kiapo cha mwanzo wa uhusiano wa Mapenzi na Mwenzako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kiapo cha mwanzo wa uhusiano wa Mapenzi na Mwenzako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Sep 18, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Usiusaliti moyo wako

  Leo nataka tuzungumzie kiapo mwanzo wa uhusiano, ambapo wengi hawakifahamu au hawajui kinatumika wakati gani. Wengi wamevunja viapo vya mapenzi na kujikuta wakigeuka mateso kwa wenzao.


  Siku zote mapenzi ni mkataba wa watu wawili waliokubaliana kuwa kitu kimoja kuishi katika hali ya shida na raha. Wapendanao wa kweli huishi katika mkataba ambao mmoja akienda kinyume huwa msaliti.


  Mapenzi ya wawili ni mkataba wa makubaliano ambayo hutengeneza katiba inayokuwa muongozo katika uhusiano wao.


  Mnapoanza mapenzi kila mtu huukubali mkataba huo na kuahidi ataulinda kwa nguvu zake zote, nguzo kuu za makubaliano huwa ni uaminifu, tabia nzuri, huruma upendo na uvulivu. Tuangalie kitu kimojakimoja ndani ya mkataba huo:


  UAMINIFU: Mpaka mnaamua kuwa mwili mmoja ina maana mmekubali kwa ridhaa yenu. Mmewaacha wengi na kuamua kuwa pamoja hivyo mnatakiwa kulilinda penzi lenu kwa kuwa waaminifu. Mmoja wenu akisaliti ni lazima kuvuruga penzi.


  TABIA NZURI: Ndiyo inayobeba uwakilishi wa mwanadamu ndani ya nyumba, ni nguzo imara ambayo itakufanya usimame popote kwa kujiamini. Wengi hukosea wanapojiona wana sura umbile zuri au fedha, hivyo kuanza kuwanyanyasa wenzao kwa kujivunia walivyonavyo wakisahau kuwa hakuna kiumbe kilichoumbwa kwa ajili ya kukasirishwa.


  HURUMA: Ndani ya uhusiano huruma ni kitu muhimu sana kwa wapenzi kwa vile ukiwa na huruma huwezi kumuumiza mwenzako. Nyumba yenye huruma kwa wapendanao hudumu milele. Ambaye hana huruma hufanya jambo lolote bila kujali maumivu ya mwenzake.


  UPENDO: Huu ndiyo unaobeba kila kitu kwa vile mwenye upendo ana huruma, ni mvumilivu na tabia njema ndiyo asili yake. Wote mkiwa hivyo hata familia yetu itakuwa yenye tabia nzuri kwa vile nao watakuwa sehemu ya upendo kuwapenda wote.
  Hapa mara nyingi kumekuwa na tatizo kwa baadhi ya watu kuchagua wachache wa kuwapenda, hasa wanawake wamekuwa na kasumba ya kuchukia ndugu wa mume na mwisho wa siku ndoa huvunjika.


  UVUMILIVU: Huu ndiyo muhimu katika maisha yetu ya kila siku, wengi wasio wavumilivu wamekuwa wakitengana na wenzao. Katika maisha ya mwanadamu kuna vitu ambavyo tunatakiwa tuvumiliane kwa vile wanadamu ni viumbe ambao hawajakamilika.


  Kukosana ni sehemu ya maisha lazima mvumiliane, mtangulize kusameheana na kuyasahau yaliyopita. Yapo ya kuvumilia, lakini si yaliyovuka mipaka kwa mtu kushindwa kujirekebisha. Mwanadamu mwenye akili timamu ujifunza kutokana na makosa na kuwa tayari kukosolewa na kuomba msamaha anapokosea.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu asante sana kwa maneno yako na uchambuzi wako
  Ni kiapo kizuri sana iwapo kila upande utafuata na kutimiza kiapo hicho ila upande wowote utakaoacha kufanya hivyo ni mbaya sana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. m

  miksel Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Xafi xana thanks
   
Loading...