Kesi ya zombe, Bageni akiri kudanganya tume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya zombe, Bageni akiri kudanganya tume

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 12, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,770
  Trophy Points: 280
  Mauaji: Baada ya Zombe, Bageni akiri kuidanganya TUME
  *Afichua kuwa waliidanganya Tume ya Rais

  James Magai


  MSHITAKIWA wa pili katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva teksi wa Manzese Dar es Salaam, Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni amezidi kumuweka pabaya mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe.


  Bageni na wenzake tisa, akiwemo Zombe, wanashitakiwa kwa tuhuma za kuwaua wafanyabiashara watatu wa madini ya rubi kutoka Mahenge mkoani Morogoro- Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva wa teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu.


  Bageni alidaiwa na Zombe kuwa ndiye aliyeamuru wafanyabiashara hao kuuawa, lakini jana alimshambulia Zombe kuwa muhusika mkuu. Hadi sasa, mtuhumiwa mmoja katika kesi hiyo, Koplo Saad Alawi, ambaye anadaiwa kufyatua risasi na kuwaua wafanyabiashara hao, hajakamatwa.


  Katika utetezi huo uliodumu kwa saa sita, Bageni aliieleza Mahakama Kuu kuwa Zombe alimrubuni kuwa wapeleke taarifa ya uwongo kwenye tume ya Jaji Musa Kipenka, iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza ukweli wa vifo vya wafanyabiashara hao.


  Mbele ya Jaji Salum Massatti anayeisikiliza kesi hiyo, Bageni alidai kuwa Zombe alimweleza kuwa walisoma na Jaji Kipenka darasa moja katika Shule ya Sekondari Songea na kwamba ameahidi kuwasaidia katika suala la mauaji hayo.


  “Mshitakiwa wa kwanza aliniambia kuwa Jaji Kipenka ni “classmate” wake... walisoma naye darasa moja Songea Boys na kwamba wamewasiliana na amemwambia kuwa tupeleke taarifa iliyorekebishwa ili awasaidie vijana wetu,” alidai Bageni wakati akijibu maswali kutoka kwa wakili wa serikali, Angaza Mwipopo.


  Bageni alidai kutokana na ushauri huo wa Zombe waliamua kuibadili taarifa waliyoipeleka kwenye tume hiyo, tofauti na taarifa waliyoiandaa ambayo ilipelekwa katika kitengo cha uhalifu, maarufu kama 99.


  Wakati akijitetea, Bageni pia alijikuta akimwaga machozi kizimbani. Hata hivyo tofauti na kilio cha Zombe alichodai ni kuchezewa mchezo mchafu, Bageni alimwaga machozi akimkumbuka dada yake aliyefariki dunia baada ya kusikia kuwa amekamatwa (yeye Bageni).


  “Kwa hiyo uliandika maelezo ya uongo ili kuipotosha Tume ya Rais,” alihoji Wakili Mwipopo.


  Bageni: Si mimi tu, aliyenieleza kwani wapo na wengine pia.


  Mwipopo: Kwa nini uipotoshe tume ya rais wakati unajua ukweli na wewe ni mwaminifu?


  Bageni: Niliamini kuwa kuwasaidia vijana wetu ni jambo jema.


  Mwipopo: Unadhani kufanya hivyo ilikuwa ni halali na ni busara?


  Bageni: Mimi niliona ni busara kuwasaidia na niliona huruma.


  Mwipopo: Kwani walikuwa na tatizo gani mpaka uwahurumie?


  Bageni: Tatizo la mauaji.


  Mwipopo: Kwa nini uliandaa taarifa hiyo ya uwongo?


  Bageni: Mimi nilielekezwa.


  Mwipopo: Kwani ilikuwa ni amri?


  Bageni: Maagizo ya mkubwa ni kama amri.


  Mwipopo: Kwa hiyo hata maelezo uliyoyaeleza, mbele ya tume yalikuwa ni ya uongo?


  Bageni: Hii taarifa mimi nilielekezwa tu na mtu nimwandalie.


  Mwipopo: Kwa hiyo mbele ya tume uliongopa”


  Bageni: Wewe wasema.


  Mwipopo: Mshitakiwa wa kwanza alikuwa na tatizo gani hasa hadi akwambie umsaidie kuandaa taarifa hiyo ya uongo?


  Bageni: Sijui lakini siyo mimi tu ila aliwaambia na wengine hata OCD (mkuu wa polisi wa wilaya) wa Ilala.


  Mbali na kumkaanga Zombe, Bageni pia aliieleza mahakama kuwa maelezo yaliyoandikwa na mshitakiwa wa 11, Koplo Rashid Lema na Koplo Rajabu Bakari ambayo yalitolewa mahakamani hapo kama ushahidi kuwa, ni ya uwongo na kwamba anashangaa na hajui ni kwa nini aliamua kuyasema hayo.


  Washitakiwa hao katika maelezo yao, pamoja na mambo mengine, walieleza kuwa wafanyabiashara hao waliuawa katika Msitu wa Pande na kwamba, msafara wa kwenda huko uliongozwa na Bageni ambaye aliwaeleza kuwa Zombe aliagiza wachinjwe, na kwamba baadaye Bageni alimshinikiza mtunza silaha wa kituo cha Oysterbay abadili taarifa ya urejeshaji wa silaha.


  Ingawa Bageni alidai hajawahi kukosana na mshitakiwa wa 12, alikiri kuwa alikuwa na tofauti za maelewano na mshitakiwa wa 11, baada ya kumchukulia hatua kutokana na tuhuma za kuvunja na kuiba pesa katika kantini ya kituo cha polisi cha Oysterbay.


  Bageni alidai kuwa awali mshitakiwa wa 11 alikuwa dereva wake kabla ya kumtoa kutokana na tuhuma hizo ambazo alisema alizichunguza na kupata ukweli, hivyo akampelekea jalada OCD wake, SSP Edward Maro.


  Alidai kuwa OCD huyo alikaa na jalada hilo kwa muda mrefu na ndipo baadaye akamrudishia na kumweleza kirafiki kuwa, kwa kuwa alikuwa anataka kustaafu asingependa kuwaharibia vijana na kwamba wanatoka naye Kilimanjaro.


  “Sikukubaliana naye hivyo nilipeleka taarifa kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) kwa sababu siwezi kukaa na askari jambazi,”alisema Bageni.


  Sambamba na mshitakiwa huyo pia Bageni alidai kuwa hata shahidi wa 30, ACP Mmari, ana uhasama naye wa siku nyingi wakati wakifanya kazi Moshi, akidai kuwa Mmari alikuwa anataka gari ili aende nalo kwao hata kwa kukodi, lakini akamkatalia kuwa hana gari zaidi ya lile la serikali na ndipo uhasama wao ukaanza.


  Katika mahojiano na wakili wa upande wa mashitaka, Bageni alikiri kuwa alifika katika eneo la ukuta wa Posta, Sinza mahali ambapo ilidaiwa kuwa kulikuwa na mapambano siku moja baada ya tukio na kwamba, ingawa aliona mashimo kwenye ukuta yaliyodaiwa kuwa ni ya risasi, lakini hakuweza kuona damu katika eneo hilo.


  Wakati akimuweka Zombe katika mazingira magumu, Bageni aliwajengea mazingira mazuri washitakiwa watatu baada ya kuieleza mahakama kuwa siku hiyo wao walikuwa katika eneo tofauti na eneo hilo.


  Bageni alidai aliambiwa na mkuu wa upelelezi wa kituo cha polisi cha Chuo Kikuu, James Masota kuwa alikuwapo kwenye tukio hilo na kwamba siku hiyo washitakiwa hao Emmanuel Mabula (mshitakiwa wa saba), Michael Sonza (9) na Festus Gwabisabi (13), walikuwa kwenye doria Makongo Juu.


  “Alidai wakati wakirudi kutoka Makongo juu kupeleka kundi hilo, walipitia Chuo cha Ardhi ndipo waliposikia taarifa za tukio la uporaji wa fedha za kampuni ya Bidco na ndipo walipoenda huko,” alidai Bageni.


  Awali wakati akitoa ushahidi wake jinsi alivyopata taarifa za tukio la Bidco, huku akiongozwa na wakili wake Gaudiz Ishengoma, Bageni alionekana kumtengenezea mazingira mazuri Zombe kabla ya upepo kubadilika.


  Bageni alidai Zombe alifika kituo cha polisi cha Urafiki baada ya kuitwa na OCD wa Magomeni, SSP Kisuto Matage kwa ajili ya makabidhiano ya vielelezo ambavyo inadaiwa vilikamatwa kwa wafanyabiashara hao watatu.


  Alidai kuwa hakuwepo kwenye tukio hilo na kwamba, alipata taarifa hizo majira ya saa 1:30 alipofika kituoni akitokea kwenye eneo lake la ujenzi Pugu na kwamba aliarifiwa na askari wa zamu kuhusu tukio la uporaji wa fedha za Bidco.


  Alidai muda mfupi aliitwa na OCD wake Matage na alipojaribu kumueleza kuhusu tukio hilo, Matage alionekana kulijua na ndipo akamwambia kuwa, majambazi hao wamekamatwa na akamwagiza afuate vielelezo vilivyopatikana kutokana na tukio hilo katika kituo cha Urafiki, Sh.5mil na bastola moja.


  Alidai wakiwa kituoni hapo, OCD Matage alimtuma mshitakiwa wa tatu, ASP Ahmed Makelle apeleke vielelezo hivyo na kwamba baada ya kuzihesabu, zilikuwa zimepungua badala ya Sh 5milioni zilikuwa Sh2.3 milioni.


  Kutokana na upungufu huo, Bageni alikataa kuzipokea na ndipo Matage akatikisa kichwa na kumuita Zombe, ambaye baada ya kufika na kupewa taarifa za upungufu huo alikasirika na kuagiza pesa hizo zipatikane kesho yake kisha akaondoka.


  “Zombe alisema zilitangazwa redio na kila mwenye redio alisikia kuwa ni Sh5 milioni ndipo nilizichukua zilizobaki na kuondoka kurejea kituoni kwangu,”alidai.


  Alidai baadaye ndipo OCD wake alipomueleza kuwa wale majambazi walikuwa wamefariki dunia na kwamba, usiku huo kulikuwa na mfululizo wa matukio ya uhalifu kiasi kwamba alifanya kazi hadi saa 11:00 alipomaliza kuandika taarifa za matukio hayo na kuziweka ofisini kwa OCD ndipo akaondoka kwenda nyumbani.


  Alidai akiwa nyumbani asubuhi hiyo, OCD wake alimpigia simu na kumweleza kuwa wanahitajika kwa Zombe na baadaye akampitia na kwamba wakiwa njiani alimuuliza kama zile pesa zilikuwa zimepatikana.


  “Wewe unamchezea Zombe, Matage alizileta usiku,” alidai akimkariri OCD wake SSP Maro.


  Alidai walipofika ofisini walikuta Ma-OCD wengine na baadaye wakamkabidhi Zombe fedha hizo na baada ya kuzihesabu, Zombe akampa azipeleke kwa ofisa mmoja aliyekuwa akiandaa mkutano kati ya Zombe na waandishi wa habari asubuhi na baadaye wakatawanyika.


  Katika maelezo yake mengi juu ya tukio hilo ambayo baadaye yalionekana tofauti na yale aliyokuwa ameyaandika katika tume ya Jaji Kipenka na kwenye timu ya upelelezi ya tukio hilo, Bageni aliiomba mahakama imuhukumu kwa maelezo aliyoyatoa mahakamani hapo jana na kwamba mengine ni ya kupikwa.


  Hata hivyo katika mahojiano na wakili wa serikali Mwipopo, Bageni alijikuta katika wakati mgumu na alilazimika kuyakataa maelezo aliyowahi kuyaandika
   
 2. vengu

  vengu JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2016
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 518
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 60
  duh
   
 3. N

  NEPTUNE JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2016
  Joined: Jan 8, 2013
  Messages: 546
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 60
  Unaenda mahskamanumahskamani kutetea washtakiwa wenzio hapo lazima ubebe msalaba wao.
   
 4. s

  sienta Member

  #4
  Sep 17, 2016
  Joined: Jul 13, 2016
  Messages: 71
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 25
  OK wajifunze
   
 5. UncleBen

  UncleBen JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2016
  Joined: Oct 27, 2014
  Messages: 9,095
  Likes Received: 9,705
  Trophy Points: 280
  Huyo Zombe kama hukumu ya mahakama imeshindwa kumtia hatiani na kama kweli alihusika siku sio nyingi atavuna alichopanda
  Damu ya mtu haipotei
   
 6. f

  ffq Senior Member

  #6
  Sep 17, 2016
  Joined: Oct 24, 2015
  Messages: 173
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  sjaelewa kitu wale wafanyabiashara waliuwawa hapo posta sinza na sio msituni???...
   
 7. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2016
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 80
  Ninavyokumbuka kutokana na habari wakati huo, wafanyabiashara waliuawa msituni huko kwingine (Posta na Sinza) walidai ndiko walikofyatuliana risasi na hao "majambazi" ndio maana kasema kulikuwa na alama za risasi Sinza lakini hakukuwa na damu..
   
 8. f

  ffq Senior Member

  #8
  Sep 17, 2016
  Joined: Oct 24, 2015
  Messages: 173
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  thanks....akipatikana mwenye info kamili atatusaidia....hii kitu ilikua hatar sn....dah
   
 9. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2016
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,405
  Likes Received: 6,591
  Trophy Points: 280
  fiat justitia ruat coelum
   
 10. T

  TRUVADA JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2016
  Joined: Jan 6, 2014
  Messages: 4,529
  Likes Received: 1,178
  Trophy Points: 280
  zombe mganga aliyempata asimwaachie
   
 11. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2016
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Huyu Zombe afunguliwe mashtaka upya
   
 12. Madrid86

  Madrid86 JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2016
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 1,251
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  Duuuh unaweza tengeneza movie ya ukwel ya hili tukio.
   
 13. Hansss

  Hansss JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2016
  Joined: Jul 17, 2015
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,483
  Trophy Points: 280
  KWA USHAHIDI UPI MKUU ULIOUANDAA MAANA ULE WA TOKEA 2006-2016 HAUKUTOSHA KUMTIA HATIAN
   
 14. MKWEPA KODI

  MKWEPA KODI JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2016
  Joined: Nov 28, 2015
  Messages: 18,227
  Likes Received: 37,132
  Trophy Points: 280
  Wavunja UKUTA wana learn the hard way
   
 15. bonga basiri

  bonga basiri Member

  #15
  Sep 17, 2016
  Joined: Sep 4, 2016
  Messages: 19
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  Hayo ndiyo yanayo fanyika jaman kwa vyombo vyetu vya usalama
   
 16. muhomakilo jr

  muhomakilo jr JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2016
  Joined: Jul 28, 2013
  Messages: 10,146
  Likes Received: 3,248
  Trophy Points: 280
  Huyu Zombe atakufa kifo kibaya Sana...
   
 17. Root

  Root JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2016
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,307
  Likes Received: 13,016
  Trophy Points: 280
  Watoto wa hao waliouawa walisoma shuleni kwetu
  Nakumbuka siku hiyo walilia sana darasani
   
 18. tutafikatu

  tutafikatu JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2016
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,525
  Likes Received: 1,332
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani ushahidi upi umemtia hatiani Bageni?
   
 19. sifi leo

  sifi leo JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2016
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 1,957
  Likes Received: 1,484
  Trophy Points: 280
  Bageni, kumbuka dadako alikufa baada ya kusikia kuwa umekamatwa sasa subiri Broo MAGU,asaini unyongwe umfate dada yako.
   
 20. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2016
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Lishukuriwe gazeti la mwananchi. Wao ndiyo waliokuwa wa kwanza kutilia shaka taarifa ya Police kuwa waliouwawa ni majambazi.
   
Loading...