KESI ya Ubunge Ubungo, Hawa Ng'humbi atia mpira kwapani, Mnyika; kazi inaendelea







Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika.


Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili ya uchaguzi wa jimbo hilo wa mwaka 2010, baada ya Mahakama kutupilia mbali mashitaka yote matano yaliyokuwa yakimkabili ambayo ni :

1)Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
2)Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3)Kuingia watu wengi wa CHADEMA ktk chumba cha kuhesabia kura
4)Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5)Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)

Mlalamikaji Hawa Nghumbi (CCM) anatakiwa kulipa gharama zote za kesi hiyo kama ilivyoamriwa na Mahakama.






 
Oh Ndio Maana NAPE NNAUYE anakuwa kichaa kumzungumzia JOHN MNYIKA...

POLE KIJANA KATIBU MWENEZI wa CCM... Na BADO subiri asubuhi ya 2015... CCM Nje

Sijali CHAMA CHOCHOTE KITAKACHOCHUKUA DOLA...
 

Hapo kwenye bold hilo ndio jina halisi la Dr.Kigwangalah mbuge wa Nzega au umekosea mdau?

Yaap ndiyo jina lake halisi;Nina uhakika wa asilimia zote mkuu Kijereshi!Alishindwa hapa kujitetea vyema ni vipi basi yy mwenye wazazi wote waislam awe na jina la kiroma!
 
mnyika.jpg

Kwa mara nyingine Hawa Ngh'umbi ambebwaga manyanga kiasi cha kuondoa shauri lake mahakani. Sijui Nape atalielezeaje hili nalo. Maana anajifanya anazijua sheria wakati hajui kitu.
 
Nape anachofanya kisa siku asikike
Kwenye media hata kama yupo wrong,
Tatizo anajifanya anajua kila kitu wakati hata ilani yao kashindwa kuielezea hapa jamvini sembuse sheria.
 
Nape ni Kilaza tu, hana ubavu wa kusimama na JJ Mnyika in any ground. Mnyika amepigania maisha yake bila kubebwa na mgongo wa mtu yoyote hadi kuwa mwanasiasa anayeheshimika, licha ya kuwa ni proven genius wakati anasoma. Nape aliyepata DIVISION ZERO form six amekuwa akitembelea nyota ya baba yake na ndio maana anajiita Nnauye Jr badala ya Nape ili kusafiria nyota ya mzee.

Kwa kuwa CCM haina mfumo wa kulea na kukuza viongozi wa baadaye wanaishia kuokoteza vijana wa hovyo hovyo kama Nape kisa tu wanatumika kirahisi kwenye siasa za makundi, lakini hawana tija yoyote kwenye maendeleo ya nchi yetu. CCM ni janga la kidunia kwa kweli, inatia aibu kuwa tutaendelea kuongozwa na hiki chama chenye viongozi kama Nape na JK kwa miaka mi3 mingine...
 
Hii ni habari mbaya sana kwa Nape na CCM kwa ujumla.

CCM wana wivu na uchungu sana kuona majimbo muhimu ya Dar (Ubungo na Kawe) kuwa chini ya CHADEMA, hivyo hivyo kwa Arusha(Arusha mjini na Arumeru Mashariki), Kilimanjaro(Moshi mjini, Hai, Rombo), Mwanza(Ilemela na Nyamagana), Mbeya(Mbeya mjini na Mbozi magharibi), Iringa mjini.

Kila kada mwandamizi wa CCM anajua siku za kukaa madarakani kwa CCM zinahesabika kabisa.
 
Kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kusalimu amri kwa aliyekuwa mgombea wa NYINYIEMU ktk nafasi ya ubunge kupitia jimbo la ubungo amekubali yaishe na kuondoa pingamizi lake katika mahama ya rufani jijini dar. Hata hivyo mgombea huyo ameomba asidadawe gharama za kesi na mpinzani wake kitu ambacho hakijakubaliwa na atapaswa kulipa gharama zote zilizojitokeza wakati wa rufani hiyo ikiwa inaendelea.
 
Kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kusalimu amri kwa aliyekuwa mgombea wa NYINYIEMU ktk nafasi ya ubunge kupitia jimbo la ubungo amekubali yaishe na kuondoa pingamizi lake katika mahama ya rufani jijini dar. Hata hivyo mgombea huyo ameomba asidadawe gharama za kesi na mpinzani wake kitu ambacho hakijakubaliwa na atapaswa kulipa gharama zote zilizojitokeza wakati wa rufani hiyo ikiwa inaendelea.

Nape Nnauye and others DO NOT like this !!! Men !!!
 
ccm kwa sasa sera hawana na uonga ndio unawaingia na kuwanyemelea kila kukicha kuelekea 2015 yaani mtawaona wengi wanalia mbele ya wapiga kura, pengune hata kupiga magoti maana mwelekeo sio wanahofu kubwa sana
 
Back
Top Bottom