Kiafya, Kamasi zitoleweje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiafya, Kamasi zitoleweje?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mzizi wa Mbuyu, Mar 17, 2010.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Wengine wanabana pua upande mmoja kisha wanfyatua mnpyuu!! inadondoka chini, wengine wanatumia mashati waliyovaa, wengine wana penga kwenye kitambaa maalumu na kuzifadhi mfukoni kisha wanatemea nazo kutwa nzima n.k n.k
  Jamani naomba msaada ukibanwa na makamasi njia bora na inayofa kiafya kuyatoa ni ipi?
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Tissue is the best (coz hakuna haja ya kufua). Kuna aina za tissue ambazo zina vumbi kidogo sana (maana hata kitambaa kina vumbi to some extent). Kitambaa, licha ya kutembea na mafua yako kutwa nzima mfukoni, pia nadhani inasababisha multiple infections(lolz!). Ila kupenga/kufyatua waziwazi ni kusababisha maambukizi kwa wengine na ni uchafu uliokithiri. (Bora umeze hehehe!:rolleyes:)
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,720
  Likes Received: 8,274
  Trophy Points: 280
  Unayavutavuta kwa ndani then unayatelekeza kwenye aliemntary canal...!!!!
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Duh! Hii babu kubwa!
   
 5. S

  Silvershadow Member

  #5
  Apr 9, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani utotoni mama alikufundisha ufanyeje wajemeni?
   
 6. m

  mimi-soso Senior Member

  #6
  Apr 9, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tupenge, ndio maana ndugu kauliza njia ipi ni sahihi?

  Kama kuna doctor tunaomba msaada
   
 7. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Mie naona hili swali si la mzaha. Ni zito kweli kweli! Jibu la KingÂ’asti kwamba tumia tishu ni zuri, ila ukiwa barabarani hiyo tishu utaiflashi wapi? Nyumbani tunatumia tishu kisha tunaflashi msalani.

  Naona wengi tunatolea kwenye kitambaa na kuweka mfukoni. Sasa tufanyeje? Au sio lazima kutoa?
   
 8. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  tukiongelea mambo ya tissue kuna yule wa kijijini hata haifahamu, yeye nae ni wa kumuangalia pia na kushauriwa apengeje maana nako kule...mmmh!!
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  upengaji wa mafua kitaalamu unatakiwa upenge kwa kuziba tundu moja na usitumie nguvu kuyatoa.
  pili unatakiwa mafua ukiwa nayo uyatowe, kwa sababu usipoyatoa yaani yale ma germs yote unayarudisha ndani ya mwili wako

  suala gumu linaguja upengee wapi? wenzetu ulaya hutembea na paketi vya tissue, unapenga kama hakuna dust bin unatia katika mfuko wa plastik unaufunga unatia kweenye handbag yako unatembea nayo mpaka ufike nyumbani

  holla!
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  1. Kupenga kamasi kunahitaji umakini vinginevyo waweza kujiletea madhara kwenye mfumo wako wa pua, masikio na hata koo ( ENT).Kumbuka makamasi au Mucous iliyoko puani huchuja vijidudu vilivyomo hewani vyenye kuleta uambukizo. Wataalamu wa tiba wa ENT hushauri kuwa pressure inayotokea unapopenga huweza kuathiri mishipa damu na huathiri mfumo wako wa hewa, hivyo tunatakiwa kuwa makini tunapopenga.
  2. Ili kupunguza madhara, kama alivyosema Gaijin hapo juu, unatakiwa kupenga ukiwa umeziba pua moja ( one nose at a time)..ili kusiwe na pressure kubwa sana puani, maskioni na hata kichwani... nadhani mtakubaliana nami kuwa unapokuwa na mafua ukapenga wakati mwingine unajisikia kama ubongo nao unataka kutoka lol!.
  3. Penga kwa kutumia kitambaa safi ( epuka kurudiarudia kitambaa maana utajiletea uambukizo), au penga kwa kutumia tissue. Ukiwa unaoga au kunawa uso usiogope kupenga kwa mkono. Infact njia nzuri zaidi ya kupenga ni kwa kutumia maji ya uvuguvugu yenye chumvi ukavuta mvuke na kusaidia kutoa mafua. Hapo kwa vyovyote utatumia mikono yako na inabidi unawe vizuri baada ya hapo. Njia ya kupenga kwa mikono hata hivyo siyo sahihi uwapo nje ya nyumbani kwako au sehemu utakayopata maji na sabuni ya kunawa.
   
 11. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Kibongo bongo watakuambia kinyaa lakini ndio ukweli na utaratibu wa kupenga makamasi kiafya na kistaarabu ili husimwambukize mwingine. Mada nzuri sana hii
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Asante Mama WOS
  hapa umemaliza kila kitu. This is the value of Mama
   
 13. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Angalizo kwenye tissue. Sio tissue za aina zote zinafaa kutumika kupengea makamasi
   
 14. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  mwenzio nimeshanunua toilet paper....so now which is which?
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Apr 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  makamasi yanatolewa kwa kupenga; katika kufanya hivyo tumia njia ambayo haitasambaza vijidudu na kuosha mikono yako kwa sabuni au disinfectant (hasa kama uko mwenye nchi ambazo vitu hivyo ni rahisi kuvipata). Jambo la msingi ni kutojipangusia mwenyewe au kwenda kusalimiana na watu bila kusafisha mikono. Tunaweza kupunguza maambukizi mengi kwa kusafisha mikono yetu mara kwa mara.

  Watu wabaya ni wale wanaopenda kwenye hendikachifu halafu wanaitumia kutwa nzima huku wakiigeuza upande upande na jasho likiwatoka wanajipangusia usoni! halafu anakuja na kukusalimia!!!
   
 16. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Kamanda MM, hii si ndiyo yenyewe Kibongo bongo. Kwa mfano niko Kariakoo sokoni, kama vile nina mafua na kuna jua la kufa mtu na uchumi wenyewe ndio huo unagonga pande zote mfukoni nina Anjifu moja tu, nitafanyaje halafu katika zunguka zunguka nimekutana na Ngosha mwenzangu, kweli nisimpe mkono Mkuu. Je nikikutana na Mama Mkwe je, nimpotezee vilevile.
  Ni approach nzuri lakini utamaduni na hali halisi ya maisha ya kibongo ni ngumu. Wengine tissue tunakutana nazo hotelini tu kwa mbinde, huko home ni almasi bana
  Asante
   
 17. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hii ushauri imetulia sana, acha tuiweke kwenye makabrasha itusaidie msimu wa vumbi kali , senksi greti thinka.
   
 18. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135

  hawa labda watumie ugoro ( tumbaku la kuweka puani), hii inasaidia sana kuleta automatik nacharal chafya na inapatikana bure vijijini ! huna haja ya tishu wala kubana pua.(side efekti) rejea post ya WOS.
   
Loading...