Kesi ya shambulio la mkuu wa Wilaya Igunga, CHADEMA yashinda

[h=2]Mbunge ahukumiwa jela [/h]
Jumamosi, Julai 21, 2012 09:23 Na John Makambo, Tabora



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, imemhukumu Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbai (Chadema), kifungo cha miezi minne jela ama kulipa faini ya Sh 100,000, baada ya kumtia hatiani.


Mahakama hiyo, ilimtia hatiani Kasulumbayi kwa kosa la kumshambulia aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario ambaye sasa amehamishiwa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.


Mbali ya Kasulumbayi, mahamaka hiyo ilimhukumu kifungo cha miezi minne jela ama kulipa faini ya Sh 100,000 mwanachama mwingine wa chama hicho, Robert Magilani (30) kwa kupatikana na kosa hilo.


Washitakiwa wengine, Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga na Katibu wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Wilaya ya Igunga, Anuary Kashaga waliachiwa huru na mahakama, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa yao.


Kasulumbai pamoja na kupatikana na hatia ya kosa hilo, pia alitiwa hatiani kwa kosa la shambulizi la lugha chafu dhidi ya Kimario.


Pia mahakama hiyo, ilimwamuru Magilani kulipa faini ya Sh 50,000, ama kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela.


Mahakama hiyo pia iliwahukumu washitakiwa hao wawili kumlipa fidia Kimario ya Sh 100,000, kila mmoja kutokana na kumsababishia madhara kwenye mwili.


Akisoma hukumu hiyo, iliyochukua muda wa dakika 30, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, Thomas Simba, alisema mahakama imewatia hatiani washitakiwa hao katika makosa mawili ambayo ni shambulio na kutumia lugha ya matusi dhidi ya Kimario.


Hata hivyo, alisema mahakama ilifuta mashitaka mengine mawili yaliyokuwa yakiwakabili washitakiwa hao, ambayo ni kumwibia simu mbili za mkononi aina ya Nokia na kumweka chini ya ulinzi isivyo halali.


Baada ya kuwatia hatiani washitakiwa hao, wakili wa utetezi Mpogolo aliiomba mahakama kutotoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa huyo, kwa sababu ana umri wa miaka 62, wake watatu na watoto 27, huku akiwa na maradhi ya ugonjwa wa moyo na miguu kwa muda mrefu hivyo ana majukumu makubwa kifamilia.


Huku Magilani akielezwa kuwa ni kijana mdogo, ana mke na mtoto mmoja hivyo kupewa kwake adhabu kali kutaiathiri familia.


Itakumbukwa mapema mwaka huu, Kimario alikutwa na viongozi wa Chadema katika Kijiji cha Isakamaliwa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, akifanya mikutano na viongozi wa Serikali za vitongoji, kata, vijiji na madhehebu ya dini kinyume na sheria za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).



Mbunge ahukumiwa jela
 
Kaka wewe ndio una-mix mambo,
Yule mama alivaa mtandio, sio hijabu.

Pili ni mfuga/mla kitimoto mzuri tu, hivyo Mtandio na Noah damudamu!!

Hahahahaaaaa! Mkubwa Sorry, ukweli ni mimi mwenyewe ndiye niliyejimix. Tabu ya viongozi wetu wa kiislamu ni kukurupuka hasa linapokuja suala la kisiasa. Sijui wanapewaga hela ngapi! Ona sasa mwisho wa siku wamejikuta walikuwa wakimtetea mla na mfuga Noah.
 
Mahakama ya hakim mkazi Tabora imewakuta wabunge na makada wa CHADEMA hawana hatia katika shitaka la kumshambulia mkuu wa wilaya ya Igunga wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga.

Akisoma hukumu hiyo hakimu alisema hakukuwa na ushahidi wakutosha kuthibitisha makosa waliyo shitakiwa nayo wabunge na makada wa CHADEMA pia aliwaonya upande wa mashitaka kwa kufungua kesi zenye mlengo wa kisiasa akisema ni kuipotezea mahakama muda na kuaribu pesa za walipakodi.

Alisema anakubaliana na hoja za utetezi kwamba mtandio nivazi linaloweza kuvulika pasipo shambulio hata wakati mtu akitembea laweza vulika pia alisema kwa sheria ya ulinzi shirikishi wananchi waweza kumshikilia mharifu popote mpaka polisi wafike hivyo kuweka chini ya ulinzi DC huyo halikuwa kosa.

Nawasilisha.

Source: nilikuwepo mahakamani.

hivi wale wabunge waliohukuwa miezi sita au kulipa faini ya 200,000/- inahusu nini? tafadhali nijulisheji plz
 
Back
Top Bottom