Kesi Ya Wakina Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi Ya Wakina Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri...

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Risk taker, May 5, 2009.

 1. R

  Risk taker Member

  #1
  May 5, 2009
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya
  wafanyabiashara wa madini, Abdallah Zombe, ameiomba Mahakama Kuu aruhusiwe kutoa tena ushahidi wake mahakamani hapo ili kutoa ufafanuzi kuhusu baadhi barua alizodai kuwa zina utata. Barua hizo ni alizodai ziliandikwa na washitakiwa wenzake katika kesi hiyo wakiwa gerezani, ambazo zilielekezwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) wakati huo (Geofrey Shahidi) bila kufuata utaratibu wa kuzipitisha kwa Mkuu wa Gereza na zikiwa na tarehe zinazopishana.

  Akiongozwa na wakili wake, Jerome Msemwa, Zombe ambaye wakati wa tukio alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Dar es Salaam alidai mbele ya Jaji Salum Massati kuwa anaiomba mahakama imruhusu kutoa tena ushahidi kama ilivyoomba notisi ya wakili wake aliyoitoa Februari mwaka huu ili atoe ufafanuzi ambao hakuutoa wakati akijitetea awali. “Mheshimiwa Jaji naomba shahidi namba moja (Zombe) aje atoe tena ushahidi wake mahakamani hapa na naamini hii ni mahakama ya haki, lazima haki itendeke hivyo nyaraka hizo tulizoelezwa zipo kwa DPP ziletwe sasa hivi maana ofisi yake si mbali ili mteja wangu asikilizwe,” alidai Msemwa.

  Wakati huo Zombe akiwa kizimbani tayari kutoa ushahidi tena, tafrani fupi ilizuka baada ya Zombe kutaka kujitetea mwenyewe kwa kumtaka Jaji asimamie haki itendeke kwa kusema; “Jaji naamini hii ni mahakama ya haki….” Hata hivyo, Jaji Massati alimtaka atulie kwani malumbano baina ya mawakili hayajafikia mwisho hadi kumwezesha shahidi kuingilia kati shauri.

  Aidha, ombi hilo la kurudia utetezi wake, lilipingwa na mawakili wa serikali pamoja na mawakili wengine wa upande wa utetezi akiwamo, Gaudias Ishengoma anayemtetea mshitakiwa wa pili (Christopher Bageni) na Majura Magafu anayewatetea washitakiwa watano katika kesi hiyo kwa madai kuwa endapo barua hizo zitaletwa mahakamani kama kielelezo na Zombe akapewa nafasi ya kujitetea tena, akiwagusa washitakiwa wenzake, mahakama itoe nafasi ya wao kujitetea vilevile.

  “Tunaomba suala hili liangaliwe kwa makini sana, wakati ule mawakili wa serikali walibaini kuwa nyaraka nyingine ni za bandia, tunaomba lisichukuliwe kirahisi, tunaomba maelezo ya kina yatolewe ili lisiathiri mwenendo mzima wa kesi,” alidai Magafu. Jaji Massati alisema atatolea uamuzi suala hilo leo saa nne asubuhi ili kujua kama atatoa utetezi tena au la, na akamruhusu shahidi pekee wa Zombe kutoa ushahidi mahakamani hapo.

  Shahidi huyo, Mkuu wa Gereza la Ukonga, Samwel Nyakitina (59) akitoa ushahidi wake uliolenga kuieleza mahakama anachofahamu kuhusu utaratibu wa wafungwa na mahabusu kutembelewa gerezani au uandikaji wa barua na washitakiwa kumiliki simu na fedha baada ya Zombe katika ushahidi wake wa awali kulalamikia baadhi ya washitakiwa wenzake walikamatwa na simu gerezani na barua na namna ambavyo aliandika barua za malalamiko kwa DPP na Waziri wa Mambo ya Ndani kupitia kwake, shahidi huyo alionyesha kuwa kinyume na matarajio ya Zombe. Sehemu ya mahojiano baina ya shahidi na Wakili Msemwa mbele ya mahakama hiyo yalikuwa kama ifuatavyo.

  Wakili: Shahidi hebu ieleze mahakama utaratibu wa mfungwa au mahabusu kuandika barua na kuipeleka nje ya gereza ukoje.

  Shahidi: Akishaandika barua inapita mapokezi kisha inakwenda ofisi ya Mkuu wa Gereza inagongwa mihuri na saini ndipo inaenda nje, bila hivyo inakuwa si halali na ni ngumu kutumika katika ofisi za serikali…..lakini sasa ni juu ya mwandikaji na mpokeaji huko nje.

  Wakili: Unasema nini kuhusu barua ya Zombe ya Februari 14, 2007 kwenda kwa Jaji Mkuu Mfawidhi na ile ya kutoka kwa Zombe kwenda kwa Waziri wa Mambo ya Ndani akimlalamikia kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka amemtengenezea kesi ya mauaji?

  Shahidi: (akiwa ameshika barua hizo) Saini ni kama yangu na mihuri ya Gereza la Ukonga, lakini sina ukakika nazo mpaka nikaangalie katika makabrasha yangu maana mmenishtukiza sikujiandaa.

  Wakili: Unaiambia nini mahakama kuhusu vielelezo kama simu na fedha ulizowakuta nazo washitakiwa wakati kuwa na hivyo vitu gerezani ni kinyume cha sheria na taratibu za gereza.

  Shahidi: (akatoa vielelezo ambavyo ni simu nne) siku ya tarehe 15/09/2006 siwezi kusema hapa mshitakiwa yupi alikamatwa na simu, labda mpaka nikaangalie katika majalada, lakini siku hiyo askari waliwapekua mahabusu 30 na waliotoka mahakamani na wafungwa zaidi ya 1,000 walioenda kazini kama utaratibu unavyoelekeza na walikutwa na simu nne na fedha taslimu Sh 153,000. Tukio hilo sina kumbukumbu zake zote hapa.

  Awali katika ushahidi wake, mshitakiwa wa 13 ambaye ni wa mwisho katika kesi hiyo inayowakabili washitakiwa tisa hivi sasa, Festus Gwabisabi alidai kuwa alishiriki kuwapekua watuhumiwa waliouawa katika eneo la Sinza Palestina wakiwa hai siku ya tukio bila majibizano yoyote ya risasi na kwamba alishangaa kusikia kupitia vyombo vya habari siku mbili baadaye kuwa wameuawa.

  Akiongozwa na wakili wake Longino Myovela, Gwabisabi alidai akiwa na Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Urafiki, Ahmed Makelle, mshitakiwa wa tatu, alimpekua mtuhumiwa mmoja na kumkuta na bastola moja na mkoba mweusi waliodai una Sh milioni tano na kwa mara ya pili huo mkoba na bastola aliuona mezani kwa Zombe asubuhi ya Januari 15, 2006 walipoitwa kupongezwa kwa kazi nzuri ya kukamata majambazi.

  Alidai pia kuwa Zombe aliwafundisha washitakiwa hao namna ya kujieleza pindi watakapoitwa kuhojiwa katika Tume ya Jaji Kipenka kuhusu tukio hilo kwamba waeleze kulikuwa na majibizano ya risasi katika Ukuta wa Posta, Sinza jambo ambalo yeye (shahidi) alilikataa kwani aliwakamata kwa amani bila majibizano na alishauri wapelekwe kituoni kuhojiwa, lakini hakujua walikopelekwa.

  Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua Sabinus Chigumbi, Ephraim Chigumbi, Matius Lukombe na dereva taksi, Juma Ndugu katika msitu wa Pande, Mbezi Louis, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Januari 14, 2006. Wakati kesi hiyo inaahirishwa Februari mwaka huu, Jaji Massati aliwaachia huru washitakiwa watatu ambao ni Noel Leonard, Moris Nyangelela na Felix Cedrick baada ya kuonekana kuwa hawana kesi ya kujibu kuhusu mauaji hayo.

