Khaaa! wauzza madawa waanikwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Khaaa! wauzza madawa waanikwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LOOOK, Jun 21, 2011.

 1. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,378
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikilla ‘ameifungukia’ kauli ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa, baadhi ya viongozi wa dini nchini wanajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, Ijumaa Wikienda linashuka naye.

  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Ijumaa iliyopita, Mtikilla alisema tamko la JK ni la kweli kwa vile wapo baadhi ya viongozi wa dini wasiofuata maadili ya kazi yao na kufanya biashara hiyo. Akaongeza kuwa, yeye anamjua mmoja (jina tunalo)
  MamaLwacrop.jpg
  “Rais alisema kweli, wala wasipinge. Kama kuna kiongozi yeye hafanyi biashara hii, ajue kuna wenzake wanafanya,” alisema kwa kujiamini Mtikilla.

  Aidha, Mtikilla ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha DP, alimtaja mchungaji mmoja wa kanisa la kiroho la jijini Dar es Salaam ambaye ana waumini wengi kuwa, na yeye anafanya biashara hiyo na watu wengi wanajua.

  “Mfano…(akamtaja jina) yule ni mfanyabiashara wa haya madawa, nani asiyejua bwana. Huyu na wenzake wengi ndiyo siri nzito ya kuwa matajiri wakubwa kwa sababu ya fedha haramu
  . imgres.jpg
  Pia, alisema kuwa, mchungaji huyo alidakwa na madawa miaka ya karibuni, baadhi ya viongozi hao wa dini walisikia, lakini akahoji, “ni kwa nini hawakutoa tamko?”
  Mchungaji Mtikilla aliongeza kuwa, haoni sababu ya viongozi wa Baraza la Maaskofu Tanzania kumkomalia JK kuweka hadharani majina ya viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

  Akahoji: “Mbona kuna maovu mengi yanayofanywa na viongozi wa dini ikiwemo ubakaji, ulawiti, utapeli na ushirikina lakini baraza halitoi tamko lolote?

  “Kila mmoja ana mapungufu yake, serikali kuna mahali inakosea kwa sababu suala hili siyo la kulizungumzia kwenye majukwaa bali kama wapo wanaotuhumiwa, wakamatwe na uchunguzi wa kina ufanyike ili sheria ichukue mkondo wake
  Archbishop-Dr-Valentino-Mokiwa.jpg
  “Pia viongozi wa dini wanakosea sana kutoa tamko dhidi ya rais. Hakuna sehemu ambapo maandiko matakatifu yanawataka kutumia jazba kukabili changamoto wanazokutana nazo.
  “Kama kiongozi hafanyi haya, ajue kuna wenzake wanajihusisha na michezo isiyofaa, ikiwemo hili la biashara ya madawa ya kulevya. Tuache kuteteana na kujificha nyuma ya mwavuli wa dini. Siku hizi wengi hawaaminiki, wanajali fedha kuliko huduma ya kuchunga kondoo wa Bwana,” alisema Mtikila.

  Wiki mbili zilizopita, katika hafla ya kumsimika Askofu John Ndimbo wa Kanisa Katoliki, Mbinga, Ruvuma, Rais Jakaya Kikwete alisema kuna baadhi ya wachungaji wanaojishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya.
  Alisema watumishi hao wa Mungu wamekuwa wakitumia nafasi zao kwenye paspoti kuingiza au kutoa madawa ya kulevya.

  Ndipo maaskofu wanaounda Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) walipokutana Juni Mosi, mwaka huu mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti, Mchungaji Peter Kitula na kumpa saa 48 Rais Jakaya Kikwete kuwataja kwa majina viongozi aliodai wanafanya biashara hiyo haramu.

  Viongozi wengine wa dini wanaounda jumuiya hiyo ni Askofu Valentino Mokiwa (Anglikana, pia ni Kaimu Mwenyekiti), Alex Malasusa (KKKT) na Moses Kulola (EAGT).
  Wengine ni maaskofu kutoka makanisa ya Moravian, African Inland, Baptist Tanzania, African Brotherhood, Church of God na Kanisa la BibliaMakanisa mengine yaliyopo kwenye Jumuiya hiyo ni Mbalizi Evangelist, Mennonite, Presbyterian, Salvation Army na Tanzania Yearly Meeting.
  Miaka ya karibuni, kumekuwa na baadhi ya wachungaji wa kiroho wanaolalamikiwa na baadhi ya waumini wao kwa kuwa na utajiri mkubwa.

