Kesi ya Ugaidi wa Mbowe Jumuiya ya Kimataifa, Mabalozi, EU na UN wadaiwa kumaliza kazi iliyokuwa inawapeleka Mahakamani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,377
217,438
Nilifanikiwa_kuwasiliana_na_mabalozi_na_maafisa_wa_balozi_mbalimbali_ambao_walikuwa_wanahudhur...jpg

Hii ndiyo Taarifa inayozagaa chini kwa chini, kwamba Jumuiya ya Kimataifa imemaliza ngwe yake kwenye kesi ya Ugaidi wa gharama nzito yenye kufikia kitita cha Tsh laki 6 inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu , na kugundua kwamba kesi hiyo ni ya kupikwa na ya uongo.

Taarifa zinaeleza kwamba Jumuiya hiyo ya Kimataifa imependekeza kwa serikali ya Tanzania kufuta kesi hiyo ya uongo haraka iwezekanavyo ili kuepusha uonevu usio na Tija yoyote kwa yeyote

Kuanzia sasa ni kwa uchache sana tutawaona wazungu hawa Mahakamani kwa vile shughuli walioifuata wamemaliza .

He_is_not_a_terrorist_mzee_Mbowe....jpg
 
Kuna wakati mkuu huwa naona aina yako ya kufikiri haina tofauti na wale vijana wa CCM. Unapata faida gani kweka unfounded information like this!?

Tofauti yenu ni platforms tu mnazotumia kuonesha umaamuma wenu. Jitofautishe na mazezeta walioko UVCCM kwa kuweka taarifa ambazo zinaonesha mental maturity badala ya ushabiki kama huu
 
UGAIDI haupimwi na kiwango cha fedha au utajiri wa mtu/watu.

Ugaidi ni Dhamira na Matendo maovu ya kihalifu ambayo yanaweza kufanywa na mtu yeyote yule masikini au tajiri, mwanasiasa au mfanyabiashara, mwenye dini au asiye na dini.

Vyombo vyetu vipo huru kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, haviwezi kushinikizwa wala kuingiliwa na EU, UN wala kuguni.

kama wafuasi wa Mbowe walidhani vyombo vya kusimamia haki vitatishwa na wazungu basi hapo wamekosea sana, tena wamevikosea heshima vyombo vya sheria kwa kuwatishia wazungu, yaani karne hii unamtishia mtu mwenye akili zake eti Mzungu!

Pambaneni huko mahakamani acheni kuruka ruka
 
UGAIDI haupimwi na kiwango cha fedha au utajiri wa mtu/watu.
Ugaidi ni Dhamira na Matendo maovu ya kihalifu ambayo yanaweza kufanywa na mtu yeyote yule masikini au tajiri, mwanasiasa au mfanyabiashara, mwenye dini au asiye na dini....
Vyombo vya kuviamini ni hivi vya akina kingai na Mahita ?
 
Namshambulia mleta mada kwa sababu hana ushahidi/uhakika na habari yake yaani ni amesikia sikia tu za chini chini basi karuka nayo.. Kwa kifupi mleta mada ni mkurupukaji.
Watu makini hushambulia mada badala ya mwandishi , tena mwenye ID fake
 
naona nchi inaigiza maswala ya ugaidi hewa, siku ugaidi wenyewe ukiwadia ndio tutajua tulikua tunaigiza movie ya vita kwa kutumia bunduki halisi.

Madam President na Government kwa ujumla, mambo ya ugaidi ni mazito tuache kuyafanyia drama.

wenzetu wa DRC ,Nigeria Somalia, Central Africa nk wanalia na ugaidi kila siku na hawajui lini utaisha nchini mwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1956343

Hii ndiyo Taarifa inayozagaa chini kwa chini , kwamba Jumuiya ya Kimataifa imemaliza ngwe yake kwenye kesi ya Ugaidi wa gharama nzito yenye kufikia kitita cha Tsh laki 6 inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu , na kugundua kwamba kesi hiyo ni ya kupikwa na ya uongo .

Taarifa zinaeleza kwamba Jumuiya hiyo ya Kimataifa imependekeza kwa serikali ya Tanzania kufuta kesi hiyo ya uongo haraka iwezekanavyo ili kuepusha uonevu usio na Tija yoyote kwa yeyote

Kuanzia sasa ni kwa uchache sana tutawaona wazungu hawa Mahakamani kwa vile shughuli walioifuata wamemaliza .

View attachment 1956344
Magufuli aunganishwe kwenye kesi. Inakuaje anaandamana na gaidi?
 
Back
Top Bottom