Kibaka aduwaza walinzi Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibaka aduwaza walinzi Ikulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by raisi, May 9, 2009.

 1. Kibaka aduwaza walinzi Ikulu

  2009-05-08 13:51:35
  Na Jacqueline Mosha


  Mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam, Ally Nasoro (41) amefikishwa mahakamani kujibu shitaka la kuingia Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete na kuiba ua moja lenye thamani ya Sh. 5,000, mali ya Ikulu hiyo.

  Mshitakiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mwajuma Diwani wa Mahakama ya Mwanzo Kariakoo jijini Dar es Salaam jana, na kusomewa shitaka hilo.

  Akisoma hati ya mashitaka, karani wa mahakama hiyo, Caphren Maduhu, alidai mbele ya hakimu Diwani kuwa mshtakiwa alifanya kitendo hicho Mei 2 mwaka huu.

  Mahojiano mahakamani hapo yalikuwa kama ifuatavyo:

  Karani: Kesi hii ni ya wizi na imefunguliwa na mlalamikaji ambaye ni askari mwenye namba E 4716 Koplo Mnyaga.

  Mshitakiwa katika shitaka hili ni Ally Nasoro, anaishi eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam na anakabiliwa na kosa wizi alilofanya Mei 2, mwaka huu, saa 4:24 usiku huko Ikulu ya Rais.

  Hakimu: Mshitakiwa umesikia mashitaka ya kosa lako, unajibu nini?

  Mshitakiwa: Mimi nilikuwa napima uwezo wa akili wa walinzi waliowekwa Ikulu ili kumlinda Rais wa nchi, maana isije ikawa wako wako tu kumbe hawana hata uwezo wa kumlinda.

  Hakimu:
  Ile ni sehemu ya heshima na inalindwa iweje wewe upate wazo la kutaka kuingia ndani, ulikuwa na nia gani?

  Mshitakiwa: Nilichokigundua siku hiyo ni kwamba kumbe naweza kuingia Ikulu kiulaini bila hata ya kuguswa na mtu.

  Kwanza nilipofika pale getini nilitaka kufahamu kama naweza kufanikiwa kuingia, hivyo, nilisimama kwa saa nne nje ya geti bila hata kuulizwa chochote na walinzi.

  Baadaye nilifanikiwa kupata mwanya wa kuingia ndani na kweli niliingia kiulaini bila hata 'shobo'.

  Hakimu:
  Ilikuwaje mpaka ukaiba hilo ua?

  Mshitakiwa: Nilipolichukua lile ua na kulibeba ndipo walinzi waliniona na baada ya kuniona walinzi hao walibaki wakitetemeka huku mimi nikiwa nimeshikilia ua na ndipo waliponikamata na kunichukulia hatua.

  Kama naweza kuchukua ua si ningeweza hata kuingia ndani kwa Rais kiulaini? Yaani walinzi wamelala pale. Hawako makini kama nilivyodhani.

  Hakimu: Unajibu nini kuhusu shitaka la wizi huo?

  Mshitakiwa: Si kweli, sijaiba ua.

  Hakimu Diwani aliahirisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa tena mahakamani hapo Mei 11 mwaka huu. Mshitakiwa alipelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ambayo ni kuwa na wadhamini wawili.
   
 2. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Raisi mwenyewe huwa hayupo nchini, ni reflection ya nchi inavyoendeshwa, kama mwananchi anaweza kuiba ua ikulu, wakina Rostam mnadhani wamechuma ngapi benki kuu...
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  May 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Huyu alistahili kuachwa, ni fundisho kwao kuwa hawako salama!
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mimi nilidhani walinzi ndio waliokuwa wanastahili kuwa mahakamani au naota?

  Inasikitisha... taasisi gani hapa kwetu inafanya kazi vizuri naomba moja tafadhali?
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa wanalinda kwa mazoea licha mi kamera waliweka kwa bei mara 3 na tenda waliyompa mtoto wa Apson eti afunge kamera za ikulu...kama ameweza kusimama nje kwa saa 4.....kazi ipo.ila pia wakampime akili.
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kaka tatizo sio camera, tatizo ni walinzi wanaangalia matukio kwenye camera?

  Ila sisi hatujui matumizi halisi... maana camera zina matumizi ya namna mbili.

