Kesi za wanasiasa (Wa upinzani) huwa zinaishia wapi?: Miaka nenda rudi wanadunda mitaani

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,491
2,355
Nalikuwa mtoto na sasa ni mtu mzima sijawahi kuona hata kusikia tetesi kuna mwanasiasa amefungwa kwa kutoa kauli za uchochezi kama tunavyotangaziwa kila kukicha na jeshi la polisi.

Nadhani ni muda muafaka wa waziri husika kutueleza watanzania tatizo ni nini, NI KUKOSEKANA KWA USHAHIDI? NI KUKURUPUKA KWA JESHI LA POLISI? NI RUSHWA MAHAKAMANI AU NI KITU GANI?. Ni vyema tukapata maelezo maana rasilimali na nguvu zinazotumika ni mali ya watanzania.
 
Back
Top Bottom