Kiama posho serikalini chaja: Serikali, Bunge Mahakama wakaribia kubwaga manyanga chini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiama posho serikalini chaja: Serikali, Bunge Mahakama wakaribia kubwaga manyanga chini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Feb 18, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  POSHO za vikao ambazo mjadala wake umechukua takriban mwaka mmoja sasa, huenda zikafikia ukomo mwaka huu kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba wabunge wamepania kuzifuta katika Bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

  Habari ambazo zimelifikia gazeti hili kutoka bungeni na serikalini zinasema Tume ya Huduma za Bunge tayari imeanza kujadili suala hilo na kwamba uamuzi ni kuanza kufuta posho za vikao kwa wabunge ambazo ni Sh70,000 kwa siku.
  Taarifa za kuwapo kwa mpango huo zimekuja siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete alipokataa kuidhinisha mapendekezo mapya ya posho za vikao kwa wabunge kutoka kiasi hicho cha Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku.

  Ikiwa uamuzi huo utatekelezwa, utakuwa ni ‘ushindi’ kwa wabunge ambao waliasisi vita dhidi ya posho za vikao kiasi cha kusababisha tofauti za wazi na wabunge wenzao ambao wamekuwa wakiwatuhumu kwamba wanatafuta umaarufu wa kisiasa.

  Miongoni mwa wabunge hao ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe.

  Mwingine ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye aliwahi kuziita posho za vikao kuwa ni wizi wa kitaasisi ulioasisiwa hali ukiwa hauna tija kwa Taifa na badala yake kupoteza fedha nyingi za Serikali.

  Mmoja wa viongozi waandamizi wa Bunge ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema suala la wabunge kufuta posho za vikao tayari limeanza kujadiliwa na Tume ya Huduma za Bunge ambayo Mwenyekiti wake ni Spika Anne Makinda. “Kuanzia mwaka ujao wa fedha tunataka kuacha kabisa kulipwa posho za vikao (sitting allowance), kwa hiyo hata hiyo Sh70,000 hatutachukua itakuwa ni ziro kabisa maana tumechoka kuandamwa,” alisema kiongozi huyo na kuongeza: “Lakini wakati tukifanya uamuzi huo, serikalini, mahakamani na katika mashirika mengine ya umma nako wajiandae, hakuna bajeti yoyote ya posho za vikao itakayopitishwa na hili tutaanza kuwapa maelekezo rasmi wakati wa vikao vya mipango ya bajeti mwezi Aprili mwaka huu.”

  Spika wa Bunge, Makinda alipotafutwa juzi na jana kuzungumzia taarifa za taasisi yake kuweka mkakati wa kufuta posho hizo, simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita kwa muda mrefu bila majibu.
  Kwa upande wake Naibu Spika, Job Ndugai alipoulizwa iwapo kuna mpango wa wabunge kusimamia kufutwa kwa posho zote za vikao ndani ya Bunge, serikalini na katika Idara ya Mahakama hakukanusha wala kuthibitisha suala hilo, badala yake akashauri kwamba: “usubiriwe wakati mwafaka.”

  Alipoulizwa wakati mwafaka ni upi alisema: “Mimi nadhani suala la posho linachosha, hakuna jambo jingine la kuzungumza ina maana ni posho tu? Tumesema sana kama ni kuhusu kufutwa basi mimi nadhani tusubiri wakati mwafaka, wakati wa bajeti maana mchakato wake unaanza Aprili, tusubiri tutapata majibu mwafaka,” alisema Ndugai ambaye amekuwa msemaji wa suala hilo kwa muda mrefu sasa.

   
 2. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Je, hiyo tume ya nini sijui, wajumbe wake wanalipwa posho za vikao?
   
 3. chubulunge

  chubulunge Senior Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  posho posho posho picha bado linaendelea
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,519
  Likes Received: 19,944
  Trophy Points: 280
  kudadadeki visasi hadi kieleweke na futeni posho zenu futeni posho hadi za walimu na mkae mkijua 2015 hamrudi. si ni visasi?
   
 5. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haki ya nani wakifuta kote kuna watu wanakimbia utumishi wa umma. Kuna watu wanajua wako serikali wako kwa ajili ya posho hizo tu, ukitoa posho mishahara yao ya mwisho wa mwezi ni midogo sana unless walikimbie jiji, hawataishi tena Dar es Salaam
   
 6. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Mbona vituko?

  Mpanngo huo ulikuwepo ama ni baada ya JK kukataa kuusaini marekebisho ya posho zao?
  Kweli Tanzania,vilevile ni zaidi ya unavyoijua...
   
 7. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Muasisi wa swala hili ni Dr. SLAA.
   
 8. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ndo uone wanasiasa wanavyokosea timing za matukio. Nadhani itafikia wakati mtu akitaka kukutukana atakwambia "Mwanasiasa mkubwa weh"
   
 9. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ukimwaga mboga tunamwaga ugali, VITA NI VITA MURAA.