  1. Kuzuia matukio, kwa hiyo wapo watu live wanaoangalia matukio 7/24/365 na kwa mapungufu ya binadamu walinzi hawa wanatakiwa kubadilishwa kila baada ya masaa mawili (2)... kwa sababu baada ya hapo wanaloose concentration. [PRE]

  2.Kurecord matukio, ili likitokea tukio baya,,, tuunde kamati ya kutafuta lilianzia wapi... Mungu saidia kama system ya camera yenyewe isiharibike...[POST]

  Sasa ni muhimu tujue zinatumika kwa matumizi yapi kati ya hayo hapo juu.

  Ila inauma kwa kweli na si haki kitu kama hiki kupeleka mahakamani, mimi nadhani wangemalizana bila kuonyesha umma...maana jambo lolote likiwa mahakamani linakuwa wazi.

  Kwa hiyo kama zile camera ziko kwa ajili ya (2) hapo juu, kesho yake ndio tungejua jana aliiba mtu ua, kama tungeona upungufu wa ua.
   
 7. M

  Manundu Member

  #7
  May 9, 2009
  Joined: Apr 7, 2008
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Iliyoratibu wizi wa EPA!
   
 8. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  BUnge tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika , Unguja na Pemba.
   
 9. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hawa walishaonyesha udhaifu siku nyingi, wakwa mazoeatu. Ndo maana hata ruksa alishambuliwa. Sasa majukumu yao ni nini? Lakini tatizo ni mtoto wa mjomba, wa makamba, na nani vilee...hata hawana elimu maalumu ya usalama
   
 10. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pia alitakiwa apelekwe shule ya usalama wa taifa, atakuwa mtumishi makini sana
   
 11. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Jamani hii ni issue sensitive sana, wananchi wanajaribu effectiveness ya watendaji wetu kila sehemu, hakuna palipo na usalama. Hivi angekuwa amejifunga mabomu na mkuu wa kaya yupo ingekuwaje?

  Hii inadhibitisha kwanini Mzee Kichaka alipokuja wakaweka ulinzi mpaka juu ya paa maana wanawajua walinzi wetu walivyo lazy kiasi kuwa Al-Kaeda wangeenda mpaka chumbani kwake.
   
 12. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #12
  May 9, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Mkuu daima mambo huwa tofauti na uhalisia wenyewe. Inasikitisha, binafsi sikufikiria hata wangempeleka mahakamani. Anastahili pongezi kwa kuwaonyesha penye udhaifu ambapo wanatakiwa kurekebisha mara moja.
   
 13. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  yap yap yap ee bwana enhee! hii ndiyo Tanzania!
   
 14. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hata hivo kulingana na majibu ya huyo mtu anaye itwa kibaka inaonyesha si mwizi hata, na huenda ni shushu tu, kwani ua tu ndo limuingize ikulu kuiba tena la elfu 5? Nadhani alikuwa kazini, na ujumbe ama jukumu lake limekamilika kwahiyo hao askari wa ikulu wajiandae kibarua kuota nyasi very soon!
   
 15. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  hivi wanaolinda pale ni polisi wa kawaida au walinzi wa rais, au wote? na criteria zipi zinafuatwa kuwapata hawa watu?
   
 16. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mdau

  Wanaolinda pale ni Ndugu zake JMK ama kutoka Msoga kijijini, Bagamoyo au Rufiji kwa wajomba. Si kla mtu anayekwenda pale wanamjua?
  In the worst case scenario wanaweza kuwa wametoka Lindi kwa akina Salma.

  End this thread!!
   
 17. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Waandishi wa magazeti yetu mimi wananiacha hoi sana, kichwa cha habari unamuita mtu kibaka, kwenye habari yenyewe unampandisha cheo na kumpa ufanya biashara!!
  This is an embarassment kwa wote wanaouhusika na ulinzi hapo ikulu, i'll be very suprised kama wao wenyewe hawatawajibishwa. Bwana Ally Nassoro alipaswa apewe zawadi kabisa badala ya kuburuzwa mahakamani, amewasaidia kuonyesha jinsi utendaji wao ulivyo mbovu, this would have cost them a fortune kama wangetumia consultant!
   
 18. I

  Iddi Rajab Member

  #18
  May 9, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo Ally Nassor Hastahili kuitwa Kibaka na wala hana Shitaka la kujibu.
  Anachostahili ni Kupewa Tuzo ya Uchunguzi na Kupelekwa "Kijitonyama" pale ziziniiii ! akapate mafunzo sahihi maana alichokifanya ni kwa manufaa ya Usalama na Kiongozi wetu wa nchi.
   
 19. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sure huyo jamaaa hastahiri kufungwa wala kuhukumiwa kwani alikuwa anafanya utafiti na kaprove hakuna security pale
   
 20. kui

  kui JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2009
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 6,478
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  Very, very true!
   
Loading...