Kesi ya 'Samaki wa Magufuli': Serikali yapigwa 'bao la kisigino' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya 'Samaki wa Magufuli': Serikali yapigwa 'bao la kisigino'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Jul 14, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imewaachia huru washitakiwa 31 kati ya 36 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kuvua samaki bila kibali katika Bahari ya Hindi, eneo la Tanzania. Washitakiwa watano, kapteni wa meli Hsu Chin Tai (61), wahandisi wa meli ya Tawariq 1, Cai Dong Li (44) na Chen Rui Hai (34) na mawakala Zhao Hanquing (39) na Hsui Sheng Pao (55), wameonekana wana kesi ya kujibu. Mahakama pia imeamuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuwarudishia hati za kusafiria na kuwaandalia utaratibu wa kuwarudisha makwao washitakiwa walioachiwa huru. Imeamuru Jackson Toya (39), ambaye hana hati ya kusafiria arudishwe nchini Kenya.

  Jaji Augustine Mwarija alitoa uamuzi huo jana, na kupokewa kwa hisia tofauti na wahusika, baadhi wakitokwa machozi ya furaha, wengine wakikumbatiana na hata kuzungumza Kiswahili, kwamba wamechoka kuishi Tanzania, hivyo ni bora warudi kwao. Mmoja wa washitakiwa hao raia wa Vietnam, alisema kukaa kwake gerezani kumemwezesha kujifunza Kiswahili, jambo lililomwezesha kupata marafiki wa Kitanzania, waliokwenda kumjulia hali gerezani na kumpatia chakula.

  Kesi hiyo awali ilikuwa ikiwakabili washitakiwa 37 kutoka mataifa mbalimbali, ambao Juma Juma, raia wa Kenya aliyefariki dunia wakati kesi ikiendelea kusikilizwa. Walikuwa wakidaiwa Machi 8, mwaka 2009, saa 6.00 usiku, katika ukanda wa Bahari ya Hindi, ndani ya eneo la Tanzania, walikamatwa wakivua bila kibali. Jaji Mwarija akitoa uamuzi jana, alisema, amewaachia huru washitakiwa hao kwa kuwa hati ya mashitaka haielezi bayana ni washitakiwa gani walikuwa wakivua samaki, kwani wengine walikuwa wapishi na walikuwa wanatimiza majukumu yao ya kazi. Alisema kapteni alikuwa msimamizi mkuu wa meli hiyo, hivyo pamoja na wenzake wanne wana kesi ya kujibu, hivyo watatakiwa kujitetea katika kikao kijacho cha mahakama.

  Baada ya uamuzi huo kutolewa, mawakili wa washitakiwa hao, Ibrahimu Bendera na John Mapinduzi, waliiomba mahakama iwapatie hati za kusafiria ili waweze kurudi kwao, kwani zilitolewa mahakamani kama vielelezo. Wakili wa Serikali, Biswalo Mganga, alidai vyombo vinavyohusika ni lazima vifanye utaratibu ili waweze kuondoka na kurudi kwao. Washitakiwa hao kutoka China, Indonesia, Kenya, Vietnam na Philippines, Machi 10, mwaka huu, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu walikosomewa mashitaka, kabla ya kesi kuhamishiwa Mahakama Kuu.

  Uhuru
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Hatareeeee!!!! Mlungula ushapita hapo!!!!!!
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu kama hiyo. Sheria msumeno.
   
 4. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli kuna umuhimu wa kuangalia ufanisi wa ofisi za DPP na mwanasheria Mkuu. Bila shaka umefika wakati muafaka wa kuwa na muendesha mashtaka wa UMMA kwenye kesi kubwa zenye public interest.
   