  SOURCE: Habari Leo
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Kazi ipo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. M

  Msindima JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mmhh,hii kesi huwa siielewi kabisa,huwa najitahidi sana kufatilia lakini napata mashaka kama kuna mtu atahukumiwa naona kama viini macho.
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Watahukumiwa tu, wewe vuta subira. Hukumu ina sehemu mbili, kushinda kesi, ama kushindwa. Hivyo hukumu itatoka, kama una maanisha hukumu kwako ni mpaka mtu aonekane ana makosa, hiyo ni nje ya sheria. Majaji watafuata sheria kuwatia hatiani ama kutowatia.
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa maelezo ya hakimu leo,kupitia radio-one stereo:

  Washtakiwa wooooote wakiongozwa na Zombe mwenyewe wamekutwa na hatia,na watahukumiwa kwa mujibu wa sheria!

  Hakimu ameongea mengi sana,akizungumza ukiukwaji wa maadili ya taaluma kwa maaskari hao.Pia ameelezea namna alivyopitia upande wa ushahidi dhidi yao na kutoa hitimisho WOTE WANA HATIA!na watahukumiwa

  Kesi itaendelea tena kesho,baada ya baraza la wazee kukaa!


  WAKUU,nadhani tupo kwenye episode ya mwisho mwisho,stay tuned!
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  They are reaping what they sow!
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  pamoja na 'kumuondoa' koplo lema bado haijasaidia
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  yah! Zombe's folks walihakikisha Afande Lema anakufa kabla ya kutoa ushahidi wake pia wakawachinyia baharini akina Afande Saad Alawi ili ionekane wamekimbia na kutishwa msala mzima.
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Wanaweza kufungwa maisha?
   
 10. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Mandatory death sentence, kama conviction ni murder.

  Jaji hana discretion hapo. ( Penal Code, 1980, Sect. 197 )
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nimekubali!
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kwa hiyo kesi inaweza kuzaa kesi!
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tatizo ni kuithibitisha hiyo kesi inayozaliwa!
   
 14. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 912
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  Na James Magai

  MAWAKILI wa Serikali katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, mkoani Morogoro na dereva wa teksi wa jijini Dar es Salaam, jana walipigilia msumari wa mwisho katika hoja zao na kuainisha kanuni tatu ambazo mahakama inaweza kuzitumia kuwatia hatiani.


  Sambamba na kanuni hizo, mawakili hao pia walimkemea na kumtaka mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe aache kujifananisha na Yesu Kristo kwa kuwa hastahili kufanya hivyo.


  Mawakili hao, ambao ni waendesha Mashtaka, walitoa msimamo huo walipokuwa wanawasilisha hoja zao za mwisho ambazo zilikuwa zikijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo.


  Zombe, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam ( RCO) na wenzake tisa, wanashtakiwa kwa makosa manne ya kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara hao katika msitu wa Pande ulio nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.


  Katika hoja zao za mwisho, mawakili wa utetezi waliibua changamoto mbalimbali kuhusu ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka wakidai kuwa, umeshindwa kuwahusisha moja kwa moja washtakiwa katika mauaji hayo na kuiomba mahakama iwaachie huru washtakiwa wote.


  Lakini jana mawakili hao wa serikali, waliieleza mahakama jinsi washtakiwa hao walivyofanya mauaji hayo kwa kutumia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi wa upande wa mashtaka.


  Kiongozi wa jopo la mawakili hao, Revocatus Mtaki aliieleza mahakama kuwa kwa mujibu wa sheria, washtakiwa hao wanabanwa kwa kanuni nne kuthibitisha bila shaka kuhusika kwenye mauaji hayo.


  Alizitaja kanuni hizo kuwa: Mtu anayeonekana na mtu kwa mara ya mwisho kabla ya mtu huyo kufikwa na mauti ndiye anayepaswa kueleza mazingira yaliyosababisha kifo cha mtu huyo.


  "Katika kesi hii ni jambo la kushangaza kuwa, marehemu walikamatwa wakiwa hai na kesho yake wakakutwa wamekufa kwa majeraha ya risasi na washtakiwa hawaelezi mazingira ya vifo vyao," alidai Mtaki.


