Kheri upweke kuliko mpenzi asiyejua maana, mapenzi hajaribiwi

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,306
Mapenzi yana siri kubwa. Kila mmoja ana ugonjwa wake wa kupenda. Wengine wanawapenda wapenzi warefu, lakini kuna kundi ambalo huchanganyikiwa zaidi kwa wafupi.Pamoja na mchanganuo huo, kuachwa inauma hata kama anayekutosa hukuwa na mapenzi naye.

Ile dhana tu ya kuachwa ndiyo hutesa watu. Kuna dhana kwamba anayeacha mara nyingi hujiona mshindi dhidi ya aliyemuacha. Na hiyo ndiyo sababu ya wengi kuumiawanapofungiwa milango ya kukatisha.

Uhusiano ambao pengine hata hawakuwa na masilahi nao.Mathalani, mwanamke anaweza kuwa havutiwi na mtu aliyenaye kwa maana moja au nyingine. Ilitokea kuwa naye kama ajali tu!

Kutokana na kutokuwa na hisia naye, hakuona tatizo kumsaliti kwa mwanaume mwingine, lakini huwezi kuamini siku akiambiwa basi, atalia machozi na kuomba msamaha.

Si kwamba atalia kwasababu ya mapenzi ya dhati aliyonayo kwa mwenzi wake, kwamba inamuuma kuachana naye, ila kinachomtesa ni zile hisia za kuachwa. Na ingetokea kuwa yeye ndiye anayeamua kuacha, tafsiri ingekuwa kinyume chake.

Macho yangekuwa makavu na ikiwezekana angekwenda kusimulia kwa marafiki: “Aah, James nimempiga chini kanililia huyo!”Anafurahi dada yetu na wenzake watampongeza kwa kugongesheana viganja!

Tatizo kubwa ambalo linawagharimu wengi ni kuwa mapenzi yanabebwa kama aina ya mchezo wa kuigiza. Watu wanaingia kwenye uhusiano kwa kujaribu. Kuna waliofunga ndoa si kwa kuchaguana, isipokuwa walidanganyana kwa hisia za “mapozeo” mwisho wa siku wakazoeana, ikawa ngumu kuachana.

Wapo wanaoingia kwenye ndoa si kwa kuvutwa na nyoyo zao, ila wanakabiliwa nafikra za “waoaji wenyewe hawapo, acha nimkubali huyu huyu!” Mapenzi ni nguzo maalum mno kwa maisha ya binadamu, kwa hiyo ni vema yabebe heshima inayostahili.

Ogopa sana mtu anayekuwa na wewe kwa sababu haoni chaguo lake. Adhabu yako ni kubwa mbele ya safari ingawa unaweza kujiona upo kwenye bwawa la asali mwanzoni.Kiama chako ni pale atakapomuona anayedhani ndiye sahihi kwake. Utasilitiwa upende usipende.
 
Nakupa salute kwa heshima na taadhima,iwapo makala haya yametoka kwenye upeo wako wa kufikiri mpaka ukatuletea mchanganuo huu,basi sina shaka Mungu amekuzawadia akili pevu na kukufanya wewe GENIUS ,hakuna shaka kwa hilo wewe utakuwa GENIUS,umeongea kiuhalisia kabisa bila chembe ya shaka,.,.,.UBARIKIWE
 
Back
Top Bottom