Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Tuhuma za askari polisi kutesa na kupiga watuhumiwa zimekithiri hapa Tanzania. Iwe ni kwa kesi ndogo hadi kubwa linapokuja suala la kuandika maelezo ya onyo ili yatumike mahakamani, watuhumiwa wanalalamika kupigwa na kuteswa. Na baadhi yao wamepata ulemavu na hata kupoteza maisha.
Kesi ya ugaidi inayomkabili Mbowe inaendelea. Lakini watuhumiwa wenzake na Mbowe wanalalamika kupigwa na kupata mateso makubwa. Hii ni kinyume na katiba ya JMT na hata sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 57. Ambacho kinataka maelezo ya polisi yachukuliwe kwa hiari bila shuruti.
Ni aibu kuwa na taifa linalojinasibu kuwa ba bill of rights kwenye katiba yake alafu bado haki za binadamu zinavunjwa.
Hivyo ni bora kuwa na video Camera kila kituo cha polisi ili kurekodi maelezo ya watuhumiwa ili kusudi kusiwepo na habari za kutesana kama vile sio binadamu.