Kesi za epa-wafanyakzi wa bot jela miaka 5

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
Wafanyakazi wa bot ambao walikuwa wanshatakiwa kwa kesi zile epa kutoka kitengo cha madeni ya nje, wamapatikana na hatia katika hukumu ilyosomwa jioni na kuhukumiwa miaka 5 jela

source: Mahakamani jioni hii
 
Tukumbushe majina yao Mkuu maana nakumbuka wachache kama Imani Makosya, Esther Komu, Bosco Kimela na wengine wawili sikumbuki. Sema wana kesi tofauti tofauti. Dah!!
 
changa la macho hilo!! Wafanyakazi wa hali ya chini ndo wanaenda jela!!! Yale mafisadi papa wala hayataguswa!!!
exactly mkuu, hawa walipewa amri watoe pesa, wengi wao ni maskini wa kutupa, wale waliotajirika na hizi pesa, rostam, lowasa, mangula, jk wako mtaani wakijinafasi.
Mungu atakuwa na hawa
 
exactly mkuu, hawa walipewa amri watoe pesa, wengi wao ni maskini wa kutupa, wale waliotajirika na hizi pesa, rostam, lowasa, mangula, jk wako mtaani wakijinafasi.
Mungu atakuwa na hawa

Ni kweli mkuu, nasikia ni instructions tu zilikuwa zinatoka na wanaamriwa wakatekeleze hata kama ni week end walikuwa wanaitwa na kupigiwa simu na wakubwa ili kufuatilia kama mzigo uko tayari. Wametolewa Kafara kabisa hawa. Hawakuwahi kuwa na kampuni ya kuuiba hela ya EPA.
 
Du! hao si sawa na wasogeza mafail mezan messengers, ndowanao fungwa, watia saini na pesa mfukoni kitaani! duuu
 
Sasa ofisini nitakuwa makini kila dili la mkubwa nitakuwa mjanja maana ukikubali kila kitu hawa hawakawii kukutumia kama karai na kukuacha hapa inabidi kuwa mbishi hata kama una njaa
 
Sasa ofisini nitakuwa makini kila dili la mkubwa nitakuwa mjanja maana ukikubali kila kitu hawa hawakawii kukutumia kama karai na kukuacha hapa inabidi kuwa mbishi hata kama una njaa

Kweli mkuu, yaani hawa mabosi wanatupeleka pabaya kabisa!! Kuna wakati nilishakataa kusaini file la boss wangu miaka hiyo maana alikuwa mzungu asiye mwaminifu kama Technical Expert mimi nikiwa kama incharge wa mambo yote ya finance and adminisrtation. Alinitolea macho na sikuogopa!!
 
huo ni uonevu tuuuuu!mafisadi papa wanatesa mtaani,masikini ndiye anayehukumiwa.Tangu lini mwizi anaambiwa arudishe hela thn anasamehewa?
 
Wafanyakazi wa bot ambao walikuwa wanshatakiwa kwa kesi zile epa kutoka kitengo cha madeni ya nje, wamapatikana na hatia katika hukumu ilyosomwa jioni na kuhukumiwa miaka 5 jela

source: Mahakamani jioni hii

Hawa kina Liyumba, Mwakosya, Komu, Bosco ni changa la macho tu, tunawataka Kagoda, Meremeta, Deepgreen,Richmond,Kiwira Coalmine nk. EPA sinior wako wapi, hawa ni vichelema tu.
 
sasa hao kwa nini wasingesema tu ukweli,au wameamua kufa na tai shingoni.!
 
Wafanyakazi wa bot ambao walikuwa wanshatakiwa kwa kesi zile epa kutoka kitengo cha madeni ya nje, wamapatikana na hatia katika hukumu ilyosomwa jioni na kuhukumiwa miaka 5 jela

source: Mahakamani jioni hii

Habari za uhakika ni kwamba wafanyakazi wa BOT wameamriwa kulipa fidia na kila mmoja amesomewa hukumu yake kwa jinsi alivyoshiriki na kama akikosa faini basi watafungwa. Njoja nipate details za hukumu ya kila mmoja halafu nitawatundikia wakuu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom