Kiapo: Nitafanya lolote ili niondokane na umaskini

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,640
35,954
Zamani nikiwa mwinjilisti mdogo niliyejaa moto nilisema kuwa matatizo makuu yanayowakabili wanadamu wa kizazi cha leo ni matatu; Dhambi, umaskini na magonjwa.

Sasa hivi nimegundua kuwa ile arrangement yangu haikuwa sahihi na kwamba natakiwa niyapange hivi ;

1.Umaskini
2.Magonjwa na
3.Dhambi.

Umaskini ndio baba mzazi wa magonjwa na Dhambi.

Leo wakati nakwenda nyumbani nikitokea Pugu kwenye mishe za kusimamia ujenzi wa nyumba yangu nimehangaika sana juu ya usafiri. Nimeona watu wanavyopigana kisa daladala.
Nikajisemea moyoni kuwa adui nambari moja sasa ni umaskini na kuanzia hii leo afe kipa afe beki umaskini lazima niukimbie.

Nitafanya juu chini umaskini unikimbie. Daladala nipande kwa emergency tu, chakula nile kile ninachokipenda tu na si maadamu tu kipo mbele yangu.

Note : Ninaposema nitafanya lolote sijajumuisha matendo ya kihayawani kama ushoga, ujambazi n.k.
 
Lolote ulilomaanisha ni lipi mkuu nijifunze toka kwako
Sasa hapa dhana ya lolote tunstofautiana kulingana na mazingira.
Mwingine anamaanisha yako tayari hata kuwa mvuvi, kwenda kufanya kazi ngumu za migodini n.k. Huku mwingine akiamua kuangia kwenye uigizaji, ubunifu n. K
 
Kumbuka pia maandiko yanasema
"Ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa Mungu"
 
Kumbuka pia maandiko yanasema
"Ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa Mungu"
Maskini wa leo ni rahisi kuingia jehanamu kuliko matajiri. Why?
Maskini furaha huipata kwa awamu kama vile mgao wa umeme miaka ya 2000 Dar.
Ile furaha anayoikosa maskini ndio funguo ya amani na amani huleta uzima(mbingu)
 
Zamani nikiwa mwinjilisti mdogo niliyejaa moto nilisema kuwa matatizo makuu yanayowakabili wanadamu wa kizazi cha leo ni matatu; Dhambi, umaskini na magonjwa.
Sasa hivi nimegundua kuwa ile arrangement yangu haikuwa sahihi na kwamba natakiwa niyapange hivi ;
1.Umaskini
2.Magonjwa na
3.Dhambi.
Umaskini ndio baba mzazi wa magonjwa na Dhambi.
Leo wakati nakwenda nyumbani nikitokea Pugu kwenye mishe za kusimamia ujenzi wa nyumba yangu nimehangaika sana juu ya usafiri. Nimeona watu wanavyopigana kisa daladala. Nikajisemea moyoni kuwa adui nambari moja sasa ni umaskini na kuanzia hii leo afe kipa afe beki umaskini lazima niukimbie.
Nitafanya juu chini umaskini unikimbie. Daladala nipande kwa emergency tu, chakula nile kile ninachokipenda tu na si maadamu tu kipo mbele yangu.
Note : Ninaposema nitafanya lolote sijajumuisha matendo ya kihayawani kama ushoga, ujambazi n.k.
"Dhambi, umaskini na magonjwa".

Zamani ulikuwa na akili kuliko sasa. Mpangilio huo ndio halisi tangu kuumbwa kwa ulimwengu hadi leo, dhambi ndio chanzo cha matatizo yote, vingine vinafuata, umaskini na halafu magonjwa na mwisho kifo. Hata vitabu vitakatifu vinatuambia hivyo, mshahara wa dhambi ni mauti.
 
Umaskini unaweza kufanya ushindwe kupambana na hao maadui wengine.
Ukiwa maskini unakosa msimamo ni rahisi kuingia dhambini.
Ukiwa maskini inakuwa ngumu kukabiliana na maradhi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom