Kesi ya Zitto vs CHADEMA:Kuna mazingira yanaandaliwa ku-influence uamuzi wa mahakama

lakini kwanini huyu jamaa asianzishe chama chake, maana anaonekana ana wafuasi wengi sana!

Huyu mhaini alishatangaza siku nyingi kuwa anataka kuachana na siasa ili akafundishe, hivyo jukumu alilopewa na mabosi wake hapo Lumbumba ni kuivuruga Chadema kabla hajaacha siasa na ametengewa fungu kubwa sana kwa kazi hii, na kinachoendele sasa ni utekelezaji wa jukumu hilo.
 
Mpaka sasa hvi ni mambo mengi yemedhihilisha Zitto hana mapenzi mema kwa Chadema. Hata kama hakufanya kosa, amepoteza sifa zote za kuendelea kuwa mwanachama. Hao wote wanao shabikia Zitto inabidi wote watolewe kama wana uongozi wowote katika Chama. Kwa sasa aliyenyuma ya Zitto ni adui wa Chadema.
 
Kamanda tulishalitambua hili, ni ukweli usiopingika, hapa hatushindani na Zitto bali tunashindana na ccm na vibaraka wake wachumia tumbo, si uliwaona jana hapo mahakamani, tangu lini ccm wamshabikie mtu wa chadema, ila wamegonga mwamba, chadema itazidi kuchanja mbuga.
 
zitto akishinda nikwanguvu za giza tu. chadema tunaamini mungu atasaidia.tunatambua uwepo wa mtandao wa zitto unaundwa na maccm na wengine wasio penda haki hapa tz
 
Naomba niseme tu yaliyokuwa yanaendelea na yanayoendelea mpaka muda huu kuhusu kesi ya Zitto nje ya mahakama na hata kupitia baadhi ya vyombo vya habari, ni mkakati wa makusudi wa maadui wa CHADEMA wanaojifanya ni wapenzi na mashabiki wa Zitto wenye lengo la ku-influence mahakama itoe uamuzi unaolenga kumbeba Zitto.

Zitto kama Zitto hawezi kuwa na nguvu kiasi hiki na isitoshe jambo hili linahitaji matumuzi makubwa ya fedha na rasilimali watu.Huu bila shaka ni mkakati unaoungwa mkono na baadhi ya vyama vya siasa na matajiri "uchwara" kadhaa wa ndani ya nchi.

Haihitaji kuwa na degree kubaini ukweli huu bali ni swala la kusoma ushahidi wa kimazingira tu(circumstantial evidence)

CHADEMA,kwa sasa adui yenu si Zitto tu,bali adui yenu mkubwa ni mtandao ulio nyuma ya Zitto.

Unaota wewe! Unaishi kwa kudanganywa. Ishi kwa akili yako binafsi inaonekana kichwa chako Mbowe na Slaa wanakimiliki %90.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
zitto akishinda nikwanguvu za giza tu. chadema tunaamini mungu atasaidia.tunatambua uwepo wa mtandao wa zitto unaundwa na maccm na wengine wasio penda haki hapa tz
Kha! Unachekesha kweli! Basi Mungu wako wa ajabu kweli.


Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
cuf na ccm jana wameleta wafuwasi wao kwa kuwavesha kofia za chadema na kuwapa bendera za chadema, kwa nguvu inayo tumiwa na ccm na serekali yake dhidi ya chadema, chadema kina itaji nguvu ya mungu ili kupona.

We Kweli kbosho , tulia tu , nguvu ya mungu yaani huyu huyu anaichukia wazinzi, wazi , wajokwezao, wafilaji, waongo na wasengenyaji?
Labda mungu wa kibosho
 
mfa maji hakosi kutapatapa ZZK bado ni akili kubwa kuliko CDM ndo basi tena chezea ZZK manyang'au nyinyi!!!!!!!!!!!
 
Unaona mbali ndugu. Hii inanikumbusha uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 huu mtandao ulipofaulu kwa kiasi kikubwa kuizima na kuizamisha nguvu ya NCCR mageuzi kwa kumtumia Mabere Marando na mahakama. Tulidhani wakati ule ni ugomvi ndani ya NCCR lakini baada ya uchaguzi ndio ukweli ulipojidhahirisha (Marando alizawadiwa na chama tawala ubunge wa E. Afrika). 'It was too late for us to realize' kuwa tumekihama chama chenye mwelekeo wa fujo kumbe zilikuwa rafu za kupandikizwa. Wakati huu tunawaambia 'hatudanganyiki tena!!'
 
Kinacho nishangaza nikuona watu na makunzu mahakamani utadhani wapo msikitini,kulikoni.
 
Kila njia ya mafanikio haikosi wanafiki, wasaliti watakao jifanya wako na wewe kumbe lao ni kukuchunguza unafanya nini ili wakuzibie njia usitoke, sio wote wanao kwenda msikitini wanaenda kuswali wengine wapo kuvizia tu marapa ya wenzao.
Hili jambo likowasi tu nguvu ya cdm inainyima usingizi ccm, hivyo lazima tu watafute mianya ya kujinasua, kila cdm inapo jipanga kusonga mbele upande wa pili wanawaza njia ya kutegua, hapo ndio kila mbinu inapo tumika ikiwemo kuwa tumia wale walioko kwenye msafara wa kenge kumbe wao mijusi tu wanao vujisha siri.
 
Back
Top Bottom