka aliyejaribu kuchomoka na zawadi za harusi ya mtoto wa SumayeMonday, May 25, 2009 4:31 AM
  Katika kuonyesha kwamba vibaka wa Tanzania wanatumia mbinu mbali mbali za ajabu, kibaka mmoja aliyejifanya mgeni mualikwa katika harusi ya mtoto wa Sumaye alipewa kipigo cha nguvu baada ya kukamatwa akijaribu kuchomoka na zawadi za maharusi.Wizi katika kumbi za sherehe hasa katika hoteli kubwa jijini Dar es Salaam umezidi kushamiri kwa kasi ya ajabu.

  Katika harusi ya mtoto wa Sumaye iliyofanyika jumamosi kijana mmoja ambaye alijifanya kuwa ni mmoja wa wanandugu wa waziri mkuu wa zamani Fredrick Sumaye alipata kipigo cha nguvu baada ya kukamatwa akiwa amebeba kifurushi kilicho kuwa kimejaa zawadi za maharusi akijaribu kuondoka nazo kutoka katika ukumbi wa Hoteli ya Ubungo Plazza.

  Katika kumbi nyingi hivi sasa kumekuwepo na vijana wasichana kwa wavulana ambao huwa wanavalia kinadhifu na bila kujua utadhani ni miongoni mwa wageni waalikwa, na pindi unapofika wakati wa kwenda kuchukua chakula wengi wa wageni huacha simu zao na zawadi zao mezani na vibaka hutumia nafasi hiyo kuzichukua na kuondoka nazo.

  Kijana huyu aliyekamatwa alikuwa tayari kishaanza kutafuta tax kwa ajili ya kuondoka na mizigo aliyoiba.

  Mizigo aliyoiba ilikuwa ni zawadi za maharusi na kama angefanikiwa kutoweka nazo basi angefaidika sana maana kulikuwa na vitu vingi vya thamani sana.

  Katika sakata hilo hata walinzi wa Ultimate Security hawakumshitukia kibaka huyo kwani walidhani ni miongoni mwa wahusika katika sherehe hiyo.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,185
  Likes Received: 3,114
  Trophy Points: 280
  Karibu kwa picha zaidi
   

  Attached Files:

 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 889
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Na mambo ya siku hizi zawadi huachwa mlangoni. Hata wanandugu au marafiki wetu tunaowaamini wanaweza kutokomea na mojawapo ya zawadi inayoonekana kuwa ya thamani. Kwani utajuaje ilikuwepo zawadi kama hiyo ikikumbukwa kwamba huambiwi aksante kwa zawadi aina.....uliyotoa. Tuwe makini.
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,864
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Huyu kibaka naona ana akili!
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,185
  Likes Received: 3,114
  Trophy Points: 280
  Hiyo inawaonyesha sherehe za wakubwa hazina ubaguzi hata vibaka ruksa
   

  Attached Files:

 6. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Aliingiaje bila vazi la harusi?
   
 7. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #7
  May 26, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu,

  heshima mbele.
  Hebu nipashe...hana au ana akili?
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Namwona mzee wa Lupaso na tabasamu la nguvu! Hongera kijana kuvuta jiko
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,254
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 0
  vazi la harusi likoje?
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  May 26, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 70,251
  Likes Received: 27,863
  Trophy Points: 280
  tuxedo?
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,254
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 0
  shem shori bonge huyu.....alafu naona nyuma hakujatuna....
   
 12. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #12
  May 26, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Duh!!..Yo Yo banaeee!!!!!!!..vipi tena aisee???? Mke wa mtu unamtizama
  nyuma?...astaghafirulahi laadhim!
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Shem hana mvuto kwa kifupi.....kapigwa pasi fulani....!
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,254
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 0
  aaaah mkuu kwenye harusi wwe unaangaliaga keki nini?

  yah shem si unajua wachaga tena sijaangalia guu......
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Zitakuwa fito....!
   
 16. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #16
  May 26, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,061
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 180
  Mtu na shemeji yake (Yo Yo en Masa)
  Oeni na nyie tuje kuwachambua hapa vimwana wenu, isije ikawa mna flatscreen hamjijui..ha ha
  Hongera kwa maharusi, mwanaume karidhika na mwanamke wake mwacheni aenjoy maisha ya ndoa esp. ya awali..
   
 17. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Hivi huu ukumbi wa ubungo plaza kuukodi kwa harusi kama hivi ni kiasi gani?
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  May 26, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 70,251
  Likes Received: 27,863
  Trophy Points: 280
  Wapigie simu uwaulize
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  May 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Duu Flat Screen ...... am afraid theres no space to keep it.....labda Yo Yo!
   
 20. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #20
  May 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,254
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 0
  kwikwikwikwikwi
   
Loading...