Kesi ya Zitto vs CHADEMA:Kuna mazingira yanaandaliwa ku-influence uamuzi wa mahakama

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
1,195
ni hatari sana kum-underestimate adui yako wakati bado hata hamjaanza mapigano....mlimdharau Zitto mkidhani is a lone wolf...mtakoma

Mkuu hawa jama wameshafanya kila hapa nchini ni mali yao,zile kesi walizokuwa wanashinda kwa kuhonga pesa kutoka kule Marekani walidhani na hii ni nyanya tu,si unakumbuka isiku ya kwanza ya kesi walivyokuwa wanabeza na kukenua?!
 

Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,824
1,225
Nakumbuka hata kipindi kile Rostam Azizi alipojing'atua na SIASA UCHWARA za adharani, watu wengi walilia na wengine kuzimia.
 

DZUDZUKU

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
3,858
2,000
Kinachoendelea cdm, "ukinipiga/ ukinifikuza umenionea, ukiniacha/usiponifukuza umeniogopa"
 

m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,369
2,000
ni hatari sana kum-underestimate adui yako wakati bado hata hamjaanza mapigano....mlimdharau Zitto mkidhani is a lone wolf...mtakoma

Tulijua yupo pamoja na ccm! ni mamluki wao hivyo hata haya yanayoendelea tuliyategemea!
 

ndenga

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,764
2,000
Baada ya kesi kuisha leo ZZK atakuwa na cheo kingine cha Mbunge wa Mahakama mpaka mwakani October 2015.. then ataachana na Siasa..
 

KIGENE

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,501
2,000
Hizi sarakasi haziwezi kamwe kumsaidia Zitto hatima yake ipo mikononi mwa CDM yatafanywa na kusemwa mengi lakini mwisho wa siku uwepo wake kwenye chama hautaamuliwa na wapambe waandamanaji vyama vya siasa wala mahakama bali CDM.
Kwa hali yoyote ile itakavyokuwa inaonekana kuendelea kwake kuwa mwanachama ni kama hakuna tena,nafikiri naye alilijua hili kabla hajaenda mahakamani,kwa sasa hata hilo Baraza kuu analolitaka sidhani kama linaweza kumuunga mkono tena.
 

Bugota

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
265
250
Jamani mi naomba kupata Updates juu ya kinachoendelea Mahakama kuu maana sioni uzi unaotoa Live Updates kama ilivyokuwa jana...
 

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,017
1,500
He he he, mlitiwa kujua nguvu ya adui yenu kabla ya vita hii. Kama yuko ndani ya mtandao, bsi mtandao huo ndio nguvu yake.

Acheni kupiga makelele wakati vita ishaanza, komaeni na vita hadi kieleweke. Hii ni sawa na kuomba PO.
 

kabungu

Member
Dec 1, 2013
9
0
Naomba niseme tu yaliyokuwa yanaendelea na yanayoendelea mpaka muda huu kuhusu kesi ya Zitto nje ya mahakama na hata kupitia baadhi ya vyombo vya habari, ni mkakati wa makusudi wa maadui wa CHADEMA wanaojifanya ni wapenzi na mashabiki wa Zitto wenye lengo la ku-influence mahakama itoe uamuzi unaolenga kumbeba Zitto.

Zitto kama Zitto hawezi kuwa na nguvu kiasi hiki na isitoshe jambo hili linahitaji matumuzi makubwa ya fedha na rasilimali watu.Huu bila shaka ni mkakati unaoungwa mkono na baadhi ya vyama vya siasa na matajiri "uchwara" kadhaa wa ndani ya nchi.

Haihitaji kuwa na degree kubaini ukweli huu bali ni swala la kusoma ushahidi wa kimazingira tu(circumstantial evidence)

CHADEMA,kwa sasa adui yenu si Zitto tu,bali adui yenu mkubwa ni mtandao ulio nyuma ya Zitto.

Acha kuweweseka
 

martin mwamlima

Senior Member
Oct 31, 2013
146
225
Mara ya tatu? umewekewa na link hapo juu tu post ya #3 , hawa watu si wema saa hizi subiri timbwlitimbili huko HC
pia kuna Thread kibao za Zitto naona zinaminywa
tusizichangie ni kwa nini Mods?
Unyama: Mwenyekiti wa CHADEMA Temeke ambaye chama hicho kinamtuhumu kushirikiana na CUF kumuunga mkono Zitto avamiwa usiku na kupigwa nusura auawe - MPEKUZI
1.jpg


Si muda mrefu nilipost thread 'bias ya jf' nikatoa mfano wa thread Za Zito. Wengi walikubaliana na Mimi. Lakini wameiondoa. Wameshakuwa wanasiasa wa upande mmoja
NADHANI MODS HAWAKO HURU
 

The Invincible

JF-Expert Member
May 6, 2006
5,988
2,000
ZZk akifanikiwa kubaki CHADEMA lazima alipe fadhila,sasa jiulize atalipa fadhila kwa gharama ya nani kama sio kuhujumu chama?

Salary Slip
Trust me. Zitto is finished in Chadema. Hata mahakama ikimbakisha, atakuwa mwanachama kwa mujibu wa mahakama tu. Mwaka huu huu vumbi lita-settle.
 

twijuke

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
548
500
Ndugu wana janvi poleni na majukumu ya ujenzi wa Taifa letu, na kwa wale wabomoaji wa taifa letu tusema basi inatosha.

