Testar
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,606
- 12,813
1.KESI DHIDI YA MKE:
Jamaa mmoja liyejulikana kwa jina Peter Wellis alimpa talaka aliyekuwa mke wake na hakutaka kumlipa fidia.Hivyo alimshtaki kwa kosa la wizi wa mbegu zake za kiume kwa madai kwamba hakumtaarifu kama alikuwa akitumia njia za uzazi wa mpango.
2.KESI DHIDI YA KITUO CHA REDIO:
Mwanamke mmoja kwa jina la Cathy McGowan wa US alishinda shindano la kujibu swali kwenye kituo cha redio.Kituo hicho kiliahidi mshindi angepewa gari aina ya Renault Clio, lakini Mama huyo alipofika alipewa mdoli wa gari [Toy car].Alifungua kesi dhidi ya kitu cha redio, alishinda na kulipwa $28,000.
3.KESI DHIDI YA McDonald's:
Mwanamke mmoja wa New Mexico US, alinunua kahawa kwenye mgahawa wa McDonald na kuweka kikombe katikati ya magoti yake ili aongeze cream na sukari.Wakati wa kufungua kikombe kahawa ilimmwagikia na kuungua.Alifungua kesi dhidi ya McDonald akiwalaumu kwa kuuza kahawa ya moto zaidi.
4.KESI DHIDI YA MUNGU:
Mfungwa mmoja huko Romania, Pavel M. baada ya kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kuua, alimshitaki Mungu kwa kushindwa kumkinga na vishawishi vya Shetani.Kesi ilitupiliwa mbali mwishowe.
5.KESI DHIDI YA MJANE:
Mwanamke mmoja aliyemkuta mwendesha pikipiki amefia kwenye barafu, alimshitaki mke wa marehemu kwa sababu kifo cha mumewe kilimsababishia matatizo ya kisaikolojia baada ya kushuhudia kifo cha mumewe.
6.KESI DHIDI YA MWENYE NYUMBA:
Watoto wawili, Jeffrey Kline na Bret Birdwell waliunguzwa na waya wa umeme usio ungwa vizuri wakati wakijaribu kuingia nyumbani kwa mtu bila ruhusa.Watoto hao walimshitaki mwenye nyumba kwa kosa la kuto kuunga waya wa umeme vizuri na kisha wote kwa pamoja walipewa fidia ya $24.2M.
7.KESI DHIDI YA KITUO CHA TV:
Mwanamke mmoja wa Israel alishitaki kituo cha TV kwa utabiri fake wa hali ya hewa.
Kwa mujibu wa Mama huyo, kituo cha TV kilitabiri hali ya hewa kuwa nzuri na yeye bila wasiwasi alivalia mavazi mepesi.Bahati mbaya mvua ilinyesha na akapatwa na homa.Alishitaki kituo cha TV na kulipwa fidia pamoja na gharama za matibabu.
8.KESI DHIDI YA KLABU YA USIKU:
Mwanamke mmoja, Kara Walton alitaka kuingia Klabu ya usiku kupitia dirisha la chooni ili asilipe kiingilio cha dola tatu na nusu.Matokeo yake alianguka na kuvunjika meno mawili ya mbele.Aliishtaki ile Club na mwisho wa kesi alilipwa $12,000 pamoja na kulipiwa gharama zote za kutibu meno.
9.KESI DHIDI YA CHUO:
Mwaka 2009 Trina Thompson NY, alifungua kesi ya kukishitaki chuo cha Monroe alikohitimu degree ya IT kwa kukosa kazi ya maana miezi kadhaa baada ya kuhitimu.Msichana huyo alitaka chuo kimrudishie gharama za ada alizotumia.Alitaka alipwe $ 72,000 kama fidia.
10.KIBAKA AMSHITAKI MWENYE NYUMBA:
Terrence Dickson alivunja nyumba ya mtu na kutaka kutoka nje kupitia mlango wa garage.
Kwa kuwa mlango wa garage ulikuwa mbovu, aliamua arudi ali apite mlango wa nyumba.Kwa bahati mbaya mlango wa kuingilia garage haukufunguka, kwa kuwa wenye nyumba walikuwa vacation, ilimbidi TD asubiri ndani ya garage kwa muda wa siku nane.Baada ya wenye nyumba kurudi kibaka alifungua kesi akitaka alipwe dola laki tano kama fidia juu ya mfadhaiko na matatizo ya kisaikolojia yaliyompata alipokuwa ndani ya garage.Mwisho wa kesi jamaa alilipwa fidia yote.