Kibaha: Afungwa miaka 30 jela kwa kukutwa na bangi

Adam-Saffi

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
394
305
AFUNGWA MIAKA 30 JELA KWA KUKUTWA NA BANGI - Ukiiba mabillion ya serikali utafungwa miezi miwili

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Pwani (Kibaha) imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Ridhiki Omary Marimbwa kwa kosa la kusafirisha kilo 21.86 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Hukumu hiyo ilitolewa tarehe 29 mwezi Julai 2021 na hakimu Mhe. Joyce Mushi baada ya mtuhumiwa kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha Dawa za kulevya aina ya bangi

Akisoma hukumu hiyo mheshimiwa Joyce Mushi amesema kwamba, upande wa Jamhuri umethibitisha kosa hilo pasi na kuacha shaka hivyo imemtia mshtakiwa hatiani. Kwa kuwa, makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya yamekithiri mkoani Pwani, hana budi kumpa mshtakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Wakati akijitetea mshtakiwa aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani ana familia yenye watoto wadogo wanaomtegemea.

Pamoja na hukumu hiyo Mhe. Mushi aliamuru kutaifishwa kwa pikipiki iliyotumika kutekeleza uhalifu huo pamoja na kuteketezwa kwa bangi iliyokamatwa.

Mshtakiwa alikamatwa tarehe 18 mwezi Agosti mwaka 2020 kwenye hifadhi ya wanyamapori ya Selous mkoani Pwani akisafirisha dawa hizo.

Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya mwaka 2015 kama
 
MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Pwani (Kibaha) imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Ridhiki Omary Marimbwa kwa kosa la kusafirisha kilo 21.86 za dawa za kulevya aina ya bangi.
Wale waliokutwa na shehena ya madawa ya kulevya ya heroin yenye uzito wa karibu tani mbili wakati wa kimbunga JOBO wamefungwa miaka mingapi? Kama bado kesi yao inaendeleaje?

Sheria ni msumeno inakata kote kote! Kwa hiyo sitegemei ikate bangi iache heroin wakati yote kisheria yanaitwa madawa ya kulevya.
 
Huyo mfungwa utakuta hata ajui Bangi inaoteshwaje, Polisi wanatakiwa wawasake wakulima wa bangi siyo kuwakamata watumiaji, Wazalishaji wa Bangi ndio wakusakwa.
 
Mahakimu wetu wana uwezo mdogo sana wa reasoning.

Yaani jambo lenye madhara kidogo wanatoa hukumu kubwa na jambo lenye madhara makubwa kwa jamii kwa jamii wanatoa hukumu ndogo.

Kwa mfano kuna wale wanaosafirisha madawa ya heroin kutoka nje bado wanapeta tu mitaani au wakishika wanaambiwa wachague kifungo cha miaka 5 au walipe faini ya milioni 5, kuna mafisadi waliokwapua mabilioni ya wananchi wanapeta tu mitaani, mtu kama sabaya ametenda makosa makubwa na kuleta madhara makubwa kwa jamii ila hukumu yake ikitoka mtashangaa wenyewe.

Labda watuambie kwamba hukumu zao zinatolewa kulingana na kiwango cha umaskini wa mtuhumiwa husika.
 
Huyo mfungwa utakuta hata ajui Bangi inaoteshwaje, Polisi wanatakiwa wawasake wakulima wa bangi siyo kuwakamata watumiaji, Wazalishaji wa Bangi ndio wakusakwa.

Tatizo ni wabunge wanaotunga sheria Kali pasipo kusoma na kuitafakari madhara yake.

Wakati nchi zingine zimeanza kuruhusu tafiti na kilimo Cha bangi huku tz ni kosa la jinai. Jera watajaa wauzaji na wasafirishaji wa madawa ya kulevya na wabakaji kwa kuwa vifungo vyao ni vilefu miaka 30.
 
Adhabu za Mahakama zetu Zunategemea UTASHI wa HAKIMU
ukitakatisha pesa Bil 1 unalipa Faini Mil 1.5 ukikutwa na bangi Miaka 30
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom