Kesi ya Salakana dhidi ya NdesaPesa ni kituko kitupu

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
1. Msiwapigie kura mafisadi na wale waliowagawia fulana, kofia na skafu kwani hao ndio wanaoharibu nchi.

Niliyonukuu hapo juu ni kauli ya utata ya Padri huko Moshi na ndio msingi wa kesi iliyo mezani... Katika sheria wana kitu wanaita "ushahidi usio na shaka yoyote"... Swali jee huu ni ushahidi tosha au anataka kuisaidia mahakama kumaanisha maneno ni kijembe kwa CCM???
Mimi bado naangalia nini maana halisi ya hayo maneno maana Salakana keshaitafsiria mahakama kuwa yanamaanisha CCM kwa kuwa yeye "sijui ni fisadi??" au aligawa kofia, fulana na Skafu...

Salakana analalamikia uchaguzi huo kuwa, ulitawaliwa na ukiukaji taratibu, ubaguzi na rushwa na kufanya uchaguzi usiwe huru na wa haki na kuomba mahakama kumzuia Ndesamburo kugombea kwa miaka kipindi cha mitano.
Pia, analalamikia matamshi ya Ndesamburo na mawakala wake kumuita yeye kuwa ni Mrombo, hana nyumba, amevamia Msitu wa Rongai na kutoa zawadi ya Sh2 milioni kwa mtu atakayeonyesha nyumba yake Moshi mjini.

2. Salakana analalamika kuwa, matamshi hayo yalimaanisha kuwa Mrombo kwa kabila, hakuwa na sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge, hivyo wapiga kura wakaacha kumchagua na kufanya uchaguzi huo kuwa batili kisheria.

Hapa kuna kazi kweli!!! Kesi ya msingi iko juu kabisa hii mbili tunaita kesi ya ziada dhidi ya unaemtuhumu... Hapa Salakana anajaribu kutafsiria mahakama... Kwamba wachagga nao hubaguana kwa ukabila upi sijui?? au umaeneo?? Kuhusu nyumba pia hana la maana kwa kuwa hata mimi ningeibuka tuu ghafla kutoka hata NY kwenda kugombea???....Ndio maana kuna nchi inawalazimu watu wawe wakazi wa hilo eneo kuwa wameeishi zaidi ya miaka mitano au mitatu... Wanaogopa wezi wa mchana!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom