Kesi ya Uhalali wa Muungano kuhamia The Hague

Nje ya muungano hakuna Zanzibar bali kuna Unguja na Pemba kama nchi mbili tofauti. Najua issue kubwa inayowasumbua ni kutaka kuifanya zanzibar kuwa nchi ya ki-islam na kupata misaada toka kwa nchi za Ki-islam. Lakini hilo halitowezekana angalau kwa sasa.

Punguza chuki
 
Hata Ingeenda The Uji,

Wale ni Wadogo Zetu tu lazima tuwaangalie kwa Ukaribu wazazi Wao na wetu walituachia maagizo ya kuwaangalia
 
La ajabu lipi hapo?. Nyerere alitaka Biafra ijitenge na Nigeria unaona ajabu Zanzibar kujitenga na Tanganyika?. Sudani ni nchi moja na imejitenga na sasa kuna Sudan mbili. Acheni Zanzibar ijitenge maana Tanganyika imejigeuza KOLONI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano wetu adhimu, Tanzania ni nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu ni union, nchi mbili zimekuwa fused together hizo nchi zikafa na kuunda nchi moja mpya ya JMT. Muungano wetu ni muungano wa aina yake kama chemical process ya two compounds zina undergoes chemical reactions to form a new product ambapo huwezi tena kuzirudisha kwenye ile hali yake ya awali, hata kwenye Articles of the Union, kuna provisions za kuungana tuu, hakuna provisions zozote za kuuvunja muungano, muungano wetu adhimu ni muungano wa milele, mawazo, maneno au matendo yoyote ya kuvunja muungano ni uhaini.

Hakuna Taasisi yoyote duniani sio UN wala mabeberu wowote wanaoweza kuingilia mambo ya ndani ya JMT kwasababu kimataifa Tanzania ni nchi moja tuu ya JMT.
P

Ili kuwa nchi moja kuna taratibu zake za kisheria kimataifa na taratibu hizo hazikufuatwa kama vile suala la mafuta na gas lilivyo ingizwa kwenye katiba yenu bila ya ridhaa ya wazanzibari.

Nchi moja lakini ujue kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar tunaweza kuitisha kura ya maoni juu ya suala la muungano.

Mtawala siku zote ataupamba tu huu muungano kwa majina mazuri mazuri, mmoja ni wewe, ila utambue lililo mwanzo lina mwisho, hata sudani ilikuwa moja
 
Yaani wanzanzibari wananishangaza deputy president wao ameshazema wanufaika wa muungano lkn wao hawakubaliani nao

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata magufuli anasema nchi tajiri lakini wewe masikini, nchi ina Deni, wanafunzi zaidi ya 10,000 walio maliza darasa la saba hawana pa kwenda, hospital unalipia matibabu, sasa huo utajiri upo wapi ? Wakati unalala na njaa?
 
Nani kakwambia ICJ inapokea malalamiko/kesi kutoka kwa watu binafsi?

ICJ inavyofanya kazi , Kesi labda zipelekwe na nchi au UN general Assembly kwaajili ushauri wa kisheria.

Nyie endeleeni kunywa urojo tuu na kudanganyana kwenye vijiwe vya gahawa huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili kuwa nchi moja kuna taratibu zake za kisheria kimataifa na taratibu hizo hazikufuatwa kama vile suala la mafuta na gas lilivyo ingizwa kwenye katiba yenu bila ya ridhaa ya wazanzibari.
Mkuu Ghibuu ni kweli kwenye muungano wetu kuna vitu havikufanyika ikiwemo kuipata ridhaa ya Wanzanzibari hivyo Zanzibar hawaku ratify muungano.

Vipengele vya kisheria vinapokosekana mkataba unaweza kuwa ni batili, au batilifu. Kitendo cha Zanzibar kuto ratify muungano lakini kikautekeleza then kunauhakalisha.

Ni kama ndoa hufungwa kwa ridhaa, ukimbaka mwanamke ni kosa la jinai, ili liwe kosa, anayebakwa lazima apige kelele, a resist na akiishabakwa lazima ashitaki.

Mwanamke akibakwa, na baada ya kubakwa hajashitaki popote, na kuendelea kuishi na yule mbakaji, na kumpatia huduma zote zikiwemo huduma za mke, mwanamke huyo atahesabika ameridhia, na uhusiano wa wawili hao utahesabika ni ndoa halali.

Japo Zanzibar haikuridhia muungano lakini ikatekeleza vipengele vyote vya muungano, utekelezaji huo unahesabika ndiko kuridhia kwenyewe.

P
 
Sina idadi Ila hata kama ni wengi naamini utaratibu wao wa kuwepo hapa ni tofauti na wenzetu wa hapo visiwani. Wanzanibari hawaitaji formalities za kimipaka kuishi Bara, ni kama wachaga walivyojazana Dar. Leo hii dar ikawaamuru wote warudi kwao ardhi yao naamini inaweza isitoshe sababu ya kuzaliana.
Wao kwani hawawezi kufata hizo formalities.
 
