Kesi ya Uhaini Kipindi Cha Utawala wa Mwalimu Nyerere!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Uhaini Kipindi Cha Utawala wa Mwalimu Nyerere!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rich Dad, Jan 13, 2011.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  WanaJF Habari Zenu!!!
  Natumai mko poa na michakato ya kila siku ya ukombozi wa taifa letu.

  Kuna kitabu kimoja niliwani soma miaka ya nyuma, kitabu kinachozungumzia kesi ya uhaini iliyokuwa inawakabili jamaa waliotaka kuipindua serikali ya Mwalimu. Kwa kumbukumbu zangu walioshiriki kula njama ni pamoja na baadhi ya vikosi vya jeshi, uncle Tom, Ghulam, Mc Ghee, Mkuu wa Mkoa wa Arusha kipindi hicho kama sikosei alikuwa anaitwa Kapteni Temba ( Naruhusu kusahihishwa), akina bibi Titi Mohamedi n.k.
  Katika kitabu hicho Kulikuwa kuna manowari ya kivita iliyokuwa ije taratibu ikitokea Uingereza kupitia Zanzibar. Na mwalimu ilikuwa auwawe siku aliyokuwa anakwenda kanisani kusali (Msasani).
  Katika mfululizo wa kesi kuna baadhi ya mashahidi hawakutajwa kwa majina yao, na badala yake walitajwa kwa herufi X, Y, Z.

  Kitabu hicho nasikia kimepigwa marufuku kusomwa. Naomba mwenye kujua nitapata wapi copy yake anisaidie kwa kunielekeza na nitakitafuta. Na pia mwenye kujua story nzima ya jaribio aiweke hapa ili tukumbuke tulikotoka na changamoto zake.

  Asanteni!
   
 2. L

  Lwama Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe ni Usalama wa Taifa nini???
   
 3. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama ukikosa kitabu wasiliana na Wahariri/wamiliki wa gazeti la kiingereza (nadhani Sunday Observer) la kila Jumapili la makampuni ya IPP.
  Mwaka 2008 walikuwa wakitoa maelezo ya kesi hiyo kila wiki.
   
 4. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapana mimi si usalama wa Taifa, ila napenda kujua sababu iliyopelekea serikali ya Nyerere kutaka kupinduliwa. Afu katika kitabu hicho nakumbuka aliyefichua siri alikuwa Dereva Taxi aliyekuwa anawachukua washiriki kutoka sehemu moja kwenda ingine. Na kama jamaa walikuwa wanabadili madereva Taxi kila wakati huenda watanzania tungekuwa na historia nyingine leo hii.
   
 5. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asante Kishongo nitafuatilia, nadhani ni watanzania wachache sana wanaoifahamu hii kesi.
   
 6. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  niliwaikusoma mtiririko wa hii story katika gazeti la rai wakati linamilikiwa na Ulimwengu. aliyekuwa msimulizi likuwa jamaa anaitwa maganga kama sikosei. ukikipata hicho kitabu tujulishane. Na hapa JF ipothread ya tukio zima
   
 7. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu Ngoja ni search may be nitabahatika kuiona. Nikipata hicho kitabu nitaku pm
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Poa bwana, chimbua unufaike!
   
 9. m

  mzambia JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kama kuna mtu anayo aweke haraka humu jamvini.
   
 10. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Kanunue usome kitabu hiki cha: Godfrey Mwakikagile, "NYERERE AND AFRICA: END OF AN ERA: EXPANDED EDITION" (Atlanta, Georgia: Protea Publishing Co., 2004).

  Chapter 13 ya kitabu hiki utapata mambo mengi juu ya njama, ikiwemo stori ya mwanae Nyerere aliyekuwa Kapteni wa JWTZ Andrew Nyerere, ila kujua changamoto za uongozi za ndani ya nchi na nje ya nchi na mataifa beberu yanavyotaka kuburuza nchi ndogo, nakushauri ukisome kitabu chapter zote kuanzia ya mwamzo mpaka mwisho.

  Ili upate nini nasema kuhusu kitabu hiki tembelea wenusaiti hii: Julius Nyerere - SouthAfrica.com Discussion Forum
   
 11. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
 12. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu! ngoja niperuz kwanza!
   
 13. A

  AeIoU Member

  #13
  Feb 27, 2015
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Due hii kali
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Feb 27, 2015
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hapo kuna kesi mbili, ya kwanza ya miaka ya 70 na nyingine ya miaka ya 80
   
 15. Idd Ninga

  Idd Ninga JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2015
  Joined: Nov 18, 2012
  Messages: 1,982
  Likes Received: 557
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii.
  Vizuri tuwekewe mkasa mzima katika Jf ili tufahamu kilichotokea.
  TAZAMA HAPA KIDOGO.
  http://www.globalpublishers.info/m/blogpost?id=5398006%3ABlogPost%3A2701593
  PITIA NA HAPA TENA
  http://www.google.com/xhtml?q=Kesi%20ya%20uhaini%20tanzania&client=ms-opera_mb_no&channel=bh
   
 16. Sumve 2015

  Sumve 2015 JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2015
  Joined: Jun 16, 2013
  Messages: 2,215
  Likes Received: 918
  Trophy Points: 280
 17. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2015
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Ukifatilia jaribio lile la miaka ya awali ya 80 (ambayo wengi tulikuwapo hata kama tukiwa mashuleni) kuna kitu kimoja waweza kugundua ambacho ni muhimu sana kwa siasa na hali ya nchi kwa sasa.
  Kikundi kile ambacho kimsingi kilikuwa cha vijana maafisa wa Jeshi na wanasiasa wachache kilikuwa kinaongozwa na Mfanyabiashara Uncle Tom ( nick name) kama mfadhili wa kifedha. Na madhumuni yao makubwa ilikuwa ni kuondoa utawala wa Nyerere madarakani kwa kupingana nae kuhusu sera zake. Hapa ieleweke kuwa walipingana nae kuhusu sera tuu na sio kuwa walichukizwa na WIZI,UFISADI NA DHULUMA ambazo kwamba pengine zilikuwepo hapana, hayo hayakutajwa hata wakati wa kesi yao.
  Wakati wa jaribio lile Tanzania ilikuwa ni nchi moja kabisa kwa maana Serikali na wananchi na hata vyombo vya ulinzi na usalama kwa pamoja walikuwa na ushirikiano wa kina kabisa. Hakukuwa na viongozi waliojilimbikizia mali kwa njia ya kuwaibia wananchi,askari na maafisa wa usalama walikuwa rafiki wa raia na hakukua na chuki yeyote kati yao.
  Hali hiyo ilifanya jaribio lolote la kuiondoa serikali madarakani lilionekana haramu mbele ya wananchi na walikuwa wanatoa habari zozote za kutilia mashaka mienendo yeyote isiyokuwa ya kawaida waliyoona. Ndio maana hata wakati wa kesi tuliona wapo madereva wa Tax walitoa ushahidi kuwa wao ndio walipeleka taarifa za kutowaelewa vizuri wateja wao na taarifa hizo zilikuwa za msaada mkubwa katika kufichua njama hizo.
  Nimesema hapo awali kuwa tunacha kujifunza hapo. Jee sasa hivi serikali na raia wake wako katika hali ya urafiki wa kweli na usio na mashaka kama wakati ule? Jee wasio iunga mkono serikali kwa wakati huu nao ni kuwa wanapingana nayo kwa ktofautiana sera tuu au wanapingana nayo kwa mambo mengine kama UFISADI,WIZI, NA DHULUMA? Maana mara nyingi kutofautiana kisera mara nyingi hayo ni mambo ya kisiasa zaidi na wananchi wa kawaida kwao huwa hawajengi chuki na watawala ila wanaona ni kama kuchagua kupenda taarabu au Rumba tuu.
  Siombi litokee ila ni vema kujiweka on alert, tupo vizuri kiasi kwamba njama kama zile zikijitokeza wananchi wanaweza kuisaidia serikali kwa kuipasha habari zinazoendelea kama ilivyokuwa miaka ile ambayo kila mwananchi alikuwa mlinzi wa taifa lake? Uzalendo ule bado upo? Na kama haupo nini kimepelekea kuwa hivyo? Kama ni chuki kwa sababu viongozi wameamua kuwa mafisadi na kudhulumu wananchi tunafanya nini kuondoa hali hiyo ili taifa lirudi kwenye umoja wake?
  Ukienda nchi zenye maendeleo, hutakuta uadui wa ndani bali ni mashindano ya kutangaza sera tuu hayo mengine yanachukuliwa kuwa ni makosa ya jinai bila kujali itikadi na wahusika wanahukumiwa. Hapa kwetu mtu anatenda kosa la jinai kabisa lakini kwa vile ni "mwenzetu" basi anatetewa kwa nguvu zote na chama chake na mwishoe watu walioona kosa lile wanaligeuza kuwa la serikali au chama na kuongeza chuki.
  Napata mashaka kuwa njama kama zile zikijitokeza sasa hivi na kwa mgawanyiko tulio nao iwapo tutabaki salama. Serikali ili iwe ya wananchi kutoka moyoni isisite kuchukua hatua za wazi na kulingana na sheria kwa viongozi wake wanao jihusisha na maovu, hii tabia ya kuwalinda ndio inayowapa kiburi hata wakiiba wanasema " hivyo ni vjisenti tuu" katika nchi yenye masikini wanaopata mlo mmoja kwa kubahatisha. Ona wengine nao wamekuja na dharau eti "Milioni 10 hela gani? Hizo ni za mboga tuu" tena hayo yanasemwa sio chumbani kwake bali mbele ya tume ya maadili na media zote. Ni kama anawaambia wananchi ujumbe huo.
   
Loading...