Kesi za Uhujumu Uchumi zilikimbiza wafanyabiashara, Kesi za Ugaidi matokeo yake kwenye Utalii mtayaona hivi karibuni

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,958
28,437
Taifa lolote likishaanza kua na kesi za namna hiyo ni mbaya sana kwa uchumi wa nchi.

Kama mtakumbuka vizuri kesi za uhujumu uchumi zilikimbiza wafanyabiashara wengi wakiogopa kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi.

Uzoefu unaonesha kua kesi za ugaidi popote duniani huua utalii kwa kiasi kikubwa yaani ni kama mchezo wa kuigiza lakini unaposhtaki watu kwa ugaidi unakuwa umeitangazia dunia kuwa kwako kuna ugaidi hivyo unahitaji kazi ya ziada kuutangazia ulimwengu kuwa wewe hauna ugaidi waelewe kuwa kwako kuna amani ya kutosha waje kutalii kwa amani.

Mkumbuke kila kitu unachofanya kwa nia mbaya au nzuri kina matokeo ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja.

RAFIKI YANGU WA MAREKANI KAAHIRISHA KUJA KUFANYA UTALII BONGO SABABU KASEMA AMEFUATILIA KUNA UGAIDI HIVO ATAENDA KENYA.
 
Back
Top Bottom