Kiatu cha Rais Magufuli kinaweza kumtosha Mh.Majaliwa

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,873
14,302
Wakuu habari za Leo? Natumaimi mu wazima wa afya njema.

Baada ya Mh .Magufuli kumaliza muda wake 2025 Tanzania itapata pengo kubwa ambalo lina hitaji umakini ulio tukuka katika kuona namna ya kuliziba, hii ni kutokana na utawala wa Mh.JPM kuwa na machungu ya raslimali za nchi yetu ,kama nchi hatuna budi kuangalia mtu ambaye atakuwa makini na mwenye falsafa kama za JPM na ambaye atakuwa tayali kupigana kufa kupona kwa masirahi mapama ya taifa lake.

Binafsi namuona Mh. Majaliwa kama mtu makini na mwenye umakini wa hali ya juu sana ambaye akipewa viatu vya JPM vitamtosha pasina shaka,the man is so calm ,so wise and not egoist.pia ni mtu mwenye uchungu wa rasilimali za nchi yake,

Mungu ampe kheri aweze kuvivaa viatu vya JPM ili atufikishe katika nchi ya maziwa na asali

Wapinzani wasubiri kwanza labda baada ya miaka 100 mbele ndo wanaweza kufikiliwa kukabidhiwa hii nchi.

Ni hayo tu.

Majaliwa for 2025-2030

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chezea JPM wewe! Atampata anayeweza kuendeleza falsafa yake! Anaweza asiwe Majaliwa!
 
Kila mtu amepewa utashi wake na Mungu. Hawezi kuwa kama JPM ila atakuwa na namna yake ya kuongoza ambayo itamtofautisha. Inaweza kuwa nzuri kupita ya JPM ama kuwa mbaya zaidi.
 
Wajinga sisi, kuwaza kutawaliwa tu, yani kuwaza tu nani kesho atakuwa kiongozi wangu, na sio namna gani nitakuwa kiongozi ama kufanikisha maisha ninayoyataka!

Mabwege kweli sisi tunaowaza tu nani atatuongoza!
 
Kwa hiyo hutaki kutawaliwa? Kuna nchi gani ambayo haina mfumo wa uongozi ?
Wajinga sisi, kuwaza kutawaliwa tu, yani kuwaza tu nani kesho atakuwa kiongozi wangu, na sio namna gani nitakuwa kiongozi ama kufanikisha maisha ninayoyataka!

Mabwege kweli sisi tunaowaza tu nani atatuongoza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
digba sowey,
Unasemaje 2025
kwani uchaguzi ushafanyika?

Na kila siku huwa anasema ile kazi ni ngumu sana. Ki busara anatakiwa kupisha kiti na kuwaachia wanaoiweza waifanye.
 
Umemchoka wewe na nani? Mbona unaongelea nafsi za wengine,wewe uko kwenye fikra zangu,mbona Mimi naona kama ingeruhusu tungemfanya jpm life president kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli nyani haoni.......! Unamkosoa mwenzako kwamba anaongelea nafsi za wengine, na wewe ukaingia keenye mtego huo huo. Unasema kama ingeruhusu tungemfanya jpm life president kabisa. Sasa na wewe nikuulize mngemfanya awe life president wewe na nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu hizi siasa za kurithishana sio nzuri jamani sote tunafahamu majaliwa ni ndugu yake Mama salma Kikwete,Majaliwa hakuwa chochote ndani ya CCM na Serikalini ni upendeleo wa kikwete ndio maana tunamuona hapo leo!
Kumpa majaliwa nchi baada ya JPM, ni sawa na kikwete kuendelea kuongoza kwa muongo wa 3 mfululizo!.
 
Wakuu habari za Leo? Natumaimi mu wazima wa afya njema.

Baada ya Mh .Magufuli kumaliza muda wake 2025 Tanzania itapata pengo kubwa ambalo lina hitaji umakini ulio tukuka katika kuona namna ya kuliziba, hii ni kutokana na utawala wa Mh.JPM kuwa na machungu ya raslimali za nchi yetu ,kama nchi hatuna budi kuangalia mtu ambaye atakuwa makini na mwenye falsafa kama za JPM na ambaye atakuwa tayali kupigana kufa kupona kwa masirahi mapama ya taifa lake.

Binafsi namuona Mh. Majaliwa kama mtu makini na mwenye umakini wa hali ya juu sana ambaye akipewa viatu vya JPM vitamtosha pasina shaka,the man is so calm ,so wise and not egoist.pia ni mtu mwenye uchungu wa rasilimali za nchi yake,

Mungu ampe kheri aweze kuvivaa viatu vya JPM ili atufikishe katika nchi ya maziwa na asali

Wapinzani wasubiri kwanza labda baada ya miaka 100 mbele ndo wanaweza kufikiliwa kukabidhiwa hii nchi.

Ni hayo tu.

Majaliwa for 2025-2030

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona mapema mno? Au unamchulia kifo rais wetu mpendwa mapema?
 
Mnajichosha 2025 kisiasa ni mbali sana huwezi kuipredict sasahivi, tupige kazi mengine tumwachie Mungu
 
Back
Top Bottom