Kiapo Cha Udaktari wa Tiba ya Binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiapo Cha Udaktari wa Tiba ya Binadamu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 2mbaku, Jul 17, 2012.

 1. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwanza inua mkono wako wa kulia ulishwe kiapo kwamba unakubali kwa yakini:

  1.Kwamba sikuzote utafanya kazi ya udaktari kwa ujuzi na uwezo wako wote kwa ajili ya mema, afya na usalama wa watu wote watakaofika mbele yako kwa nia ya matibabu.

  2.Kwamba hutafanya kwa makusudi wala kwa nia kitu chochote au kuwapa kitu chochote cha kuwadhuru au cha kuwaondolea heshima.

  3.kwamba hutatoa siri yoyote imhusuyo mgonjwa uliyosikia au kuigundua katika uwezo wako wa udaktari kazini bila sababu rasmi.

  4.Kwamba hutatumia njia za siri za matibabu wala kuwaficha madaktari wenzio namna yoyote ya matibabu utakayogundua kuwa ni matibabu safi.

  5.Kwamba hutajitangaza wala hutakubali utangazwe kwa nia ya kujivutia wagonjwa.

  6.Kwamba katika uhusiano wako na madaktari wenzio siku zote utajiweka katika mwenendo safi wa heshima kama inavyotakiwa na umoja wa kazi muhimu ya udaktari.


  Basi ukitimiza hivyo, Mungu pamoja na Umma watakutukuza.

  Hebu tujadili kiapo hiki bila ushabiki, hasa kifungu cha 1,2 na 6. Je katika vifungu hivyo, kuna chochote kinamzuia daktari kugoma directly au indirectly?
  Vipi kuhusu umoja wa madaktari, je kifungu cha 6 hakiwahukumu wale wote ambao waliwasaliti wenzao na kuendelea na kazi?
  Nawasilisha>>>>
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  siasa zimeharibu kazi za WITO
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  si wachungaji wala walimu(wa sasa) wanaozingatia neno WITO.....wenyewe wanakwambia ni KAZI KAMA KAZI NYINGINE
   
 4. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Zipi ni kazi za wito katika nchi yetu ya Tanzania?
   
 5. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,177
  Trophy Points: 280
  Hatuna kazi za wito, wanasiasa wamevunja katiba mara ngapi waliyo apa kuilinda?
   
 6. B

  BULOLE BUKOMBE JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  polisi
   
 7. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  watu wanapotosha wengine kisa watz ni wavivu wa kusoma na kujua maana ya wito. Mbona nchi zingine hatusikiagi hayo mambo ya wito. Wito kwa doc ni pale anapoangalia k yako, mku...u wako and all your body matatizo aafu akameza mate. Msifikiri kazi rahisi, sometime hata mgonjwa anaona kinyaa ila we unatakiwa ushike,unuse na usafishe. Siyo kazi rahisi mwanamke/mwanaume amekuja ukamvua nguo na kupoteza hisia za kibinadamu ambazo huwa zinatoke haraka kuliko hisia nyingine. Ndo maana wengine huwa wanashindwa kuvumilia na kubaka!! Huo ndo wito wa mtu unaotakiwa uulizwe. Kuamshwa usiku kwenda kuhudumia mtu, kumhudumia hata jambazi aliyewahi kukuibia bila kinyongo. Kumhudumia mtu uliyemshauri asitoe mimba ila kwa akili yake timamu akaamua kuitoa na complications zikatokea. Kushinda na mtu ambaye jamii inamchukulia kama kichaa na kumkimbia, lakini we inabidi umchukulie kama mtu wa kawaida. Siyo kazi rahisi!! Polisi wenyewe wito umewashinda ndo maana wamegeuka majambazi, wezi, wakabaji, wauzaji wa madawa ya kulevya nk, yaani kila aina ya kosa polisi wamo? Hivi hakuna wenye barua iliyoandikwa na yule polisi wa morogoro kuelezea kundi la kina MSANGI wanavyojihusisha na ujambazi?
   
 8. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Aliyeanzisha mada kaorodhesha yaliopo ndani ya kiapo cha Udaktari.
  Inaelekeawewe ni daktari basi tusaidie kukijadili kiapo hiki na kuona kama kinakidhi haja.
  Ukila kiapo na ukaenda kinyume na kiapo unafanya kosa.
  Ni vizuri kukijua kiapo ili kama hukubaliani nacho basi usikishiriki.
  Kila kazi ina miiko yake hata polisi wanapokamata mamilioni wanatakiwa wayafikishe na wakienda kinyume wanashtakiwa hivyo hivyo wake zetu wanpokuja kwako unachungulia na unavumilia ndio miiko ya kazi ya kazi yako.Waswahilihusema usisafirie nyota ya mwenzio.
   