 5. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hii serikali huwa haina historia ya kushinda kesi, nawashauri wafungue kesi ya kudai fidia haraka sana na viongozi walioshiriki wawajibike haraka iwezekanavyo kwa kulitia taifa hasara kuhifadhi samaki kwa mabilioni na pia jamaa warudishiwe hela ya samaki wao
   
 6. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  "Jaji Mwarija akitoa uamuzi jana, alisema, amewaachia huru washitakiwa hao kwa kuwa hati ya mashitaka haielezi bayana ni washitakiwa gani walikuwa wakivua samaki, kwani wengine walikuwa wapishi na walikuwa wanatimiza majukumu yao ya kazi."
   
 7. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Nilijua hili kuna rafiki yangu tulibishana naye sana. Kosa wanalokabiliwa siyo kuvua samaki bali kupitisha meli eneo la tanzania kibahari. ili ukamatwe unavua samaki ni lazima nyavu ziwe chini ya maji na zinavutwa na hiyo meli kitu ambacho hawa jamaa hawakukifanya. Hao watano watashitakiwa kuingia eneo la tanzania bila kibari ambalo faini yake ni dola 50 na wakishindwa kulipa kifungo jela miezi kadhaa basi biashara imeisha.
   
 8. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Na bado watu wamekalia ofisi mzee, na wamewaaga wake zao kuwa wanakwenda kazini. Yaan hata mwanafunzi anayesomea shahada ya sheria kwa mwaka wa kwanza anajua hati ya mashtaka inatakiwa iwe na nini, sembuse huyu DPP! Haya si makusudi kabisa! Kumbuka kesi ya Zombe, halafu angalia mwenendo wa Kesi za kina Mramba.

  Hii ni hatari
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama DPP mwenyewe ndie anayeandika hayo mashtaka.
   
 10. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yeye ndio anatoa go ahead baada ya kujiridhisha
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Zomba tueleze vyema msemeno upi unaosema hapa .Tuna mifano kibao juu ua mlungula .Zomba karibuh jamvinij ila naamini utanawa karibuni .Una kasi ye utetezi mno lakini utanasa soon .
   
 12. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Guys elimu inasaidia sana kwa kweli,sasa mambo yameisha kimya kimya bila aibu na sisi tuelewe vipi??ina maana hatuna wasomi kwenye hii nchi zaidi ya mafisadi??
   
 13. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  -The DPP decides whether to prosecute people for committing crimes and what the charges should be. Once the prosecution starts, the Office of the DPP is in charge of the prosecution case.

  -Crimes are investigated by the Police. When Police investigate a serious crime, they send a file to the DPP who decides what charges, if any, to bring.

  How does the DPP reach a decision to prosecute?
  The decision to prosecute or not to prosecute is very important. If someone is prosecuted and later found not guilty, they can suffer a lot of damage. On the other hand, a decision not to prosecute can cause great stress and upset to a victim. So the DPP must carefully consider whether or not to prosecute.

  When the Police complete their investigation, they send a file to the DPP. The prosecutor must read the file carefully and decide whether there is enough evidence to put before the court. The judge or wazee wa Baraza have to be convinced beyond a reasonable doubt that a person is guilty. It is not enough for them to think that the accused is probably guilty.

  For this reason it is important to know if there is independent evidence that supports the victim's story. This could be evidence from a witness or forensic evidence such as fingerprints or bloodstains. Independent evidence makes a stronger case than a case based on one person's word against another's.
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280

  Sio makosa yote. Makosa ambayo anatoa go ahead ni machache sana.

  What you have written is too theoretical and text book based. That is not what happens in practice. You may say that all the prosecutions in Tanzania are the business of the DPP. In theory, this may be true at least for two reasons. First because the law as we saw it gives power to the DPP to initiate prosecutions or criminal proceedings against any person, take over any criminal proceedings begun by any person or authority whatsoever and to discontinue any criminal proceedings whether initiated by his office or any other person or authority. The second reason for the theoretical truth of the argument is that all public prosecutors are appointed by the DPP and thus subject to his control and supervision.