Wapendwa ndugu zanzgu, wakati CCM wameazimia kuvua kile walicho kiita GAMBA,Kuna swali nilijiuliza. Ikiwa CCM wamefika mahali na kuona ndani ya chama kuna watu wachafu na hivyo iliwapasa kuwaondoa maana yake lilikuwa ni tatizo. Swali hapa lilikuwa je! ikiwa ni tatizo je nguvu ya kushugulikia tatizo inalingana na ukubwa wa tatizo? na jingine ilikuwa ni je hesabu zimezingatiwa?

Tukumbuke watu walio daiwa kuwa ni wachafu ndani ya CCM, ni wale wanao tajwa kwa dhati kabisa kuiingiza serikali iliyopo madarakani,lakini si tu kuiweka serikali iliyopo madarakani baali mchakato mzima katika uungwaji mkono ulipelekea hawa watu kuwa na wafuasi wengi ndani ya chama, jambo ambalo lilifanya zoezi zima la uvuaji gamaba kuwa gumu.

Ndugu zangu suala la kumvua Zitto madaraka na mwenzie Dk. Mkumbo binafsi nakifananisa na kitendo cha CCM kuvua gamba ambalo hadi leo wote tu mashahidia ugumu wa uvuaji gamba. Kwa sasa tunapo taja vyama pinzani hapa Tanzania CHADEMA ni Mbuyu, na kama ni Mbuyu wanasema Mbuyu nao ulianza kama mchicha.


Leo Chadema kinaonekana ni chama chenye afya njema, linapo kuja sula la nani wameifikisha Chadema kilipo, Naapa tutakuwa hatumtendei haki Zitto kama hatumtaji, naamini kabisa wote tu mashahidi kuwa Zito ni mhusika katika kukinenepesha chama. Kwani umahili wake katika kujenga hoja ndani ya Bunge ni kati ya mambo yaliyo vutia wengi katika siasa za Chadema.

Zitto naye ni binadam, wakati tunamuoona kwa jicho la mabaya tukumbuke kuwa upo utitiri wa meme yake, na kama ndinvyo huenda mema yakawa ni Mlima kuliko makosa ambayo ukubwa wake ni sawa na Kichuuguu.

Lakini lipo swali lingine kuhusiana na suala la Zitto, najiuliza, Je! ikiwa MEMA yake huenda ni kama mlima, alistahiki aachwe? huenda jibu ni hapana, Je! kama ndinvyo adhabu aliyopewa inawiana na kosa? ikumbukwe kuwa si kila majira ya faa kwa kila jambo, kwani jambo laweza kuwa sahihi lakini wakati usiwe sahihi, Je! wakati ulikuwa ni sahihi?


Sifa ya mnene imetokana mwembamba, je tungemtambuaje Mrefu kama si uwepo wa mfupi? Ndugu zangu wana janvi katika nia njema ya kuteanda mema makosa yaweza kufanyika, lakini lipo jingine kubwa, nalo ni kwamba katika kutatua tatizo waweza kusababisha tatizo kubwa kuliko tatizo la awali. Naomba niweke wazi simtetei Zitto ila chondechonde hekima na busara kama havikutumika kwenye hili itakuwa sawa na kusababisha tatizo jingine katika utatuzi wa tatizo.


Mugu tubariki sote.
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,530
2,000
Acha woga! ZITTo aliwaonya sana, mkajifanya vichwa maji! Muli-undersestimate nguvu ya ZITTO! Subiri matokeo tu!

Zitto mtoto mdogo sana ...wala hatusumbui kichwa ..atakuwa mbunge kama alivyo kafulila na hamad rashid lakini chadema imeshamfukuza na hilo analijua
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,530
2,000
Si muda mrefu nilipost thread 'bias ya jf' nikatoa mfano wa thread Za Zito. Wengi walikubaliana na Mimi. Lakini wameiondoa. Wameshakuwa wanasiasa wa upande mmoja
NADHANI MODS HAWAKO HURU

tehh ..pole mwenyekiti naona unavuja michuzi
 

lutayega

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
1,276
2,000
zzk alivyokuja kigoma walisema kwakuwa huko ni kwao na kwamba mikutano yake imejaa wanaccm sasa hapo ni dsm sijui napo wamejaa wanaccm. kama ni hivyo wanachama wa cdm zaidi ya asilimia 90 ni wanaccm
 

Tougher

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
245
195
Naomba niseme tu yaliyokuwa yanaendelea na yanayoendelea mpaka muda huu kuhusu kesi ya Zitto nje ya mahakama na hata kupitia baadhi ya vyombo vya habari, ni mkakati wa makusudi wa maadui wa CHADEMA wanaojifanya ni wapenzi na mashabiki wa Zitto wenye lengo la ku-influence mahakama itoe uamuzi unaolenga kumbeba Zitto.

Zitto kama Zitto hawezi kuwa na nguvu kiasi hiki na isitoshe jambo hili linahitaji matumuzi makubwa ya fedha na rasilimali watu.Huu bila shaka ni mkakati unaoungwa mkono na baadhi ya vyama vya siasa na matajiri "uchwara" kadhaa wa ndani ya nchi.

Haihitaji kuwa na degree kubaini ukweli huu bali ni swala la kusoma ushahidi wa kimazingira tu(circumstantial evidence)

CHADEMA,kwa sasa adui yenu si Zitto tu,bali adui yenu mkubwa ni mtandao ulio nyuma ya Zitto.

Ni hatari sana pale mtu anapokuwa na matatizo kuamua kutafuta mchawi badala ya kujiuliza amefikaje pale alipo na nini afanye kutatua.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom