DOKEZO Kibaha: Baba adaiwa kumbaka binti yake. Polisi na ndugu wamkingia kifua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Baba mmoja aliyefahamika kwa majina kama Dickson Chilongola anadaiwa kumbaka binti yake wa miaka 10 hata hivyo baadhi ya Polisi wanatuhumiwa kumlinda na sasa mshukiwa kwa sasa yuko nje kwa dhamana mbali na kuwepo kwa Ushahidi wa daktari kuwa binti huyo alifanyiwa unyanyasaji wa kingono

Tukio hilo liliripotiwa kituo cha Polisi cha Mlandizi ambako washtaki walichukuliwa maelezo lakini waliopeleka maelezo waliitwa ili kusaini maelezo mengine ambayo waliambiwa maelezo yao ya awali kituoni hapo 'yalikosewa kidogo'.

Baada ya tukio hilo, mbakaji aliachiwa na Polisi na tangu kutokea kwa tukio hilo hadi sasa hakuna kinachofahamika kuendelea zaidi ya danadana za hapa na pale.

Aidha, familia hiyo iliyokuwa inaishi pamoja kwa sasa wametengana, na Ushahidi wa vitisho upo ukionesha ndugu wa mbakaji wamekuwa wakimpa mama wa mtoto huyo.

Natoa wito kwa Vyombo vya Dola kuchukua hatua dhidi ya tukio hili kwa kuwa binti ameshaathirika kisaikolojia kufuatia tukio hilo na mama mzazi anaonekana kuwa kwenye hali ya kutishiwa maisha.
 
kama kuna kama ushahidi upo wa dakitari upeleke mahakamani lakini pia uwenda kuna fitina hili jamaa afungwe mkewe achukue nyumba kama hipo hiyo ndio akili ya wamama wengi
 
Duh aiseee inahuzunisha sana,mtoto keshaharibiwa maisha. Team kataa ndoa mbeleni watamsimanga hana bikra daah
 
Back
Top Bottom