Nchi moja lakini ujue kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar tunaweza kuitisha kura ya maoni juu ya suala la muungano.
It's true kwa mujibu wa mabadiliko batili ya katiba ya Zanzibar ya 1984 yaliyofanywa 2010, Zanzibar inaweza kuitisha kura ya maoni juu ya muungano.
Na hili nimelizungumza hapa

Kitu ambacho Wazanzibari hamjajua, mabadiliko hayo kwenye katiba yetu ya JMT, hatuyatambui!. Hata GNU katiba yetu haitambui, na mabadiliko yote mliyoyafanya ile 2010 ni mabadiliko batili, katiba ya JMT haiyatambui na mengine ni kinyume cha katiba mama ya JMT.

Mfano katiba ya Zanzibar inaitambua Zanzibar kama nchi na kuielezea ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT.

Katika ya JMT inasema JMT ni nchi moja tuu ya JMT na Zanzibar ni sehemu ya JMT.

Katiba ya Zanzibar, rais wa Zanzibar anatambulika kama rais wa nchi ya Zanzibar na amiri jeshi wa KMKM, JKU, Vikosi Maalum

Katiba ya JMT inatamka Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye rais mmoja na Amiri jeshi Mkuu, rais wa Zanzibar ndani ya katiba ya JMT ni nobody, KMKM, JKU na Vikosi Maalum havitambuliwi kama majeshi ni migambo!.

Katiba ya Zanzibar imeonyesha nchi ya Zanzibar ina eneo lake na ina mipaka yake, na Rais wa Zanzibar ana mamlaka ya kugawa mikoa ya Zanzibar.

Katika ya JMT inasema Tanzania ni nchi moja na eneo la JMT ni eneo lote lilikokuwa eneo la Tanganyika na eneo lote la iliyokuwa PRZ hivyo kwa mujibu wa katiba ya JMT, Zanzibar sio nchi, Zanzibar haina eneo, rais wa Zanzibar hana mamlaka ya kugawa eneo lolote la JMT.

Hivyo hata Zanzibar ikipiga kura ya maoni kujitoa muungano, kura hiyo haitambuliwi huku bara, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar bali kuna sehemu inayoitwa Zanzibar ambayo ni sehemu ya JMT, kitendo chochote cha kuimega sehemu yoyote ya JMT ni uhaini.

Articles of the Union hazina any provisions za kuuvunja muungano, hivyo muungano wetu ni wa milele regardless Zanzibar wanautaka au hawautaki upo na utalindwa kwa gharama yoyote!.
P
 
Mkuu Ghibuu ni kweli kwenye muungano wetu kuna vitu havikufanyika ikiwemo kuipata ridhaa ya Wanzanzibari hivyo Zanzibar hawaku ratify muungano.

Vipengele vya kisheria vinapokosekana mkataba unaweza kuwa ni batili, au batilifu. Kitendo cha Zanzibar kuto ratify muungano lakini kikautekeleza then kunauhakalisha.

Ni kama ndoa hufungwa kwa ridhaa, ukimbaka mwanamke ni kosa la jinai, ili liwe kosa, anayebakwa lazima apige kelele, a resist na akiishabakwa lazima ashitaki.

Mwanamke akibakwa, na baada ya kubakwa hajashitaki popote, na kuendelea kuishi na yule mbakaji, na kumpatia huduma zote zikiwemo huduma za mke, mwanamke huyo atahesabika ameridhia, na uhusiano wa wawili hao utahesabika ni ndoa halali.

Japo Zanzibar haikuridhia muungano lakini ikatekeleza vipengele vyote vya muungano, utekelezaji huo unahesabika ndiko kuridhia kwenyewe.

P
Suala lipo palepale sisi watanganyika tuwape nchi yao wazanzibar hivi hukuona aibu kwenye SADC,na hukuona aibu kwenye mashindano ya Mpira wa CECAFA,wazanzibar waliimba wimbo wao wataifa na wana bendera yao ya taifa,Mimi sioni tatizo wazanzibar wakipewa nchi yao wajitawale,Sudani sasa zipo mbili.
Hong Kong nako hali tete wanataka kujitenga na uchina,why hatupendi kuitwa watanganyika ilhali ndo jina letu kamili na why neno Zanzibar halijafutika?
Hakuna nchi duniani ya maaajabu eti wameungana wakawa marais wawili bunge mbili n.k.

Nakazia kwanini sisi tunawahitaji sana wazanzibar kuna kitu gani kimejificha juu ya huu Muungano?
Why wao wanaukataaMuungano ila sisi tunang'ang'ania tuwe nao?
Na why ukiongelea suala la Muungano unawekwa jela rejea MASHEIKH WA UAMSHO.
 
Back
Top Bottom