 9. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Safi, umeelezea vitu ambavyo ni sehemu ya wito wenyewe.
  Mchango wako kuhusu hilo la wito ni lipi? Yeye kaainisha mambo yanayohusu wito wa daktari.
   
 10. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Well said mate.....
   
 11. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Mchango wangu uko wazi kabisa.Adhere to your ethical principles.
  Tufuate maadili ya kazi zetu ili tuwe na utendaji mzuri kazini.
  Kuna madudu mengi yanayotokea nchini ikiwemo wizi na ufisadi ambao unawaathiri maskini wengi lakini kwa kufuata kiapo cha kazi ya Udaktari hakuna fursa ya kuacha wagonjwa wafe.
  Wizi na madudud yote ya wanasiasa na wenzi wao hayahalalishi madakatari kuacha wagonjwa,tutafute njia nyingne za kukabiliana na hilo ikiwemo kujiunga na vyama makini vya upinzani na kusaidia kuwaelimisha wananchi.
  All the time tuhakikishe ya kuwa wananchi wapo upande wettu na mabadiliko yatatokea.
   
 12. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Tukifanya haya uliyosema, naimani kubwa tutakuwa tumeondoa dharau kwenye professional za watu!! Na hili linawezekana kama watu wenye professional zao kama madaktari, walimu, wahandisi na wengine tukiungana na kuacha fikra potovu na uroho wa madaraka tutakomesha hii miungu watu wasiokuwa na chembe ya huruma. Kuhusu hilo la Professional Ethics, ni kweli kabisa kama watu na professional zao wataamua kustick/ku-adhere to their professional ethics & conduct ufisadi, wizi pamoja magumashi yatamaa yatapungua tu. However, where do we start buddy? talking to online media & waiting for miracle to happen is just another failure. We may join the good promising political parties, still we have so much to do.
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kazi yoyote ni wito, lakini kwa kuwa ni kazi na inahusu pande mbili, mwajiri na mwajiriwa, lazima kila upande utimize wajibu wake vilivyo. Tusitumie neno wito kama pingu ya kuwafunga waajiriwa wafanye kazi katika mazingira magumu. Mfano kiapo cha kwanza, daktari atafanyaje kazi kwa usalama wa wagonjwa bila ya nyenzo? Pia kuna suala la ustawi wa madaktari, watafanyaje kazi ikiwa maslahi yao hayatiliwi maanani?
  BULOLE BUKOMBE amesema polisi ni kazi ya wito, ni kweli, lakini polisi kama madaktari, ili kutekeleza kazi zao vyema, wanahitaji nyenzo na maslahi bora.

  Kuhusu suala la usaliti, Tanzania ndio zetu hizo. Ijumaa iliyopita serikali ya Uhispania iliamua watumishi wote wa umma wasilipwe posho za mwisho wa mwaka. Hapo hapo yakafanyika maandamano nchi nzima hadi usiku wa manane. Cha kushangaza/kufurahisha, askari waliotakiwa "kulinda usalama wa raia" wakavua kofia zao na kujiunga na maandamano.

  Chama cha Umoja wa Maaskari kilisema, "Hata polisi tuna kiwango chetu cha uvumilivu na utii, hapa serikali imezidi". Jana serikali sio tu ililazimika kufuta uamuzi wake wa Ijumaa, bali kupunguza mishahara ya Raisi, mawaziri na wabunge kwa asilimia 7. Nina hakika kama maandamano hayo ya wafanyakzi wa umma yangefanyika Tanzania, poliCCM wetu wangeua.
   
 14. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Lete in an oroginal format bana ngeli ya genge
   
 15. C

  CAY JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Basi madaktari wapewe wito card ili wakienda kutafuta mahitaji yao waitumie hiyo wito card kupata mahitaji yao!
   
 16. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hiki Kiapo kimechakachuliwa weka hapa kama kilivyo ndipo tukijadili
   
 17. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hicho ndo kilichotafsiriwa na wanachoapa graduates siku ya mahafali pale muhas. Original hippocratic oath imetafsiriwa kwa lugha za mataifa mbali mbali with some modifications.
   
 18. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  google hippocratic oath uisome. Kuna version mbili, original na modified.
   
 19. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe ni mchochezi,kwanini umeacha baadhi ya vifungu kwa maslahi yako binafsi????
  au unadhani ni wewe pekee ndio unajua icho kiapo.unatumika wewe
   
 20. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  umeweka vipande vipande ukaacha vipengele vingine ili uwadanganye wajinga wenzako wenye uwezo mdogo wa kufikiri na kuchambua mambo
   
Loading...