Elections 2010 Kiapo cha urais kisivyo thamani!

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,660
1,802
Kwa nini rais anaapishwa Tanzania?
Miye naona ni kupoteza wakati tu, na ni kutekeleza 'routine' tu. Maana ya kiapo ni kuwa pindi rais anapokiuka hicho alichokiapa, mahakama itakuwa na dalili. Pia, mwananchi yeyote anaweza kumburuza mahakamani akiashiria ahadi ya kiapo aliyoichukua kama 'kithibitisho'
Hebu oanisha maana hiyo na yanayotokea Tanzania. Kwanza, siamini hata huyo rais mwenyewe anapoapa yuko serious. Hii ni kwa sababu tumeona ukiukaji wa mara kwa mara, tena kwa kusudi na dhereu, wa katiba yetu, na hakuna lolote linalotokea. Sasa nasema, si afadhali mkatupumzisha na 'show' hii na in the process tukaokoa mamilioni ya fedha yanayotumika bila sababu yeyote ya maana?
 
Back
Top Bottom