Kheri Denice James; Tumaini Jipya Lililorejea UVCCM

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,905
2,000
*KHERI DENICE JAMES; TUMAINI LILILOREJEA UVCCM*

*Na; Peter Kasera*

Kheri James ana vita kubwa. Ni vita vya kulitoa Jumuiya (UVCCM) katika hali ya unyonge na kulitia katika hali ya nguvu. Vita vya kuwafanya wanachama wa UVCCM kurejesha matumaini ndani ya jumuiya yao yaliyotoweka kwa muda mrefu. Vita vya kupambana na wezi, ubadhirifu na mafisadi wa mali za Jumuiya.

Pamoja na vita hii, jambo la faraja ni kuona kwamba kundi kubwa la vijana/walio wengi kwa kauli moja wameamua kumuunga mkono Mwenyekiti Kheri James. Binafsi nimeshiriki kikamilifu katika harakati hizi zilizokamilika juzi Dodoma, niweke wazi tu kuwa nimetambua uwezo, umahiri, uhodari, umakini, uchapakazi na usikivu wa Ndugu Kheri James.

Kila jambo tulilomshauri, tulikaa kwa pamoja na kuwa na majadiliano mapana na kisha kufikia mwafaka na njia bora na sahihi. Hatua hii ilipelekea Rafiki yangu ambaye alikuwa kiungo muhimu katika harakati hizi Ndugu *Hassan Bomboko* kunibatiza jina la "Chief Strategist" yamkini sio kama David Axelrod (Obama, 2008), ama David Ndii (Raila, 2017).

Ndugu *Kheri James* naomba nikuondoe hofu, unapoanza na kuendelea na mapambano yako (ambayo kimsingi ni yetu wanyonge, na ambao tuliogopa hata kukanyaga pale UVCCM Lumumba kutokana na matabaka yaliojengwa na kuwekwa baina yetu, ni vyema ukatambua kwamba vijana tulio wengi tutasimama na wewe daima kwa maslahi ya vijana wote wapenda haki.

Wiki jana nilibahatika kupitia kitabu cha Prof. Shivji "Insha za Mapambano za Wanyonge" katika kitabu hicho Prof. Shivji alibashiri kuhusu kumea kwa dalili zilizoashiria kurejea kwa misingi mikuu ya Azimio la Arusha" ushuhuda wa maono haya na maandiko haya ni jinsi Rais Magufuli anavyozidi kufanya kazi kwa niaba ya wanyonge. Amekuwa mtetezi wa haki na kulinda usawa miongoni mwa~watanzania hasa masikini waliotupwa mbali na mifumo ya uchumi kwa miaka mingi.

Sasa ni dhahiri unaenda kumsaidia Rais Magufuli katika ngazi hiyo na katika mapambano mbalimbali. Unaenda kuwa mwakilishi wetu vijana. Unaenda kuwa sauti zetu vijana. Unaenda kuwa msemaji wetu katika vikao vya juu vya Chama. Sisi kama vijana tuko nyuma yako, na tutashiriki na wewe katika kuangalia ni njia zipi bora za kutatua changamoto zinazowakumba vijana kama uhaba wa ajira, matumizi ya dawa za kulevya, namna bora ya vijana kushiriki katika kilimo ili kuzalisha malighafi kwa ajili ya kulisha viwanda vinavyojengwa kwa kasi sana katika awamu hii ya tano.

Katika kampeni zako uliongelea na kusisitiza sana dhana ya Mageuzi. Rais Magufuli pia katika ufunguzi wake wa mkutano huo wa 9 wa vijana aliweka msisitizo zaidi katika suala la Mageuzi na kufanya Mabadiliko makubwa ndani ya Jumuiya. Kwa dhana hizo ni lazima vijana ama wananchi wote watambue kwamba vijana walio wanyonge, ama vijana walionyimwa fursa kwa miaka mingi hawawezi kutaka mambo yaendelee hivi hivi tena. Kamwe vijana hawawezi kukubali hali hiyo pasipo mabadiliko makubwa kufanyika. Vijana ndio kundi la kutoa dira dhidi ya mapambano ya unyonge, hivyo ni wito kwa vijana wote kwamba tushampata Mwenyekiti mpya hivyo, lazima tumuunge mkono kwa dhati kabisa.


Katika kuongoza mapambano hayo ni jambo la heri na neema kuwa sasa Jumuiya imepata kiongozi mpya. Ndugu Kheri James amekuwa kijana msikivu, kijana makini, kijana hodari, kijana mchapakazi, na mvumilivu. Naamini Jumuiya imepata mtu sahihi na kweli tumaini jipya limerejea ndani ya UVCCM...

*Peter Kasera*
Mchambuzi Huru!...
 

Lumwagoz

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
978
1,000
Umesema ataenda kupambana na wezi na mafisadi ndani ya jumuiya yenu..Hapo ccm ndo mnaniachaga hoi kabisa....maswal yangu kwako.1. Kabla ya james kuchaguliwa jumuhiya yenu ilikua inaongozwa na wanachama wa chama gani?, 2.Huo ufisadi na uwizi uliugundua ln? Na wapi ulitoa taarifa ya ufisadi huo. Au ulikua unasubir mpaka james achaguliwe ndo utoe taarifa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom