Khaliat nahal (honeycomb breads)

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,568
16,906
Mahitaji ya shira(syrup)

1)Sukari kikombe 1
2)maji kikombe kasoro
3)hiliki kiasi
4)zafarani (saffron) au arki ya rose...

Mahitaji ya mkate

1)Unga wa ngano vikombe 3.5
2)mayai 2
3)maziwa ya unga 2 tablespoon
4)sukari 3 tablespoon
5) hamira1 tablespoon
6)chumvi 1/2 teaspoon
7)siagi iliyoyayushwa 4 tablespoon...
8)mafuta ya kupikia 4 tablespoon.
9)maji 1/2 kikombe...
10)maziwa kikombe 1
11)jibini (cheese) portion 6-8
12)baking powder 1 teaspoon..

Namna ya kutaarisha

1)Chemsha,maji,sukari,hiliki,suffron kwa dakika chache hadi iwe nzito nzito...weka pembeni ipoe..

2)weka kwenye bakuli unga,hamira,sukari,chumvi,maziwa ya unga...
2)weka mafuta,siagi uliyoyayusha na yai moja..changanya vizuri...
3)changanya maziwa na uchanganye unga wako...huku ukiengezea maji kidogo kidogo hadi uwe umekandika vizuri na laini...
4)wacha kwa dakika 10-15...
5)tengeneza viduara vidogo vidogo...ndani ya kila kiduara weka cheese kiasi...alafu weka kwenye trey...
6)ukimaliza pakaa yai juu yake..
7)weka kwenye oven 300°-350°....hadi ziwe brown


8)zikishapoa mwagia shira(syrup juu yake)....

Khaliat nahal (honeycomb bread) tayari kwa kuliwa...
 

Attachments

  • 1386337937249.jpg
    1386337937249.jpg
    62.6 KB · Views: 292
  • 1386337948518.jpg
    1386337948518.jpg
    71.1 KB · Views: 288
Last edited by a moderator:
Hhahahahhhh kesho itabidi upike...:):):):):)
Alafu chai yenyewe ile yetu ileee mdalasini,hiliki,zatar,mchaichai weee...
Kabisa naona ningesinzilia kwenye sofa!!!shogaangu anavipika hivo na ana nyunyuizia kama spice fulani hivi inafanana na seasam lkn nyeusi yaani nikianzaga kuvila mhhh shida kustop vitamujee!!
 
Kabisa naona ningesinzilia kwenye sofa!!!shogaangu anavipika hivo na ana nyunyuizia kama spice fulani hivi inafanana na seasam lkn nyeusi yaani nikianzaga kuvila mhhh shida kustop vitamujee!!

Hizi waweza weka sesame pia.....
 
Faffy..Mmh safri hii umenisahau Khaliat nahal (Bee queenhouse) si ungewekezea Black seeds"habaa souda"kwa juu..... MashaAllah Mkono wako mwema. ubarikiwe dadaytu

Amina.....next time nkikualika ntaweka na haba souda uje ujirambe:p:p:p:p:p
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom