Kesi za kikatiba kudai Tume Huru na ile ya kupinga sheria ya uchaguzi zinataanza kusikilizwa lini mahakamani?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kwa sasa hakuna kesi za kikatiba ambazo ni muhimu kwa Taifa hili kama hizi kesi mbili hivyo tungependa kujua kesi hizi zimepangwa kuanza kusikilizwa lini maana 2020 sio mbali.

Iwapo kesi hizi zitacheleweshwa mpaka uchaguzi mkuu wa 2020 unawadia, nawashauri mawakili wa upande wa mashitaka kufungua kesi mahakamu kuu kuiomba mahakama izuie kufanyika uchaguzi mkuu wa 2020 mpaka kesi ya msingi iishe vinginevyo 2020 hakuna uchaguzi bali tutashuhudia yale tulioyaona katika uchaguzi mdogo wa majimbo Kinondoni na Siha.

Na je hizi kesi zimeshapangiwa majaji wa kuzisikiliza?

Ila nikiwaza na uteuzi wa hawa majaji wapya,hakika kichwa hakitulii kabisa.

Nawasilisha.
 
Ni akina nani wanazisimamia hizi kesi? Kama ni wale walioambiwa ni wanaharakati, basi sahau maana waliambiwa hawatapewa ushirikiano, si unakumbuka ya tls ni mali ya umma au?
 
Kwa sasa hakuna kesi za kikatiba ambazo ni muhimu kwa Taifa hili kama hizi kesi mbili hivyo tungependa kujua kesi hizi zimepangwa kuanza kusikilizwa lini maana 2020 sio mbali.

Iwapo kesi hizi zitacheleweshwa mpaka uchaguzi mkuu wa 2020 unawadia, nawashauri mawakili wa upande wa mashitaka kufungua kesi mahakamu kuu kuiomba mahakama izuie kufanyika uchaguzi mkuu wa 2020 mpaka kesi ya msingi iishe vinginevyo 2020 hakuna uchaguzi bali tutashuhudia yale tulioyaona katika uchaguzi mdogo wa majimbo Kinondoni na Siha.

Na je hizi kesi zimeshapangiwa majaji wa kuzisikiliza?

Ila nikiwaza na uteuzi wa hawa majaji wapya,hakika kichwa hakitulii kabisa.

Nawasilisha.
Kamuulize Mama yako fatuma..
Hivi ungekuwa hauna uhuru ungepata wasaha wa kupost haya?
 
Back
Top Bottom