Khadija Kopa afunguka asema hajawahi kuchepuka tangu mume wake afariki

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
811bdd7d737f03a378bd4200d61a0192.jpg
0c861be3b38cdd61d39001d4aafec559.jpg
[https://1]

MALKIA wa Mipasho Tanzania, Khadija Kopa amefunguka kuwa hajawahi kuchepuka tangu mumewe afariki dunia, kwa sababu anaogopa kuchuja, kuchoka na kuzeeka mapema.

Global TV Online ilifanikiwa kuzungumza na Kopa aliyefunguka mambo mengi kuhusu muziki, maisha ya uhusiano, mafao na maisha yake ya kawaida:

Nini chanzo cha Taarab kuchuja?

“Ujue kuna watu wanaanzisha vikundi vya Muziki wa Taarab ambavyo vimekuwa vikipiga kwenye mabaa bure au kwa kiingilio cha bia.

“Sasa ikitokea tunafanya shoo, watu hawaji wa kutosha kwa sababu wanajua wataenda baa fulani wataingia kwa bia moja na kuimbiwa nyimbo zetu zote. Ni kweli Taarab imeanza kuchuja?

“Ni kweli kabisa, nashangaa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) hawaangalii jambo hilo wakati wao ndiyo wenye mamlaka ya kuzuia na kufuatilia kazi za wasanii nchini. Nini ushauri wako kwa Basata?

“Wizara itusaidie, watusimamie kwa sababu naona kama Basata hawawezi, tunawalipa kodi ya bure na wako serikalini bure tu hawashughuliki. Ni kweli hujawahi kuchepuka tangu mumeo afariki dunia?

“Katika maisha unaweza kumpata mtu kumbe hana mapenzi ya dhati kwako, anakuhitaji kwa sababu wewe ni maarufu, anahisi na yeye atakuwa maarufu au anahisi una pesa kumbe hauna kitu.

“Sijawahi kuchepuka, mchepuko mimi wa nini na umri huu, nina watoto na familia yangu. Ni kweli mwanamke au mwanaume kuishi pekee yake kwa muda mrefu si sawa, ila huwezi kuchukua mwanaume wa hovyo, kwanza wala sijakulia mazingira hayo, naogopa kuzeeka, kuchoka na kuchuja mapema. Umeshapenda mara ngapi tangu mumeo afariki dunia?

[https://3]

Khadija Kopa

“Unajua ukifiwa au ukiachana na mtu uliyekuwa unampenda inakuchukua muda mrefu sana kumuamini mtu mwin-gine, kwa sababu unakuwa unahisi inawezakana si mtu sahihi au hawezi kufikia vigezo. Wanao wanajifunza nini kwako?

“Naamini kwa tabia na mwenendo wangu wanajifunza vingi, kwa sababu wanaume wana matatizo sana, hawanioni nikibadilisha wanaume mara huyu mara yule! Ikitokea mwanaume akakupenda, uko tayari?

“Akija kama mume ambaye Mungu kamleta kwangu, nitashukuru kwa sababu bado niko vizuri, nina afya njema, lakini ni lazima awe mchapakazi, mwenye upendo wa kweli, siyo wa kufuata umaarufu wangu. Ukipata nafasi ya kuzungumza na Rais Magufuli utamwambia nini?

“Kwanza naamini kupitia Global TV Online ataniona, Mhe. Rais Dk Dk. John Pombe Magufuli tunaomba utuangalie na sisi tuliokitumikia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Bendi ya Tanzania One Theatre (T.O.T), muda wetu wa kustaafu umeishafika hivyo tunaomba tupewe mafao yetu ili tuanze maisha mengine.”
 
“Kwanza naamini kupitia Global TV Online ataniona, Mhe. Rais Dk Dk. John Pombe Magufuli tunaomba utuangalie na sisi tuliokitumikia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Bendi ya Tanzania One Theatre (T.O.T), muda wetu wa kustaafu umeishafika hivyo tunaomba tupewe mafao yetu ili tuanze maisha mengine.”


Haka kasehemu kamenihuzunisha sana, mnatumika halafu mnatupwa kama haja. Pole sana Kopa na T.O.T wenzako.
 
Back
Top Bottom