Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe kuendeshwa kwa njia ya Mtandao ni uoga wa Mamlaka dhidi ya nguvu ya umma na Jumuiya ya Kimataifa

Kwani nani kakwambia mbowe hafikishwi mahakamani. Kama unafikiri kuna mtu anamuogopa au anasingiziwa unajifurahisha tu. Naamini atafikishwa kujibu mashitaka na kesi itaamua kama ana makosa au hana makosa.
Uko nyuma sana ya muda
 
Sasa kwanini mnasumbua wauza magazeti kubeba mabango msikae kwa kutulia kusubiri waoga wafute kesi?

Kama ccm sio waoga wasiwabebeshe mzigo polisi wenye silaha kupambana na watu wasio na silaha, wajitokeze wenyewe wakabiliane na raia wenzao wasio na silaha kisha uje ulete mrejesho.
 
Nguvu ya umma maana yake sio kumtoa, bali ni ngumu sana kuendesha mashitaka ya uongo mbele ya watu wengi.
Hivi ndio mnaambiwa mkikaa kwenye hayo makongamano? Au hizi ni akili zako tu binafsi?
 
Naunga Hoja mkono. Hili suala la kuunganisha au kufuta nyuzi litazamwe upya na JF
 
Chadema wangetoka huku mitandaoni wakaungana kiukweli kutetea hicho wanachokiita haki ingewasaidia sana

Usaliti usalitini

Cdm wote wanakaa hapa Dar? Ni tukio gani linaweza kuhudhuriwa na watu wote?
 
Jana niliweka uzi humu kuhusu taarifa nilizopata kutoka ndani mwao kabisa kwamba Mbowe hatofikishwa Mahakamani kwa visingizio mbalimbali , Mtukufu Moderator akaiunganisha kusikofahamika , sasa leo Mbowe hajafikishwa kisutu kwa kisingizio duni cha Corona huku kesi zingine zikiendelea bila kujali corona .

Ukweli ni kwamba Mbowe hakufikishwa Mahakamani ili kukwepa nguvu ya umma na jumuiya za kimataifa , hasa baada ya kuonekana dhahiri kwamba Mashitaka dhidi ya Mbowe ni ya uongo .

Natoa wito kwa JF kuwa waangalifu wanapofuta nyuzi ama kuziunganisha , tuaminiane japo kidogo

View attachment 1880613View attachment 1880614
Pamoja na vitisho vyote tumefika kisutu
 
Kama ccm sio waoga wasiwabebeshe mzigo polisi wenye silaha kupambana na watu wasio na silaha, wajitokeze wenyewe wakabiliane na raia wenzao wasio na silaha kisha uje ulete mrejesho.
Halafu akili hizi hizi ndio unataka kuzitumia kusema kuwa Mbowe sio gaidi? Hakuna mwana CCM anataka kukabiliana na wahalifu, hiyo ni kazi ya polisi.
 
Cdm wote wanakaa hapa Dar? Ni tukio gani linaweza kuhudhuriwa na watu wote?

Walioko dar ni wangapi na wamefanya nini? Kwani wa mikoani wangeshindwa nini kufanya wanachokiamini katika maeneo yao?

Tukiwaambia chadema ni chama cha watu wachache sana tena wa twita hamsikii wacha mjionee
 
Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa bunge maalum la katiba na makamu wa rais wa JMT vs mwenyekiti wa chama ambacho kina mbunge mmoja bungeni
Kwa ule uchaguzi uliosimamiwa na yule dhalimu aliyeko motoni, hata mbunge mmoja ni ajabu kuwa naye.
 
Walioko dar ni wangapi na wamefanya nini? Kwani wa mikoani wangeshindwa nini kufanya wanachokiamini katika maeneo yao?

Tukiwaambia chadema ni chama cha watu wachache sana tena wa twita hamsikii wacha mjionee

Sijui hata unaoongea utoto gani, ni tukio gani linahudhuriwa na watu wote?
 
Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa bunge maalum la katiba na makamu wa rais wa JMT vs mwenyekiti wa chama ambacho kina mbunge mmoja bungeni
Hivi unamfahamu Bilionea Mbowe wewe ? hapa huyu mama alikuwa mpokea wageni tu , wakati huu Mbowe akitafuta muafaka wa kitaifa

Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram:_“Mwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana_na_Waziri...jpg
 
Sasa kwanini mnasumbua wauza magazeti kubeba mabango msikae kwa kutulia kusubiri waoga wafute kesi?
Muuza magazeti anategemea hayo mabango yenye ujumbe ili kesho auze magazeti.win win Hali ya hewa
 
Back
Top Bottom