  However, this theoretical truth belies the practical truth in practice. Except for those cases where his explicit consent is required by law before a criminal proceeding is instituted and prosecution undertaken, the DPP may never see or know anything about a case. In cases where the consent of the DPP is required before the institution of criminal proceedings not only would he demand to see the investigation file and thus evaluate the evidence, but also he may give guidance to the investigative agencies.

  Cases requiring the consent of the DPP are few and far between. The reason is that they comprise offences like raising discontent and ill will among the inhabitants, incest by males or females, abuse of office by public officials and a handful of other offences, which in reality are not the most common offences. For these reasons, it is very likely that the DPP may never have seen or known anything about the files of the persons accused in "Kesi ya Samaki wa Magufuli" unless the prosecution of these peoeple requires explicit consent from him.
   
 15. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #15
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Kila kesi tunabwagwa tu, pesa zishaliwa kwa kuendesha kesi tukijua wazi tutashindwa. Bado mtataka Rostam na wenzake wafunguliwe mashtaka?
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  For a criminal lawyer definitely yes.
   
 17. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  The DPP prosecutes all serious crimes and sometimes less serious crimes. The most serious cases are heard before a Wazee wa Baraza in the Circuit Court, Central Criminal Court or Special Criminal Court.

  Police may prosecute less serious crimes. However, the prosecution is still taken in the name of the DPP and the DPP has the right to tell the Police how to deal with the case.
   
 18. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  By DPP do you mean the Director of Public Prosecutions personam or the Office Director of Public Prosecutions? If you mean the DPP personam, have you ever seen him in court prosecuting a case whether serious or less serious? In deed, the ultimate authority for authorising prosecutions lies with the Attorney General. However, since that is a political post and it is desired to have a non-political (public service) post carry out this function in most circumstances, the prosecutorial powers of the AG are normally delegated to the DPP. That is why the DPP is assisted in the discharge of his functions by State Attorneys based at the AG Chambers.

  Nonetheless, in exercising of his powers, the DPP himself has appointed various other public officers to be public prosecutors. As such Labour Officers, Health Inspectors, Postal officials and other public officers prosecute cases related to their occupations. Public Prosecutors so appointed however remain subject to the directions of the DPP in the conduct of the prosecution.

  The important thing here is to differentiate between the DPP personam and the office of the DPP. The DPP personam does not prosecute cases. What he does is to give explicit consent in specific cases where the law so requires before a criminal proceeding is instituted and prosecution undertaken. Once he has given his consent, the prosecutors (State Attorneys) take the lead. Compare this with the Director of Criminal Investigation (DCI). Ii is not the SCI himself who investigates criminal allegations but the investigators who works under his office.

  Regarding the prosecution of cases by the police, due to the shortage of State Attorneys, the DPP was given powers to appoint police officer not below the rank of Assistant Inspector of Police as a public prosecutor. However, a law was passed recently banning any police officer from prosecuting cases, whether serious or less serious. Whether the law has come into force, I don't know.
   
 19. n

  niweze JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Who really own watanzania? Are we very very stupid au tunataka kuitwa hivyo? Kwa hiyo hapa tatizo hakuna records sio na kwa kifupi hakuna ushahidi na hakuna aliefanya makosa.

  Kumbe basi hatuna vyombo vya usalama tanzania except pale tunapoibiana na ujambazi tu ndipo mahakama na justice system ya Tanzania inafanya kazi after that nothing is working. Bing bing bing kwa walio na utajili.

  I am lost too na sijui tatizo ni nini kwa sababu ukifikiria sana unajikuta unakuwa mwehu kama kikwete, nape na ccm. Just wave boy...
  :fish:
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  ninapochoka ni hapa: hati ya mashtaka hakimu kaisoma jana? stay away from trouble if u can, manake hawa jamaa wanaweza ku-twist things ukashangaa watakavyokutenda! all this time! haya samaki wa watu tushatia ndani! kweli shamba la bibi raha yake uwe mjukuu!
   
Loading...