  Waangalie wasije wakafuta mpaka za maafande, hawachelewi kuwa majambazi wale.
   
 10. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mwandishi hana kumbukumbu Dr SLAA ndiyo alikuwa wa kwanza kupinga posho
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hiyo wanalipwa nini. Unategema tume ya nini hujui ilipwe nini?
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Aliziwacha? Tunajuwa Zitto ndio kagoma kuzichukuwa.
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Zitto Zuberi Kabwe ndiye amezipinga posho za vikao kwa vitendo baada ya kuacha kuzichukua; hakuna cha Dr. Slaa wala Mbowe, hao wamekuwa ni wa kutoa matamko tuu lakini anazila posho. Wabunge wengi wa CDM wanamchukia Zitto kwa sababu ya msimamo wake huo. Kama kweli posho zitafutwa basi Zitto ndio atakuwa ame play a big role.

  Ila sasa akumbuke kuwa kina vikao ambavyo lazima wajumbe walipwe posho, mfano vikao vya bodi. Na Zitto alikuwa makini kwa kusema kwamba huwezi kulipwa posho kwa kuwa kufanya kazi yako.
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Mwalimu anapata sitting allowance lini? Serikali inatakiwa iache wizi, ifute posho, iongeze mishahara na ipunguze kodi hiyo ndio njia pekee watu wanaweza ishi. Wengi hufurahia posho sababu hazikatwi kodi, wanaona hata mishahara isipoongezeka sawa tu kwani inakatwa kodi kubwa!
   
 15. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
  Heee wabunge kufutiwa posho wanataka na wafanyakazi wa serikali wafutiwe, hawajui wenyewe hupokea mishahara na marupurupu lukuki, na wengine hawastahili kwani HULALA BUNGENI, tungojee...
   
 16. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Heri posho zifutwe, foleni ya magari imezidi Dar kwa kuwa wengi wameyanunua kwa fedha za posho ambazo ni wizi mtupu, halafu wanayatia mafuta magari yao kwa hela hizo hizo za posho. Zikifutwa foleni itakuwepo wiki moja tu ya mwisho wa mwezi, siku ya kawaida watabanana kwenye daladala. Futa posho ndugai
   
 17. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  POSHO=WIZI WA "HALALI" dhidi ya wavuja jasho na walala hoi wa nchi hii!
  WIZI HUU LAZIMA UKOMESHWE MARA MOJA.WANANCHI WAMECHOKA.
  HUMO KWENYE POSHO UKIDADAVUA ZAIDI UTAKUTA MADUDU YA AJABU - hata kughushi kutabainika.
  Listi ya posho inaweka hata watu wasiohudhuria vikao na zinachukuliwa na wajanja.
   
 18. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  HAITAWEZEKANA KWA SERIKALI YA CCM. Wanatumia mamilioni kuupata ubunge, posho ni moja ya vyanzo vya kurudisha gharama za uchaguzi
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Masahihisho kidogo. Muasisi wa hii issue ya posho sio January Makamba wa la Zitto Kabwe. Dr Slaa kwa wale wenye kumbukumbu nzuri ndiye alianza kulia na malipo ya ajabu ajabu kwa wabunge. Ni zaidi ya miaka 5 tangu aanze kuongea hizi habari na hata kwenye kampeni za mwaka 2010 alikuwa analiongelea sana hili swala. Wakati huo nadhani elimu ya uraia haikuwa imesambaa kama sasa.

  Baada ya uchaguzi wa 2010 ndio jambo hili likapewa uzito wa juu likiongozwa na wabunge wa CHADEMA na baadae January akaliongelea kwa kutumia mpango wa maendeleo 2011-2016 ambamo swala ya posho limeotajwa. Kwa ufahamu wangu January, Zitto na hata Mnyika hawapokei posho. Inawezekana wako wabunge wengine.

  Shida hapa ni kwamba uongozi wa bunge umekataa kutenganisha daftari la mahudhurio na posho. Mbunge anatakiwa a-sign mahudhurio na bunge linatumia list hiyo hiyo kulipa posho. Wenje kaongea sana bungeni akitaka mahudhurio yatenganishwe na daftari la posho lakini uongozi wa bunge umekaa kimya. Kwa maana hiyo Tanzania inaweza kuwa nchi pekee duniani INAYOLAZIMISHA wabunge wake kupokea malipo.
   
 20. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  duh!! uzuri imewekwa wazi...... mishahara iangaliwe upya ili iwe yenye kutosha na sio kulundika maposho ambayo ndiyo kujenga ukuta kati ya wateule wa mifumo wanaohudhuria vikao na wanyonge wasiohudhuria vikao (Mbowe, 2010).
   
Loading...