KESI ya Ubunge Ubungo, Hawa Ng'humbi atia mpira kwapani, Mnyika; kazi inaendelea


Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
2,619
Points
1,500
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined Jan 6, 2012
2,619 1,500
Hawa Ng'humbi kupitia kwa wakili wake ameomba rufaa iondolewe mahakamani bila gharama.

Ilikuwa ni baada ya maombi aliyotoa mapema kwa Wakili wa mujibu rufani, kwamba aruhuhusiwe kuchomoa na asamehewe gharama za kesi hatua ya rufaa.
 
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
7,053
Points
1,225
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
7,053 1,225
Hata mimi nilitaka kuuliza kuhusu hili humu maana kimya kimezidi. Je hakuna makamanda wa kuripoti huko? Tusubiri live coverage kama ilivyokuwa kwa Lema.
 
T

Twino

Member
Joined
Mar 22, 2012
Messages
13
Points
0
T

Twino

Member
Joined Mar 22, 2012
13 0
Npo mahakamani majaji na wakili wa pande zote mbili wameshakaa tayari wanaanza kusikiliza
 
Mzururaji

Mzururaji

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
1,268
Points
2,000
Mzururaji

Mzururaji

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
1,268 2,000
Hakuna kitu hapa yericko nyerere na ben saanane cjui walienda arusha na lema au ndo ritz aliwapeleka lunch mpaka leo wapo huko badala ya kufanya coverage napata moto!
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Points
2,000
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,000
Jamani mbona majibu mafupi sana .Kafuta rufaa?
 
Power G

Power G

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Messages
3,912
Points
1,225
Power G

Power G

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2011
3,912 1,225
Hakuna kitu hapa yericko nyerere na ben saanane cjui walienda arusha na lema au ndo ritz aliwapeleka lunch mpaka leo wapo huko badala ya kufanya coverage napata moto!
Wanakula vijisenti vya uswiss hao.
 
Imany John

Imany John

Verified Member
Joined
Jul 30, 2011
Messages
2,873
Points
1,500
Age
38
Imany John

Imany John

Verified Member
Joined Jul 30, 2011
2,873 1,500
Hata mimi nilitaka kuuliza kuhusu hili humu maana kimya kimezidi. Je hakuna makamanda wa kuripoti huko? Tusubiri live coverage kama ilivyokuwa kwa Lema.
Hata mimi,kesi inaanza saa tatu asubuhi hii
 
Sabung'ori

Sabung'ori

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2011
Messages
2,102
Points
1,250
Sabung'ori

Sabung'ori

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2011
2,102 1,250
...atamkaye maneno yaukweli hufunua haki,bali shahidi wa uongo hutamka hila...kila la kheri Mnyika...
 
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
13,355
Points
2,000
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
13,355 2,000
WanaJF
Mrufani Hawa Ng'hubi wa CCM ameamua kufuta kesi na Mahakama ya Rufaa imemtangaza Rasmi John Mnyika-Chadema ni mbunge halali wa wananchi wa Ubungo.
Hii habari Imethibitishwa.
 
F

FredKavishe

Verified Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,091
Points
1,195
F

FredKavishe

Verified Member
Joined Dec 4, 2010
1,091 1,195
Hawa ngumbi kaondoa rufaa yake ushindi kwa mnyika
 
PISTO LERO

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Messages
2,821
Points
1,195
PISTO LERO

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2011
2,821 1,195
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika na aliyekuwa mpinzani wake kwenye kinyang’anyiro cha kuwania wadhifa huo katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hawa Ng’humbi, kwa mara nyingine tena leo wanatarajiwa kupambana mahakamani.

Wapinzani hao wa kisiasa, wanatarajiwa kupambana kwa hoja za kisheria, wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya Ng’humbi ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iliyomthibitisha Mnyika kuwa mbunge halali wa Ubungo.

Mnyika, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alitangazwa na Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Ubungo, kuwa mbunge wa jimbo hilo, baada ya kupata kura 66,742 huku Ng’umbi akipata kura 50544.

Hata hivyo Ng’humbi kupitia Wakili wake, Issa Maige alifungua kesi Mahakama Kuu kupinga ushindi huo wa Mnyika, huku akiiomba mahakama ibatilishe matokeo na kuamuru uchaguzi huo urudiwe.

Katika hati ya madai ya kesi hiyo namba 107 ya mwaka 2010 na wakati wa ushahidi wake mahakamani, Ngh’umbi alidai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na kanuni za sheria wakati wa kampeni, ujumlishaji na utangazaji matokeo.

Hata hivyo Mahakama katika uamuzi wake, ilitupilia mbali madai ya Ng’humbi na badala yake ikamthibitisha Mnyika kuwa mbunge.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Mei 24, 2012, Jaji Upendo Msuya alisema upande wa madai ulishindwa kuyathibitisha madai yake pasi na shaka, huku akidai kuwa ushahidi wa Ng’humbi ulikuwa ni maneno ya kusikia tu ambayo hakuyashuhudia.

Hata hivyo, Ng’humbi hakukubaliana na hukumu hiyo na kuamua kukata rufaa akiiomba mahakama ya rufani itengue hukumu hiyo ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Rufaa hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa leo na Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani; Salum Massati, Katherine Oriyo na Nathalia Kimaro.

Ng’humbi katika rufaa yake hiyo aliyoifungua Oktoba 25, 2012,
Kupitia kwa wakili wake, Maige, ameorodhesha hoja kumi za kupinga hukumu hiyo, akidokeza kile anachokiona kuwa ni udhaifu katika hukumu.

Pamoja na mambo mengine, Ng’humbi anadai kuwa Jaji Msuya alikosea katika kutafsiri sheria na kupima ushahidi wa pande zote.

Baadhi ya hoja zake katika rufaa hiyo, Ng’humbi anadai kuwa jaji alikosea kusema kuwa makosa yaliyobainika katika ujumlishaji na kuhesabu kura na kusababisha kuwapo kwa kura 14,854, zisizohesabiwa hayakuathiri matokeo ya uchaguzi.

Anadai kuwa alithibitsha makosa katika mchakato wa uchaguzi yaliyosababisha kuwapo kwa kura 14, 854 zisizohesabiwa, hivyo jaji alikose kwa kutokuhamishia kwa mdaiwa, jukumu la kuelezea sababu za kuwapo kwa dosari hizo.

“Jaji alijipotosha kumshutumu mrufani kwa kutokubainisha kuwa makosa ya msingi yaliyobainika katika kujumlisha na kuhesabu kura yalikuwa ni ya nia mbaya,” inasisitiza hati hiyo ya rufaa na kuongeza
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,600
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,600 2,000
i knew it..yule mama anamzimika sana mnyika!!!alitaka attention yake,..kamanda john kaa mbali na gamba Hawa,asikulainishe na kufuta rufani
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,600
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,600 2,000
sasa alikata rufani ya nini?hakuna uwezekano wa kulipwa gharama,hata nauli ya daladala mnyika aliyotumia?sijui sheria mimi
 
Khakha

Khakha

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Messages
2,987
Points
1,500
Khakha

Khakha

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2009
2,987 1,500
ant- ccm mama ngumbi kainua mikono mwenyewe. chezea mnyika weye.
 

Forum statistics

Threads 1,283,500
Members 493,720
Posts 30,791,897
Top