KIAMA CUF: Baada ya kugalagazwa Uzini, Temeke yapasuka wanachama zaidi ya 1,400 WAJITOA

hasan124

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
716
128
Katika kile kinachoaminika Ni DHAMBI ya ChukiUbinafsi na Fitna (Kama initials za chama husika CUF), Leo tar.13-02-2012 viongozi na wanachama Kutoka wilaya ya Temeke zaidi ya 1420wamejitoa katika chama hicho katika muendelezo wa lile gogoro linalokitafuna chama hicho baada ya kuwavua uanachama MHE. Hamad Rashid Mohamed Mbunge wa WAWI, Doyo Hasan Doyo, MHE. Shoka pamoja na Sanane wote Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Taifa KIMIZENGWE.
Habari hii mbaya mno kwa chama hicho imekuja siku moja tu baada ya kugalagazwa vibaya mno na CCM na Chadema katika chaguzi ndogo ya Muwakilishi jimbo la Uzini Visiwani Zanzibar.
Katika sakata Hilo, wanachama waliojivua Leo hii wakiaminika kabisa kupinga maamuzi ya kibabe na kutozingatia Sheria, haki na demokrasia kutoka kwa viongozi wakuu wa chama husika, hivyo kwa kauli moja wameamua kuonyesha wazi msimamo wao wa kumuunga MKONO MHE. Hamad Rashid Ni pamoja na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Temeke wa4 wakiongozwa na Bi. Rehema Chamwenyewe na mama Zainab Momba, Mkurugenzi wa Haki zaBinadamu Wilaya Rajabu Sudi, ilevile wako viongozi na wanachama wa kata za Makangarawe, Mbagala, Kiburugwa, Tandika, Azimio, Toangoma na Mbagala Kuu.
 
Katika kile kinachoaminika Ni DHAMBI ya ChukiUbinafsi na Fitna (Kama initials za chama husika CUF), Leo tar.13-02-2012 viongozi na wanachama Kutoka wilaya ya Temeke zaidi ya 1420wamejitoa katika chama hicho katika muendelezo wa lile gogoro linalokitafuna chama hicho baada ya kuwavua uanachama MHE. Hamad Rashid Mohamed Mbunge wa WAWI, Doyo Hasan Doyo, MHE. Shoka pamoja na Sanane wote Wajumbe wa Baraza Kuu ya Chama Taifa "KIMIZENGWE".
Habari hii mbaya mno kwa chama hicho imekuja siku moja tu baada ya kugalagazwa vibaya mno na CCM na Chadema katika chaguzi ndogo ya Muwakilishi jimbo la Uzini Visiwani Zanzibar.
Katika mkutano na wandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Dar Live ulioko Mbagala,wanachama waliotangaza kujitoa Leo hii wakiaminika kabisa kupinga maamuzi ya kibabe na kutozingatia Sheria, haki na demokrasia kutoka kwa viongozi wakuu wa chama husika, hivyo kwa kauli moja wameamua kuonyesha wazi msimamo wao wa kumuunga MKONO MHE. Hamad Rashid Ni pamoja na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Temeke wa4 wakiongozwa na Bi. Rehema Chamwenyewe na mama Zainab Momba, Mkurugenzi wa Haki zaBinadamu Wilaya Rajabu Sudi, vilevile wako viongozi na wanachama wa kata za Makangarawe, Mbagala, Kiburugwa, Tandika, Azimio, Toangoma na Mbagala Kuu.
Dhambi hii ITAENDELEA kukitafuna chama hiki hadi lini? Hasa ukizingatia tetesi za chama kipya cha kisiasa kinachotarajiwa kuanzishwa na MHE. Hamad Rashid, Je, CUF itapona na gharika hili?
 
Chadema + CCM propaganda @work, nani asiyemfahamu mto mada..anavyolamba miguu ya HR na chadema..

wenye akili walishakupotezea..
 
huo ni uongo
CUF haina wanachama wafikao mia mmoja huko Temeke
wanachama wa CUF temeke ni kama 46 tu
 
Chadema + CCM propaganda @work, nani asiyemfahamu mto mada..anavyolamba miguu ya HR na chadema..

wenye akili walishakupotezea..

Utaisoma Wewe, vp naskia mmeshika namba tatu tena Ni kweli?! Someni alama za nyakati itawasaidia.
 
Siasa za bongo shida tupu, watu wanapenda chama kuliko hata nchi yao..bora nchi ifilisike lakini chama kiwe na nguvu. poor Tz yangu!!
 
CUF kama hawatakubali mabadiliko kwa sasa, wakiendelea kukumbatia vyeo basi wataishia kuwa kama TLP...
 
huo ni uongo
CUF haina wanachama wafikao mia mmoja huko Temeke
wanachama wa CUF temeke ni kama 46 tu

Mbona wilaya ya Temeke ndiyo base yao Marytina? Na njia yote ya Kilwa road hadi Mbagala ni CUF kwa sana... Inaendelea hivyo hadi,mikoa ya kusini mashariki(Lindi na Mtwara)
 
Utaisoma Wewe, vp naskia mmeshika namba tatu tena Ni kweli?! Someni alama za nyakati itawasaidia.

Nini cha ajabu kusika no.3? unajua chama chako chadema kimeshika namba hiyo miaka mingapi kabla ya kwenda no.2?
 
CUF kama hawatakubali mabadiliko kwa sasa, wakiendelea kukumbatia vyeo basi wataishia kuwa kama TLP...

Timua timuatimua hiyo, uanadhani Ccmfd wenu wale? Kuna mafisadi wangapi na still wanabebana? Kama Ishu Ni kutimuana basi Leo CCM kingebaki jina tu. haiwezekani mtimue mihimili ya chama halafu mkasalimika hata kidogo Hilo halipo.....sera za ******* zile ndio siasa japo wanatutia changa la macho but still inawakandamiza kusavaiv....Leo hii kwa Ubinafsi tu wa wachache wakaonabora waue chama Inasikitisha sana.
 
Mbona wilaya ya Temeke ndiyo base yao Marytina? Na njia yote ya Kilwa road hadi Mbagala ni CUF kwa sana... Inaendelea hivyo hadi,mikoa ya kusini mashariki(Lindi na Mtwara)
hamna kitu kama base ya CUF
naomba mungu HR aondolewe ufanyike uchaguzi pemba ujionee CUF asipokuwa third again
 
Mara wanachama 1000 wajitoa mara katika thread nyingine 1400 wajitoa, mbona huna Consistence katika kureport kwako?
 
Mara wanachama 1000 wajitoa mara katika thread nyingine 1400 wajitoa, mbona huna Consistence katika kureport kwako?

Nimepost then nikaedit kurekebisha kidogo then watu wakawa washakoment kwa ile ya kwanza within a minute ndio maana nikashindwa kutoa moja....but reality Ni watu 1420 wametangaza kujitoa plus unaweza kucheki ITV & Mlimani ndio walikuwepo pia magazeti kesho like Majira, Tanzania Daima etal.
 
Back
Top Bottom