Kiambishi awali cha nafsi 'ni' na mchakato wa maendeleo ya taifa letu.

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
8,814
17,162
Nimekuwa nikimpuuza kwa sababu sikuwa na haitotokea nikawa na nia mbaya dhidi ya mtanzania mwenzangu yeyote kwa sababu tu mimi nina dhamana ya uongozi. Sinaga tabia hiyo.

"Naithamini tiba asili na tiba mbadala na Ndiyo maana nimeongoza Wizara ya Afya kufanya Mapinduzi makubwa kwenye eneo hili, ikiwemo kuweka utaratibu mzuri na rahisi zaidi wa kusajili watoa huduma, dawa zao, mazingira wanapotunzia dawa, wasaidizi wao, viwanda vyao, na pia kuweka mikakati ya uanzishwaji wa viwanda vya dawa za tiba asili na tiba mbadala sambamba na kufanyia utafiti dawa zao na kudhibiti ubora wa dawa zenyewe na dozi wanazowapa wateja."

"Mimi nilikuwa msimamizi nikiwapa nguvu wataalam wafanye kazi yao. Wataalamu walikuwepo, nao ana ugomvi nao 'binafsi'? Mwambieni awajibu kama dawa za tiba ya kisasa kukutwa kwenye eneo lake la kazi ilikuwa halali? Alikuwa na vibali vya kutunza zaidi ya maboksi 200 ya dawa? Alikuwa na vibali vya kutunza zaidi ya magunia 10 ya dawa za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa usajili? Alikuwa na uhalali wa kuendelea kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wateja wake wafuate dawa pale ili wasikatishe dozi? Tena kinyume na katazo la Baraza la tiba asili na tiba mbadala! Yeye yuko juu ya Serikali? Yuko juu ya Sheria? Ama anadhani anaweza kuidhihaki na kuiogofya Serikali?

Mwisho,
aende akafuatilie kisa cha mfanyabiashara wa kigiriki aliyesema ameiweka Serikali mfukoni - Mwalimu Nyerere alimfanya nini!"

Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.

Hapa nataka kuonyesha jinsi serkali ya JPM inavyofanya kazi kwa vipaumbele binafsi.Nimenukuu baadhi ya vipengele katika kanusho la Waziri wa afya DR Kigwangwala dhidi ya madai yaliyosambaa mitandaoni kuwa alisoma na Dr Mwaka.Kwa sie tuliosoma kiswahili, kiambishi ''ni'' ni kiambishi awali cha nafsi ya kwanza umoja,ambacho kinatoa taarifa ya mtenda wa jambo katika wingi wao na umoja.kwa kuangalia taarifa hiyo ya kukanusha bado inaonekana zoezi la kumshughulikia dr mwaka ni zoezi la mtu mmoja kama ambavyo wazir amejinasibu katika kutekeleza na kukamilisha mipango mengine.Na kauli hizi za kuonesha mafanikio (individual achievement)au utekelezaji wa jambo fulani zimekuwa common kwa karibu viongozi wengi wa serikali ya JPM ikiwemo ikulu yenyewe kujinasibu na kujitapa kwa lengo la kufurahisha au kujitetea mbele ya wananchi.Hili linaifanya mawaziri,RC,ma-DC,WAKURUGENZI,DAS,RAS n.kv kila siku kutoa matamko au maagizo yenye ukakasi na mawazo yao binafsi jinsi wanavyolichukulia jambo husika.Na hii yote katika jitihada binafsi kwamba anaperform na kufanya kazi na anaendana na kasi ya Rais ambaye naye ni mtumiaji nzuri wa kiambishi 'ni'.Je hakuna common goals au priorities ambazo mawaziri wetu na viongozi wetu watasema na kuanza na kimbishi awali cha nafsi ya kwanza wingi 'tu', mfano.."tumetekeleza jitihada za awali za kupeleka chanjo mahospitali'' AU ''tutahamia Dodoma mara baada ya bajeti kupitishwa'' Naamini kabisa jambo lolote la maendeleo ni mchakato unahusisha wataalamu mbalimbali wa fani au tasnia husika katika kupanga,kuratibu,kupanga bajeti,rasilimali,maelekezo na mwisho kuongoza hivyo kiongozi wa kisiasa hana budi kuuweka ushiriki na uhusika wao kwa herufi chache (mofimu) zinazounda kiambishi "tu"

Chini ni nukuu na kauli za viongozi wetu
".......Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” .........

"....Ninatoa agizo kuwa mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja Dodoma. Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba, na utekelezaji wake nitausimamia kwa juhudi zote,”

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim.
KAULI YA WAZIRI MKUU KUHAMIA DODOMA MWEZI WA TISA. ~ g sengo

Nataka nijue sababu za kitaalamu za kubadilisha mfumo wa upangaji wa matokeo kutoka kwenye ule wa Division (madaraja) kwenda kwenye ule wa GPA na kama huo mfumo una tija kwa elimu yetu,
waziri wa elimu prof.Ndalichako
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/5141-ndalichako-atoa-maagizo-mazito
 
Back
Top Bottom