MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Je watu wana tilia maanani wanacho kiapa kanisani? Je wanajua wana apia nini? Maana una kuta mtu ana kula kiapo cha ndoa lakini anakuja kufanya opposite. Mtu ana sema kwenye shida na raha lakini wakati wa shida ana kimbia au kulala mika. Mtu anasema kwa utajiri au umaskini lakini pale mumewe anapo kuwa masikini haishii kutamani vya wengine. Mtu ana apa kuwa mwaminifu lakini ana kuwa msaliti wa ndoa. Mtu ana sema mpaka kifo kitu tenganishe lakni wana kuja kutenganishwa na kitu kingine.
Kiapo kile mtu huapa mbele ya Mungu na mashahidi. Kiapo hiki ni kama mkataba na utamkapo maneno yale ina maana ume ya kubali. Je kwa nini uape kitu ambacho hauwezi kutimiza? Kwa nini watu wasiandike viapo vyao wenyewe badala ya kulazimika kukubaliana na hivi vilivyo sha andikwa wakati wengine wanajua hawa wezi kutimiza masharti hayo?