Kesi za kusingiziwa uhujumu uchumi na uchochezi sasa zimefika mwisho, Marekani mkombozi amefika Tanzania

Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
921
1,658
Habari wakuu,

Awamu hii ya tano inayoongozwa na Magufuli imekuwa ikiwakamata raia wanaopinga maovu yanayofanywa na utawala huu wa kidikteta na kuwaweka ndani kisha kufunguliwa kesi za uchochozi na uhujumu uchumi

Kwa sasa watanzania wanyonge waliobambikiwa kesi hizo za uhaini baada ya kupigania demokrasia hapa nchini kwa sasa mkombozi wao amefika

Matukio ya utekaji, kesi za uhujumu uchumi, kupotezwa kimyakimya, na kuuliwa kwa wapinzani wa nchi hii sasa yanaenda kuwa historia, baba wa dunia anayejua kunyoosha nchi na serikali kandamizi kwa wananci wake amesikia kilio chetu watanzania na anakuja...karibu marekani, karibu Trump Tanzania.

Erick kabendela, Tito magoti na wengine wengi kwa sasa tujiandae kurudi uraiani jiwe hana option zaidi ya kuwafutia kesi ili kuinusuru nchi

Karibu sana Marekani, njoo uninyosheeee Jiwe
 
Sidhani kama unaelewa kinachoendelea kwenye ulimwengu wa siasa za kiulimwengu! Na kukumbusha tu Tanzania tunafuata Katiba yetu ya nchi kama Taifa, sheria tulizojiwekea kanuni na Tamaduni zetu.
 
Najaribu kutafakari kama vikwazo inavyotishia US kwa Tanzania vinaweza kuwanusuru ao watu wako unawapigia upatu! Au unafikiri Waziri wa mambo ya nje anaweza kunyimwa visa yakuingia USA?
 
Kwanini ishindikane?

Mbona majuzi waziri wa mambo ya nje wa Iran amenyimwa visa kuingia USA?
Najaribu kutafakari kama vikwazo inavyotishia US kwa Tanzania vinaweza kuwanusuru ao watu wako unawapigia upatu! Au unafikiri Waziri wa mambo ya nje anaweza kunyimwa visa yakuingia USA?

dodge
 
Sidhani kama unaelewa kinachoendelea kwenye ulimwengu wa siasa za kiulimwengu! Na kukumbusha tu Tanzania tunafuata Katiba yetu ya nchi kama Taifa, sheria tulizojiwekea kanuni na Tamaduni zetu.

Hakuna sheria za kiongozi wa nchi kuonea wanaomkosoa, na kunajisi chaguzi za nchi kwa manufaa ya chama na genge lake.
 
Najaribu kutafakari kama vikwazo inavyotishia US kwa Tanzania vinaweza kuwanusuru ao watu wako unawapigia upatu! Au unafikiri Waziri wa mambo ya nje anaweza kunyimwa visa yakuingia USA?

..na UNYAMA unaofanywa na serikali ya CCM haiwezi kuisha bila key ppl in the govt kuguswa na vikwazo vya MABEBERU.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom