Kibaka aduwaza walinzi Ikulu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,232
31,032
Mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam, Ally Nasoro (41) amefikishwa mahakamani kujibu shitaka la kuingia Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete na kuiba ua moja lenye thamani ya Sh. 5,000, mali ya Ikulu hiyo.

Mshitakiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mwajuma Diwani wa Mahakama ya Mwanzo Kariakoo jijini Dar es Salaam jana, na kusomewa shitaka hilo.

Akisoma hati ya mashitaka, karani wa mahakama hiyo, Caphren Maduhu, alidai mbele ya hakimu Diwani kuwa mshtakiwa alifanya kitendo hicho Mei 2 mwaka huu.

Mahojiano mahakamani hapo yalikuwa kama ifuatavyo:
Karani: Kesi hii ni ya wizi na imefunguliwa na mlalamikaji ambaye ni askari mwenye namba E 4716 Koplo Mnyaga.

Mshitakiwa katika shitaka hili ni Ally Nasoro, anaishi eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam na anakabiliwa na kosa wizi alilofanya Mei 2, mwaka huu, saa 4:24 usiku huko Ikulu ya Rais.

Hakimu: Mshitakiwa umesikia mashitaka ya kosa lako, unajibu nini?

Mshitakiwa: Mimi nilikuwa napima uwezo wa akili wa walinzi waliowekwa Ikulu ili kumlinda Rais wa nchi, maana isije ikawa wako wako tu kumbe hawana hata uwezo wa kumlinda.

Hakimu: Ile ni sehemu ya heshima na inalindwa iweje wewe upate wazo la kutaka kuingia ndani, ulikuwa na nia gani?

Mshitakiwa: Nililichokigundua siku hiyo ni kwamba kumbe naweza kuingia Ikulu kiulaini bila hata ya kuguswa na mtu.

Kwanza nilipofika pale getini nilitaka kufahamu kama naweza kufanikiwa kuingia, hivyo, nilisimama kwa saa nne nje ya geti bila hata kuulizwa chochote na walinzi.

Baadaye nilifanikiwa kupata mwanya wa kuingia ndani na kweli niliingia kiulaini bila hata `shobo.

Hakimu: Ilikuwaje mpaka ukaiba hilo ua?
Mshitakiwa: Nilipolichukua lile ua na kulibeba ndipo walinzi waliniona na baada ya kuniona walinzi hao walibaki wakitetemeka huku mimi nikiwa nimeshikilia ua na ndipo waliponikamata na kunichukulia hatua.

Kama naweza kuchukua ua si ningeweza hata kuingia ndani kwa Rais kiulaini? Yaani walinzi wamelala pale. Hawako makini kama nilivyodhani.

Hakimu: Unajibu nini kuhusu shitaka la wizi huo?
Mshitakiwa: Si kweli, sijaiba ua.

Hakimu Diwani aliahirisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa tena mahakamani hapo Mei 11 mwaka huu. Mshitakiwa alipelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ambayo ni kuwa na wadhamini wawili.

Kibaka aduwaza walinzi Ikulu
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,254
10,275
Mh! aliyosema huyo kibaka yana-make sense. Kama hali ndiyo hiyo, basi inabidi hata walinzi wachukuliwe hatua kwa uzembe wakiwa kazini.
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,067
2,170
Kama wangekuwa hawawezi kazi basi wasingemkamata huyo jamaa. Kazi ya walinzi hao ni kumlinda rais na sio kulinda maua ya Ikulu. Kama wangekuwa walinzi wa maua ya Ikulu basi wangetakiwa wachukuliwe hatua.
 

Kaka K

Senior Member
Feb 9, 2008
129
4
Kama wangekuwa hawawezi kazi basi wasingemkamata huyo jamaa. Kazi ya walinzi hao ni kumlinda rais na sio kulinda maua ya Ikulu. Kama wangekuwa walinzi wa maua ya Ikulu basi wangetakiwa wachukuliwe hatua.

kama jamaa alikuwa tayari amesha ingia ndani...ni ishara tosha kuwa alikuwa na uwezo wa kuingiza kitu chochote...mfano bomb amabalo linaweza kulipuka badaea sana mkuu akiwa ndani na walinzi wake. Kazi ya ulinzi tena kumlinda mkuu wa nchi ina involve mambo mengi sana zaidi ya hilo la kumwangalia presida as an individual.

TOR ya hao walinzi sijui inasemaje....may be sio jukumu lao kulinda ikulu.

Nihayo tu
 

FairPlayer

JF-Expert Member
Feb 27, 2006
4,144
708
Story ya kutunga au? sasa ameibaje Uwa? , tuseme alikuwa analihamisha tu. Hapo vipi?
 

Mshiiri

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
2,012
505
Kesi haiwezi kuwa Mei na thread ni ya jana bana!! We are not PUMBAFS! Aweke case reference number ili tujue kama ni kweli au ni fiction aLA!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom