Kesi za kupinga matokeo baada uchaguzi zimeenda wapi?

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
244
Kwa wafuatiliaji wa chaguzi za kisiasa mtakumbuka kuwa pamoja na mambo mengine chaguzi nyingi hivi sasa zinagubikwa na udanganyifu, uonevu na utesaji unaofanywa na tume ya uchaguzi ikishilikiana na vyombo vya usalama na serikali.
Pamoja na kuwa na ushahidi wa uovu huo ( mfano Buyungu) wapinzani hawaitumii mahakama kutafuta haki.
Nini kimetokea?
Ombi langu wapinzani wafungue kesi za kupinga matokeo mahakamani ili pia kuweka kumbukumbu sawa.
 
Ombi langu wapinzani wafungue kesi za kupinga matokeo mahakamani ili pia kuweka kumbukumbu sawa.
hawawezi kufungua kesi kwa sababu hawana ushahidi
Upinzani unalia pale tu wanaposhindwa wao
kwenye uchaguzi wa 2015 buyungu,ccm tulishindwa kwa tofauti ya kura 156 tu,kwa nini iwe ajabu leo kwa mgombea yule yule akishinda,ukizingatia pia hakuna ukawa wala mafurikoz
 
Ni kupoteza muda tu. Danadana za mahakamani kesi inachukua miaka 2. Umewahi kujiuliza ni kwa nini kesi za CUF haziishi? Yaani kuchukua katiba ya CUF na kuisoma na kisha kutoa haki kwa Lipumba au Seif imekuwa mtihani. Katiba yenye kurasa chini ya 100 eti haisomeki.
 
Mahakama nyingi zimekuwa "Kangaroo Courts", nafikiri ndio maana wanaona hamna haja ya kwendapo.

Hata hakimu akiambiwa watuhumiwa wahana imani naye hivyo aachie ngazi kusikiliza kesi hakubali, kisa, shinikizo toka juu...!!! Sasa kwenda kwenye mahakama kama hizo ni kupoteza tu muda.
 
je hizi mahakama zipo huru,jiulize nani anateuwa majaji?nani analipa majaji?nani anawalinda? elewa kwa nchi zinazojielewa (hapa hapa Afrika) watarajiwa wa ujaji wanaomba na kuhojiwa kama mimi na wewe tunavyoomba kazi,na wanawajibika kwa BUNGE yaani kulinda katiba ya nchi na viapo vyao wanavifanya kwa jaji mkuu;na elewa kuwa wakuu wa tume zao za uchaguzi hazisimamiwi na majaji?maana kutakuwa na conflicts of interest katika utendaji wao,kwetu bado sana.
 
Kwa wafuatiliaji wa chaguzi za kisiasa mtakumbuka kuwa pamoja na mambo mengine chaguzi nyingi hivi sasa zinagubikwa na udanganyifu, uonevu na utesaji unaofanywa na tume ya uchaguzi ikishilikiana na vyombo vya usalama na serikali.
Pamoja na kuwa na ushahidi wa uovu huo ( mfano Buyungu) wapinzani hawaitumii mahakama kutafuta haki.
Nini kimetokea?
Ombi langu wapinzani wafungue kesi za kupinga matokeo mahakamani ili pia kuweka kumbukumbu sawa.
Muda wa kuendesha kesi,gharama za kesi na mnayeshindana nane yuko vipi ni mambo ambayo yanafanya wasifungue kesi.Chama cha upinzani hakiwezi (even behind the scene)kuharakisha kesi lakini Chama dola kinaweza.
Jambo jingine ni kuwaachia wananchi waupate uchungu wa kudhulimiwa.
Siha na Kinondoni ilikuwa wazi kabisa lakini waliona si sahihi kupoteza muda na pesa kwa mtu aliyeamua ushindi kwa gharama yoyote.
 
Back
Top Bottom