  Waumini hao wamekuwa wakiwatuhumu wachunga kondoo wao kuwa, wanamiliki mamilioni ya fedha, magari ya kifahari, nyumba za kisasa huku wao, wakiwa kama kondoo, wanaishi maisha ya ufukara wa kutupwa.

  Hata hivyo, uchunguzi wa kina wa gazeti hili umebaini kuwa, baadhi ya wachungaji nchini, wanashindana kumiliki magari ya bei mbaya huku baadhi ya kondoo wao wakishindwa kulipia kodi ya chumba cha shilingi elfu thelathini (30,000/=) kwa mwezi

  H A HA HA ETI JINA TUNALO ALAFU PCHA CHINI HUYOMWANDISHI BONGE LA MJANJA HAWEKI JINA HALAFU ANAWEKA PICHA DUUU!! HATA MIE NAWASIWASI BORA NIHAMIE DINI YA WAPAGAN.
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,517
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unamaanisha nini kutoa picha hizo.
  Look angalia! unaushaidi?
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,236
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe unafata maandiko au unafata viongozi wa dini...
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 7,580
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  Mkuu imani haiendi bila matendo,
  Yesu alisimama na kuwaambia kwa mtu yoyote amshuhudie kuwa ana dhambi na kulikuwa hakuna mtu wa kushuhudia hilo, alikuwa anafundisha imani na anaonyesha matendo,

  Kama hao wachungaji wapo basi wanafundisha injili mfu, injili ambayo haipo, Pepo hawezi kumfitini pepo mwenzie, Kama Askofu anauza madawa ya kulevya kamwe hawezi kukemea ulevi, uzinzi, na vitu kama hivyo kwa sababu atakuwa anawakana pepo wenzie (mwenye masikio na asikie, naongea kwenye hali ya juu kabisa ya kiroho)
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 7,580
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  "Pia viongozi wa dini wanakosea sana kutoa tamko dhidi ya rais. Hakuna sehemu ambapo maandiko matakatifu yanawataka kutumia jazba kukabili changamoto wanazokutana nazo"

  siamini kuwa kauli hii imetoka kwa Mtikila, kweli kuna mageuko
   
 6. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,664
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  kazi kweli kweli....
   
 7. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 80
  Wakuu huko simo kabisa.... kama president mwenyewe kaishia kumumunya maneno kwa kushindwa kuwataja wahusika, mimi nitatoa wapi jeuri ya kuchangia hapa?
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 4,746
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  .Luke:13:32 'Akawaambia, nendeni mkwamwambie yule MBWEHA, nipo leo na kesho nikitoa pepo na kuwaponya wagonjwa, na siku ya tatu, nitakamilishwa'.
   
 9. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,099
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hatari sana!
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  (jina tunalo)......tupen basi?????au ndio picha hiyoooooo
   
 11. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 2,629
  Likes Received: 1,747
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi huyu Mtikila anatumika kama microphone ya watu. Ni mvurugaji mzuri wa hoja. Hata hivyo nitamkumbuka kwa suala la mgombea binafsi.
   
 12. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,634
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Mtikila anatumika kama buffering agent, anajua kudance na beat vizuri.
   
 13. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 9,305
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  mimi nitamkumbuka kwa kumwita rostam fisadi mchana halafu usiku anaenda kumwomba hela,..that's all
   
 14. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Mkuu
  Ipo tofauti kati ya PCT na CCT, Askofu Moses Kulola na EAGT hawako CCT nachofahamu askofu Kulola na EAGT wako PCT ambayo ni Pentecostal Council of Tanzania na CCT ni Christian Council of Tanzania. Kwa hiyo inawezekana kuna maelezo mengi tu ambayo unaweza kuwa umeyapotosha.
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 32,124
  Likes Received: 7,086
  Trophy Points: 280
  source: gazeti la ijumaa weekenda! mods thread kama hizi naomba mzitrash, JF hatuwezi kuaccept source of information kutoka kwenye magazeti ya Shigongo huku ni kuivunjia heshima forum hii. au napendekeza thread hii hiamishiwe kwenye jukwaa la udaku.
   
 16. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Na mimi nitamkumbuka kwa hoja ya kudai Tanganyika.
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,748
  Likes Received: 1,516
  Trophy Points: 280
  Mkuu hizo picha ndio zinatupa clue au?
   
Loading...