  Katika kuitia nguvu hoja yake Mtaki alirejea kesi moja ambayo mshtakiwa, licha ya kukana kuhusika katika mauaji ya mtu mmoja, hakutaka kueleza ni jinsi gani mtu huyo ambaye kwa mara ya mwisho alikuwa naye, alimtoka na baadaye akakutwa amekufa.


  "Mtukufu Jaji, na hawa washtakiwa hawaelezi ni jinsi gani watu waliowakamata wakawafunga pingu baadaye wakakutwa wamekufa. Hili ni jambo la kushangaza," alisisitiza Mtaki.


  Mtaki aliieleza mahakama kuwa ingawa ni kweli mshtakiwa wa kwanza Zombe alisema hakuwepo katika maeneo yote ya tukio, na kwamba washtakiwa wengine katika maelezo yao wamekana, walikiri kuwepo katika maeneo ya matukio Sinza na ukuta wa Posta, lakini wakakana kwenda Pande bado hawaelezi kuwa walikuwa wapi.


  Aliomba mahakama ione utata wao wa kukana kwenda kwenye eneo la mauaji ambalo ni msitu wa Pande bila kueleza walikuwa wapi kuwa hakutetereshi ushahidi uliotolewa mahakamani na kuiomba mahakama iwatie hatiani wote.


  Kanuni ya pili ambayo Wakili Mtaki aliiomba mahakama iitumie kuwatia hatiani washtakiwa hao, ni ya kuwa na nia moja. Aliieleza mahakama kuwa washtakiwa wote walikuwa na nia ya pamoja dhidi ya marehemu.


  Alisema kuna ushahidi mbalimbali unaowaunganisha washtakiwa hao kuwa walikuwa na nia ya pamoja tangu kuwakamata marehemu, kutokuwapeleka katika kituo chochote cha polisi, kwenda Pande na kwenda kupongezwa kwa kazi hiyo, kutoa taarifa zisizo sahihi kwenye timu za upelelezi za polisi wala kuripoti tukio hilo mahali popote.


  "Hata kwenye Tume ya Jaji Kipenka (Tume ya Rais) ambako walikuwa huru kutoa taarifa sahihi, hawakufanya hivyo," alisema Mtaki.


  Alisisitiza kuwa nia ya pamoja si lazima washtakiwa wawe wamekaa na kupanga njama za kufanya uhalifu, na kwamba mwenendo na matendo yao kabla na hata baada ya tukio unaweza kuthibitisha kanuni hiyo.


  Mtaki aliitaja kanuni nyingine kuwa ni maelezo ya ungamo ambayo mshtakiwa huyo alitoa mbele ya mlinzi wa amani, ambaye ni hakimu wa mahakama ya mwanzo akikiri kosa.


  Mtaki alisema katika maelezo yaliyo mahakamani yamewataja na washtakiwa wengine pia katika kesi hiyo.


  "Kwa hiyo tunaomba mahakama yako tukufu izingatie hizo kanuni na kwa ushahidi wote uliotolewa mahakamani hapa iwaone kuwa washtakiwa wote wana hatia," alisema Mtaki.


  Hata hivyo, Mtaki katika kuhakikisha kuwa washtakiwa wote hawaponi katika ghadhabu ya mkono wa sheria, aliiomba mahakama iwatie hatiani kwa kosa mbadala Zombe na mshtakiwa wa 13, Koplo Festus Gwabisaba, ikiwa mahakama itaridhika kuwa hawahusiki kwa kuwa kwa ushahidi ulioko mahakamani, wao hawakwenda katika eneo la mauaji katika Msitu wa Pande.


  "Kama mahakama itaona kuwa mshtakiwa wa kwanza (Zombe) na wa 13 (Gwabisabi) hawakushiriki katika mauaji kwa kuwa kwa ushahidi ulioko mahakamani hawakwenda Pande, basi iwatie hatiani kwa kosa Accessory after the facts (mshiriki baada ya kosa) chini ya kifungu cha 213,387(i) na 388 cha Penal Code," alidai Mtaki.


  Mtaki aliieleza mahakama kuwa kila kesi huamuliwa kwa mazingira yake na kuitaka mahakama kuzingatia mazingira ya kesi hiyo ambayo alisema kuwa washtakiwa wote ni askari polisi, baadhi yao wakiwa ni maofisa na wapelelezi walio na uzoefu.


  "Kwa hali hiyo shauri hili linapaswa lipewe mtazamo wa kipekee kabisa kwa kuzingatia ushahidi wa pande zote na hatimaye mahakama yako tukufu iweze kufikia uamuzi wa haki ambao sisi tunaamini kuwa washtakiwa wote wana hatia ya mashtaka haya," alisisitiza Mtaki.


  Awali, akianza kutoa hoja zake za mwisho kujibu hoja za mawakili wa utetezi, Mtaki aliieleza mahakama kuwa kwa mujibu wa sheria upande wa mashtaka walikuwa na jukumu la kuthibitisha mambo manne katika kesi hiyo.


  Aliyataja mambo hayo kuwa ni kuthibitisha kuwa marehemu walikufa, kwamba walikufa vifo visivyo vya kawaida, kwamba washtakiwa ndio waliowaua na kwamba washtakiwa hao walikuwa na nia ovu katika kutenda kosa hilo.


  "Mtukufu Jaji, katika kutekeleza jukumu hili tuliita mashahidi 37 na kutoa vielelezo 25 na ni rai yetu kuwa tumelitimiza jukumu hilo mbele ya mahakama hii," alisema Mtaki na kutaja mashahidi waliohusika kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao katika kila kipengele.


  "Tumetoa ushahidi mwingi kuthibitisha marehemu hao wanne walikufa; tumethibitisha kuwa walikufa vifo visivyo vya kawaida kwa kuwa marehemu wote walikutwa wakiwa na majeraha ya risasi shingoni zilizopigwa kutokea nyuma na kutokeza kwa mbele," alidai Mtaki na kuongeza:


  "Hiyo inaonyesha hivyo si vifo vya kawaida wala ajali. Ni rai yetu kuwa ile dhana ya kwamba kulikuwa na mapambano baina ya marehemu na polisi haina nguvu kwa sababu risasi zisingetokea shingoni wote. Parten Shooting ilikuwa Systematic."


  Mtaki aliieleza mahakama jinsi walivyotekeleza jukumu lao kwa kuwaunganisha washtakiwa na mauaji hayo kwa pamoja na kisha kuainisha kila mshtakiwa jinsi alivyohusika akitumia ushahidi mbalimbali uliotolewa mahakamani hapo.


  Katika kuongeza nguvu hoja zake wakati akiithibitishia mahakama jinsi mshtakiwa mmoja mmoja alivyotiwa hatiani na ushahidi bila kuacha mashaka, Mtaki aliiomba mahakama pia izingatie sababu ambazo ilizitumia katika uamuzi wake kuwa washtakiwa hao walikuwa na kesi ya kujibu.


  Akihitimisha ushahidi jinsi unavyomhusisha Zombe na mauaji hayo, Mtaki alimtaka mshtakiwa huyo asijifananishe na Yesu kama ambavyo wakati wa hoja zake za mwisho wakili wake Jerome Msemwa alimfananisha.


  Msemwa katika kuhitimisha hoja zake Mei 7 mwaka huu aliieleza mahakama kuwa mteja wake (Zombe) ni kama Yesu Kristo, kwani ameshtakiwa katika kesi hiyo bila kosa kama Wayahudi walivyomshtaki na kumsulubisha Yesu bila hatia.


  Msemwa aliitahadharisha pia mahakama kutoa hukumu yake kwa haki si kama Pilato alivyomhukumu Yesu hata bila kuwa na hatia na kwamba baada ya kifo chake ndipo Wayahudi hao wakaona kuwa hakika alikuwa ni Mwana wa Mungu na kwamba hakuwa na kosa.


  Akijibu hoja hiyo jana, Mtaki alisema Zombe hastahili kufananishwa na Yesu kwa sababu kwanza, licha ya jaji wa ile kesi ya Yesu alikuwa Pilato ambaye alikuwa katili sana, aliwauliza Wayahudi kuwa walikuwa na ushahidi gani dhidi ya Yesu na hakuna aliyejibu, badala yake wakapiga kelele tu kuwa asulubiwe.


  "Sisi hatukupiga kelele, tumeleta ushahidi kamili hapa mahakamani. Tofauti na Pilato, wewe Mtukufu Jaji ni mtu wa haki unazingatia haki na utatoa uamuzi wa haki. Hivyo kwa mfano huu mshtakiwa wa kwanza asilinganishwe na Yesu," alisema Mtaki.


  Akizungumzia ushahidi wa aliyekuwa mshtakiwa wa 11, marehemu Koplo Rashid Lema ambao ulipingwa na mawakili wa utetezi, Mtaki aliieleza mahakama kuwa ushahidi wake ni halali kutumika mahakamani kwa kuwa wakati maelezo yake yakiwasilishwa mahakamani, alikuwapo.


  "Ingawa maelezo yake yalipingwa na baadhi ya washtakiwa, yeye aliyakubali kuwa ni yake na kwamba ndivyo alivyoyatoa. Hivyo ingawa amekufa, ushahidi wake utaendelea kutumika kwa sababu tayari ulishafanyiwa ‘Cross examination' (mahojiano ya uhakiki) kupitia kwa mashahidi waliouwasilisha," alisema.


  Lema alitoa maelezo hayo kwa hiari kwa Mlinzi wa Amani na maelezo yake ndiyo yaliyoeleza mauaji hayo yalivyofanyika katika Msitu wa Pande. Maelezo hayo ya Koplo Lema yanaungwa mkono na maelezo ya mshtakiwa wa 12, Koplo Rajabu Bakari.


  Baada ya mawakili wa serikali kumaliza kuwasilisha hoja zake kwa kutumia saa 3.10, Jaji Salim Masatti aliahirisha kesi hiyo kwa muda na baadaye kutoa muhtasari wa mwenendo mzima wa kesi kwa wazee wa Baraza ili nao waweze kutoa maoni yao kama washtakiwa wana hatia.


  Akitoa muhtasari huo, Jaji Masatti pia aliwaelekeza wazee hao wa baraza namna ya kutoa maoni yao na kuwataka kutoyumbishwa na mambo yote waliyoyasikia hasa kwenye vyombo vya habari, huku akiwataka wazingatie ushahidi ulioko mahakamani.

  Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo saa 8:00 wakati wazee hao watakapotoa maoni yao na baadaye Jaji Masatti atatangaza siku ya hukumu.


  Zombe na wenzake tisa wanatuhumiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge-Sabinus Chigumbi (maarufu kama Jongo), Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva wa teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam, Juma Ndugu.


  Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni SP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, WP Jane Andrew, Koplo Emmanuel Mabula, Michael Sonza, Ebeneth Saro, Rajab Bakari na Festus Gwabisaba.


  Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya mauaji hayo Januari 14, 2006 katika Msitu wa Pande ulio wilayani Kinondoni, nje ya jiji la Dar es Salaam

  source;mwananchi
   
 15. W

  Wandimazz Member

  #15
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 25
  sasa sijaelewa bado kama hakimu kasema wako guilty hawa wazee wa baraza wao shughuli yao ni nini? hebu tufafanulieni mnaoijua sheria ya nchini kwetu!
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Subiri leo!
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa sijaipata hii ya Zombe kujifananisha ya Yesu..lol. Watu wengine bana yaani badala ya kujitetea kwa hoja zisizo shaka wanaleta makufuru.

  Sasa kwanini uongee crime wakati unaogopa jela?
   
 18. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  substantiate
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Soma post # 10.
   
 20. K

  Kolo New Member

  #20
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wana JK kuna mtu ameuliza namna ya kutoa maji yaliyoingia sikioni wakati wa kuogelea. Simple, tia maji kwenye sikio (yes tia maji) halafu inama upande wa hilo sikio na maji yote yataka. Najua kutakuwa na woga kufanya hivyo lakini trust me, yatatoka kirahiisi kabisa
   
Loading...