MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, imetupilia mbali maombi ya kupinga kusimamishwa kutohudhuria vikao vya bunge wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Esther Bulaya(Bunda).
Sababu kutupwa maombi yao zimetajwa ni kanuni za kudumu za Bunge kupingana na Katiba, jambo ambalo Mahakama hiyo ilisema kesi za kikatiba zina taratibu zake.
Kesi hiyo ilisikilizwa jana mahakamani hapo na Jaji Hamisa Kalombola huku kina Mdee na Bulaya wakiwakilishwa na wakili wao, Fredy Kalonga na upande wa serikali ukiwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Angaza Mwipopo.
Pamoja na kutupiliwa mbali maombi hayo, Jaji Kalombola alisema Mahakama hiyo ina uwezo wa kuhoji kinachofanyika bungeni.
Kwa upande wa Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, ambaye aliweka kusudio la kufungua kesi ya kudhalilishwa na askari wa Bunge, Mahakama hiyo haijamruhusu kufungua kesi kwa maelezo kuwa hajafuata taratibu za ndani za Bunge za kupinga maamuzi yaliyotolewa na Spika Job Ndugai.
Mahakama hiyo pia ilisema kiapo cha mwombaji kilikuwa na mapungufu kwa kuunganisha hoja za kisheria na kuongelea mwenendo wa Bunge bila kufuata taratibu za Bunge jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Kinga, Maadili na Mamlaka ya Bunge kifungu namba 21.
Juni 5, mwaka huu Bunge liliazimia kuwafungia kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge Mdee na Bulaya kwa kudharau Mamlaka ya Spika.
Kwa upande wake, Mnyika akipewa adhabu na Spika Ndugai ya kutohudhuria kwa siku saba kwa kosa la kufanya fujo bungeni.
Tujikumbushe alichokisema Tundu Lissu kabla hajapeleka kesi mahakamani.