Kesi za serikali: Mpaka Sasa Ni Kesi 4,380 Tangu Mwaka 2000

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,245
Serikali imehusika katika kesi 4,380, tafadhali soma zaidi hapa chini:
Serikali imehusika katika jumla ya kesi 4,381

2007-11-08 16:17:30
Serikali imehusika katika jumla ya kesi 4,381 kati ya mwaka 2000 hadi 2007 zikiwa ni mashauri ya madai ya kawaida na maombi ya kupinga maamuzi ya mamlaka mbalimbali za serikali.

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Mathias Chikawe ameliambia bunge kuwa katika kesi 54 kati ya hizo, serikali ilikuwa mdai na kesi 4,227 ilikuwa mdaiwa.

Akijibu swali la Mbunge wa Wawi Mhe. Hamad Rashid Mohamed, Naibu waziri, amesema serikali ilishinda kesi 1,922 kati ya kesi 2, 327 zilizotolewa maamuzi na kushindwa katika kesi 400.

Kuhusu kiasi cha fedha kilichotumika kugharimia kesi hizo, Mhe. Chikawe amesema kwa kesi za kawaida na kesi za maombi ya kupinga maamuzi ya mamlaka mbalimbali, serikali huwatumia mawakili wake ambao ni waajiriwa kwa ajili ya kuendesha kesi hizo.

Amesema katika baadhi ya kesi, hasa za upatanishi, serikali hutumia mawakili binafsi kwa kuzingatia mkataba.

Ametaja sababu ya kutumia mawakili binafsi katika mashauri ya upatanishi kuwa ni pamoja na uhaba wa watalaam hao wenye cheti cha Kimataifa cha Upatanishi.

Source: IppMedia.

-- Kwenye kipengele cha mwisho hapo juu, je huu ni uhalalisho wa malipo ya kiajabu kwa Wakili Nimrod Mkono kwa niaba ya BoT?!

-- Ule utata alio uzua Waziri Magufuli nao malipo yake kwa wahusika wadai ya billion 15 (kama sijakosea) yakiidhinishwa nayo yatatoka kwenye hazina kuu?!

Naomba maelekezo wana JF tafadhali. Lakini muhimu hapa mimi naona ni wahusika wadaiwa kufungwa kama si kuachishwa kazi mara moja.

SteveD.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom