khaa!hata mbele za watoto natetemeka!!

Katika maisha yako ya kawaida inakupasa uwe ni mtu wa kujiamini, jitahidi sana kuelewa mambo na wala si kukariri.
Pia jaribu kukaa na watu werevu au kutafuta marafiki ambao ni msaada na wala sio mzigo kwa mantiki ya mawazo kichwani.
 
unapokuwa wewe ndiye muongeaji ni suala dogo sana la kujiambia kwamba kila mtu anakusikiliza wewe kwa kuwa wewe ndiye unayejua zaidi ya wote walio mbele yako. Hili litakujenga ni la kisaikolojia zaidi. Pili wakati uantaka kuongea jenga tabia ya kuwatazama wanaokusikiliza kila mmoja machoni na wawe wamekaa na wewe umesimama......

Hili la kwamba wewe unajua zaidi ya hao wanaokusikiliza (ni immagination tu usiibebe kuwa ni fact otherwise utachemka pale ukiulizwa swali linaloelekea kukukosoa). Unaweza husikubali kukosolewa na hiyo itakuwa mbaya kuliko. JIAMINI, unaweza........ Sote tulikuwa hivyo hivyo na leo tunaweza kusimama kuwafundisha hata maprofesa......
 
Onana na watu wa saikolojia watakusaidia kutatua tatizo ulilonalo.
 
Sio tatizo kubwa...ni watu wengi wana tatizo la kushindwa kuongea mbele za watu. Ushauri wa haraka zaidi ni kuanza kuongea unachotaka mbele ya watu unaowapenda na wanaokupenda; mfano mke, mume, watoto wako...ambao hata ukipata kigugumizi hautajisikia vibaya sana. Baada ya hapo unajifunza taaratibu...kuongea na watu wa aina tofauti.

Pia wahitaji kuhudhuria mafunzo maalum ya presentation...ama public speaking. kwenye mafunzo hayo wanafundisha jinsi unavyoweza ku engage na hadhira na wao wakawa wasikivu na kile unachowaambia. Na pia kuacha impact kwao.

Zaidi ya hapo..unapaswa kujiamini...na kuona kuwa unaweza!! Waongeaji wazuri wote unaowajua..walijifunza!!!

Nadhani hiyo itasaidia kidogo...wengine watajazia.
 
Katika maisha yako ya kawaida
inakupasa uwe ni mtu wa kujiamini, jitahidi sana kuelewa mambo na wala
si kukariri.
Pia jaribu kukaa na watu werevu au kutafuta marafiki ambao ni msaada na
wala sio mzigo kwa mantiki ya mawazo kichwani.

asante mkuu.
 
unapokuwa wewe ndiye
muongeaji ni suala dogo sana la kujiambia kwamba kila mtu anakusikiliza
wewe kwa kuwa wewe ndiye unayejua zaidi ya wote walio mbele yako. Hili
litakujenga ni la kisaikolojia zaidi. Pili wakati uantaka kuongea jenga
tabia ya kuwatazama wanaokusikiliza kila mmoja machoni na wawe wamekaa
na wewe umesimama......

Hili la kwamba wewe unajua zaidi ya hao wanaokusikiliza (ni immagination
tu usiibebe kuwa ni fact otherwise utachemka pale ukiulizwa swali
linaloelekea kukukosoa). Unaweza husikubali kukosolewa na hiyo itakuwa
mbaya kuliko. JIAMINI, unaweza........ Sote tulikuwa hivyo hivyo na leo
tunaweza kusimama kuwafundisha hata maprofesa......

nashukuru kwa ushauri wako.
 
Sasa wewe kama unatetemeka mpaka mbele ya watoto hiyo kazi uliyonayo uliipata bila ya kufanya interview km ni hivo kwenye interview si ulivaa sasa pampaz
 
Sasa wewe kama
unatetemeka mpaka mbele ya watoto hiyo kazi uliyonayo uliipata bila ya
kufanya interview km ni hivo kwenye interview si ulivaa sasa
pampaz

ha ha ha! kwa bahati kazi yangu sikufanyiwa interview .
 
shule yako kiwango gani? huja wahi kuwa monita, au kilanja, au kufanya morning talk shuleni? vipi hujafanya hata ngojera, maigizo primary hadi secondari? au "John Kisomo"?
Wewe hata ukienda TSJ au British Council kwa sasa hautaweza sababu unaumwa unaitaji tiba.
Dawa ya muda mfupi..
1.soma kichekesho nenda kawaambie watu wako wa karibu, wakicheka, una andika point fanya hivyo anagalu mara 10, kwa watu tofauti vichekesho tofauti.!!
2. Tunga story (ukweli/uongo/matukio ya zamani ya shule) kisha simulia, wape mda watu wakuulize, waelewe, wacheke, kama ni kuchekesha au wasikitike kama ni ya kusikitisha. Unaweza zigawa katika makundi, za kufurahisha, na za kusitikitisha (usizitoe siku moja kwa kundi moja).
3. kama ni mwanaume ukiwa njiani kwenda au kurudi kazini, daladala au chombo chochote cha usafiri, hata kwa mguu msemeshe mwanamke (kama mwanamke msemeshe mwanaume) mfanye aongee nawewe, ( she has to pay attention on YOU) kwa sababu ndo unaanza unaweza ukaanza na maswali madogo madogo kama 5, kisha ukafikisha 50 kwa watu tofauti, ambao hujakutana nao kabla.
Tiba ya muda wa kati
1 .Soma hadithi kisha isimulie kwa kifupi bila kupoteza maana, fanya kila mtu avutiwe aweza kutaka kusikiliza!
2. Ongea peke yako ndani na kujirekodi video/audio kisha baada ya muda sikiliza je unaeleweka unavutia mtu kusikiliza? 3. Angalia filamu, chagua "role model" actor jinsi anavyo ongea kisha na wewe jaribu kumugiza....... ( ila za kibongo sikushauri, kidogo za kinegeria na za kimarekani ( hasa kama ofisi yako inatumia ng'eri)
Jaribu hizo kwanza kisha utaniambia.
wakatabahu!!
 
Mimi nina mawazo tofauti;

Huyu jamaa sio kwamba ana kigugumizi??? Wakati wa utoto wangu nilikuwa na kigugumizi na hivyo nilikuwa na wakati mgumu nikisimamishwa darasani labda nielezee jambo fulani.

Sijui kiliponaje; nilishtukia nilipopewa uongozi na kuwa naongea mara kwa mara na wanafunzi niliokuwa nikiwasimamia hali hiyo ilipotea na mpaka sasa naongea bila wasiwasi wowote!
 
Back
Top Bottom