Kiapo cha Rais wa Marekani kina maneno machache (35) tofauti na cha Rais wa Tanzania, siyo lazima kusema "Mungu nisaidie"

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,058
2,000
Wiki mbili zilizopita nimekuwa nikifuatilia kwa karibu mahubiri ya mchungaji Matsai wa KKKT kimara kuhusu viapo.

Uelewa wa mahubiri yale ukanivuta kujifunza namna viongozi mbalimbali wanavyokula viapo vyao vya utumishi nikianzia wa hapa nyumbani na jana nilifuatilia kiapo cha Rais Joe Biden wa Marekani.

Bado natafakari kwanini Rais wa Marekani anaapa kuitumikia Ofisi ya Rais kwa uadilifu tofauti na marais wa nchi nyingine ambao huapa kuwatumikia Wananchi kwa uadilifu.

Je, Ofisi ya Rais ndio Wananchi?

Lakini kitu kilichonifurahisha ni maneno machache yaliyomo kwenye kiapo cha Rais wa Marekani tofauti na kiapo cha Rais wa Tanzania.

Lakini nimeshangazwa kwamba Rais wa Marekani siyo lazima aseme "Ewe mwenyezi Mungu nisaidie" anapohitimisha kiapo chake.

Nawatakia Alhamis yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
26,676
2,000
Bado natafakari kwanini Rais wa Marekani anaapa kuitumikia Ofisi ya Rais kwa uadilifu tofauti na marais wa nchi nyingine ambao huapa kuwatumikia Wananchi kwa uadilifu.
Mnaapa halafu mnakuwa madikiteita, kuua watu, kupoteza watu, sandarusi za maiti coco beach. Kuwabambikia watu kesi
TO CROWN IT ALL, KUVUNJA KATIBA WAZI WAZI MLIYOAPA KUILINDA, kama anavyofanya Ndugai na akina Halima!
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,372
2,000
Na hili neno kwenye Pesa note za Marekani linalosema IN GOD WE TRUST linamaanisha nini? Wameliondoa neno Mungu kwenye kiapo lakini wakaliweka kwenye pesa why?

1611207219100.png
 

SARO OGONI

Member
Nov 29, 2020
34
125
URAIS ni taasisi inayoundwa na uwakilishi wa wananchi wote.

Hivyo kimantiki sioni tatizo aidha ofisi ya RAIS au WANANCHI...yote heri. Shida inakuja ktk kiviishi na kuvitumikia viapo hivyo.

Hatumaanishi, tuna malengo yetu tofauti hususani tamaa ya kujilimbikizia, ubinafsi, kutokuwajibika
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,058
2,000
Mnaapa halafu mnakuwa madikiteita... kuua watu, kupoteza watu, sandarusi za maiti coco beach. Kuwabambkia wau kesi
TO CROWN IT ALL, KUVUNJA KATIBA WAZI WAZI MLIYOAPA KUILINDA......kama anavyofanya Ndugai na akina Halima!
Umechanganya sana mambo, tulia upate kisusio kwanza!
 

Del a boss

JF-Expert Member
Apr 4, 2013
328
500
Hii nchi toka 2015 hadi leo mpaka kesho imekuwa kama kikao cha familia. Hakuna linalo fanyika kwa 100% lakini utasikia mimi ni raisi wa wanyonge. Ana aapa kuilinda katiba lakini kwenye uchaguzi kavunja sheria mwishoni unasikia "eeh Mungu nisaidie" labda Mungu wa Shattle
 

LGF

Senior Member
Dec 6, 2020
141
225
Asante sana, maoni yako mazuri. Sasa kwa nini usiende huko? Washauri watuige, waongeze maneno yetu. Au ubaki hukohuko hawahitaji Mungu.
 

Dickson Edwin Mgaya

JF-Expert Member
Apr 2, 2020
216
500
Saa nyingine huwa naona kumhusisha Mungu kwenye viapo vyetu simply ni unafiki na dhihaka kwa Mungu kwani viapo vyenyewe vimebakia tu kama desturi, vinakyiukwa mchana kweupe bila hata hofu ya jina la Mungu. So ikiwezekana na sisi tuwe na viapo kama vya Amerca kuepuka ghadhabu ya Mungu.
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,438
2,000
Usipoambiwa Kwa sasa! Huwenda ukazidi kuwa mjinga zaidi!

Kwa hiyo unatamani kiapo cha Raisi wa Marekani kiwe kinafanywa na watu wote siyo?

Acha dharau kijana
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,438
2,000
Hii nchi toka 2015 hadi leo mpaka kesho imekuwa kama kikao cha familia. Hakuna linalo fanyika kwa 100% lakini utasikia mimi ni raisi wa wanyonge. Ana aapa kuilinda katiba lakini kwenye uchaguzi kavunja sheria mwishoni unasikia "eeh Mungu nisaidie" labda Mungu wa Shattle
Yafanyike au yasifanyike, yanakuhusu nini wewe?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom