Kibaha, Pwani: Mtoto ajinyonga baada ya mama yake kumtuhumu kuiba Tsh. 5000

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mtoto wa kike mwenye miaka 14 mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Mtongani amejinyonga hadi kufa nyumbani kwao Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani baada ya mama yake mzazi kumtuhumu kuiba Sh5,000.

Akizungumza leo Jumatano Mei 26, 2021 Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo limetokea juzi Jumatatu Mei 24, 2021 na uchunguzi ulipofanyika ilibainika chanzo cha kifo kutuhumiwa kuiba kiasi hicho cha fedha.

"Ni kweli tukio hili limetokea lakini sisi Jeshi la polisi tulipofanya uchunguzi wetu tukabaini huyu mtoto aliamua kujitoa roho kwa sababu mama yake mzazi, Ashura Selemani alimtuhumu kumuibia pesa ambayo ilikuwa ya mama huyo.”

“Tunamshikilia mama huyo pamoja na baba mlezi (jina linahifadhiwa) kwa mahojiano zaidi,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Ukute huyu mtoto alikuwa na stress za mapenzi, mchumba ake ambae ni boda boda mnyoa kiduku ni kichomi, plus kusingiziwa wizi ndo akaamua ajimalize tyuuh.

So , apumzike kwa amani mpendwa.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Mtoto wa kike mwenye miaka 14 mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Mtongani amejinyonga hadi kufa nyumbani kwao Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani baada ya mama yake mzazi kumtuhumu kuiba Sh5,000.

Akizungumza leo Jumatano Mei 26, 2021 Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo limetokea juzi Jumatatu Mei 24, 2021 na uchunguzi ulipofanyika ilibainika chanzo cha kifo kutuhumiwa kuiba kiasi hicho cha fedha.

"Ni kweli tukio hili limetokea lakini sisi Jeshi la polisi tulipofanya uchunguzi wetu tukabaini huyu mtoto aliamua kujitoa roho kwa sababu mama yake mzazi, Ashura Selemani alimtuhumu kumuibia pesa ambayo ilikuwa ya mama huyo.”

“Tunamshikilia mama huyo pamoja na baba mlezi (jina linahifadhiwa) kwa mahojiano zaidi,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
Polisi wamegundua kuwa amejinyonga.

Polisi wanawashikilia wazazi kwa uchunguzi. Ina maana polisi siku hizi wameajiri waganga wa kienyeji kuwapigia ramli kisha wao wanaenda kufanya provinhlg ya hiyo ramli?

Kuna mtu ameelewa hii trend kweli?
 
Back
Top Bottom