Kiama chaja, vilio vitakuwa vingi sana

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,782
Mwenyekiti mpya wa ccm amepatikana na yule yule aliyetegemewa kutokana na mazoea na utamaduni uliozoeleka ndani ya chama
Wengi walishangilia kwa unafiki wengi wakiugulia ndani kwa ndani...heri ungekuwepo utaratibu wa kupiga kura na kushindanisha matokeo yangekuwa tofauti kabisa
Mikwara ya mwenyekiti mpya tayari umeshaanza na haya ndio maazimio yake
. Kupunguza wafanyakazi wasiopungua 1200 nchi nzima
. Kuhakiki upya mali za chama
. Kuhakiki upya uwekezaji wa chama
. Kuwakataa rasmi wale wanaoitwa wafadhili wa chama nk nk
Ukiachana na hawa wanachama wa kushangilia chochote kinachosemwa na viongozi ndani ya chama Kuna kundi ambalo ndio kama engine ya chama
Hili kundi ndio
Linalokusanya michango yote kwa niaba ya chama
Linaloratibu matumizi yote
Linaloratibu chochote ambacho kitakuwa na maslahi kwao kwa jina la chama
Linalosimamia miradi mali na uwekezaji wote wa chama
Hili kundi sio rasmi lipo hapo kwa maslahi binafsi lakini kupitia jina la chama
Kiama ndio kinakuja kwenye hili kundi, maisha yao yamekuwa super kutokana na chama wamejipatia mali nyingi kupitia chama , hawa ni ccm maslahi ambao hawakupenda kabisa uenyekiti uende kwa huyo aliyeteuliwa
Hayo maazimio yakisimamiwa bila kupindisha tutashuhudia ufisadi wa kutisha, ufisadi wa karne na mambo mengi mabaya yaliyofanyika chini ya kundi hilo lenye mizizi mrefu na ya muda mrefu ndani ya chama
Waathirika wakubwa watakuwa hawa
-viongozi mbalimbali serikalini
-viongozi mbalimbali ndani ya chama
-watu maarufu wakiwemo majaji na wanasheria
-viongozi wa kidini
-matajiri na wafanya biashara wakubwa
-wazee wa chama
-wanachama vigeugeu na wanachama mtu
Ule mtandao wa ulaji ule mtandao wa upigaji uliotikiswa kuanzia bandarini mamlaka ya mapato na kwingineko sasa unaenda kuzikwa rasmi
Tutarajie nini??? Yatajitokeza mengi..!ambayo kwasasa hayawezi kusemwa
 
Mpaka 2020 vitambi vingi vitapungua
Hili laweza kutokea tena japo kwa namna tofauti tena kimya kimya sana
1469854287212.jpg

Kwakweli makufuri yupo vizuri.....akaze kamba
 
Kweli soma Heading kisha soma kilichomo ndani yake. Nilishajenga wazo kwamba Unasemea mambo ya Kiama,siku ya kurudi kwake Mwokozi. Kwa hiyo nilitegemea mambo ya Kutisha na kufurahisha kwa wengine.

WanaCCM wengi wamejisomesha namba wenyewe.
 
Kweli soma Heading kisha soma kilichomo ndani yake. Nilishajenga wazo kwamba Unasemea mambo ya Kiama,siku ya kurudi kwake Mwokozi. Kwa hiyo nilitegemea mambo ya Kutisha na kufurahisha kwa wengine.

WanaCCM wengi wamejisomesha namba wenyewe.
 
hivi zile kura zote walizompa ni kwamba walianza kujishtukia.....ila kwa mwendo huu ni ngumu kukamilisha malengo binafsi maana ngoja kwanza tusubiri tarehe MOJA!
 
Back
Top Bottom