Kesi ya Zombe na Kauli ya Rais: Tusisahau wafanyabiashara wa wahenge

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,907
2,768
Mh. Rais kauli yako kuhusu majambazi tumeisikia, lakini Mh. Ningependa kukumbusha kuhusu wafanyabiashara wa mahenge waliosemekana majambazi wakapigwa risasi na kuuwawa.

Naamini kipindi hicho ulikuwa waziri wa ujenzi na hawa wafanyabiashara walikuwa wamekuja Dar es Salaam wakiwa na madini yao, waliishia kupigwa risasi na askari wakisemekana ni majambazi. Hili suala lilienda mahakamani na nashukuru Mh. Kikwete hakuta kufunika kombe mpaka mahakama ilipomtia hatiani Bageni (OCD) kinondoni kunyongwa.

Mh. Majambazi ni watu hatari na kama jamii tungependa kusiwepo na watu wa aina hii lakini ni muhimu kujihakikishia kila jambazi anayeuwawa ni jambazi kweli? Isiwe tiketi ya kuuwa raia wasiokuwa na makosa na kuporwa mali zao kisha wakasemwa ni majambazi.

IGP naomba katika utendaji wenu mzingatie ukweli na sio kutokea matukio ya kudhurumu raia na kuwabambikizia kesi za ujambazi, mwisho wa siku tutajibu kwa mola.

Natanguliza shukrani.
 
Semina elekezi ni muhimu sana kwa viongozi wa umma ili kuweza kuzifahamu kwa undani na kutekeleza maadili, kanuni na sheria zinazosimamia mambo mbalimbali hapa nchini.
 
Nasikia wakati wa JK wengi mliomba Tz tupate Rais kichaa/Dikteta na mkaomba kwenye nyumba za Ibada Mungu bila Hiyana kawapa "Malaika Mkuu"
so pambaneni na hali zenu

Enzi za Nabii Samweli (Biblia), Israel walilia kupewa Mfalme wawe kama mataifa mengine wakapewa Sauli.
 
Policcm wataitumia hii kuendelea kunyonga akina Aqwilina, Mawazo..
na kuna siku utasikia kiongozi wa upinzani apigwa risasi katika tukio la ujambazi..
Kwani jizi la kura nalo si jambazi ?
maana nalo linanyang'anya kwa kutumia bunduki..
kwa nini libaki hai ?
 
dah, sa kwanini alisema asipelekewe majina ya waliohukumiwa kifo kutia saini? kama anasema hivi... what is hypocrazy?
 
Jamaa linajiona dunia yote kaiweka mkononi na ataishi milele na hicho cheo chake maana ana kibri kupita maelezo ila akae akijua yeye na hao watu zake ipo siku wataenda kujibu mbele ya muumba wetu.
Ni muhimu sana kutenda haki kwa raia, polisi nao ni binadamu, kuna wanaozingatia maadili na wasiozingatia
 
Nasikia wakati wa JK wengi mliomba Tz tupate Rais kichaa/Dikteta na mkaomba kwenye nyumba za Ibada Mungu bila Hiyana kawapa "Malaika Mkuu"
so pambaneni na hali zenu

Enzi za Nabii Samweli (Biblia), Israel walilia kupewa Mfalme wawe kama mataifa mengine wakapewa Sauli.
Mwisho wa Mfalme Sauli ulikuwaje? kasome biblia yako vizuri.
 
polisi na muumba wapi na wapi,mbele ya polisi hakuna cha muumba upolisi ni uwekezaji.
 
Nasikia wakati wa JK wengi mliomba Tz tupate Rais kichaa/Dikteta na mkaomba kwenye nyumba za Ibada Mungu bila Hiyana kawapa "Malaika Mkuu"
so pambaneni na hali zenu

Enzi za Nabii Samweli (Biblia), Israel walilia kupewa Mfalme wawe kama mataifa mengine wakapewa Sauli.
Hatukuomba dikteta Mpumbavu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wengi wataonewa na polisi watapata kiburi kwa kuwa hawatafanywa kitu
 
Jamani tujitolezeni kwa wingi tukaue majambazi......Maana tumeambiwa tuwe tunasaidia polisi, sasa polisi wenyewe hawawezi kuwamaliza wote.....ile dhana ya kusema usijichukulie sheria mkononi naona imeamuliwa kufutwa
 
Back
Top Bottom