Kesi ya Saileth Vithlani wa kashfa ya Rada

Status
Not open for further replies.
kama kashtakiwa kwa uongo basi hiyo kesi ni ya polisi sio takukuru, au ndio yale yale hawana utaalamu wa kutosha au utashi wa kutosha?
 
They are a part of the game; they will always find a way of twisting the truth. Nothing serious gonna happen in this country so long as CCM continues to rein. Until we come to terms with this painful fact, our efforts to shame the mafisadi are doomed!
 
Sasa ndio napata picha kwa nini wanamshitaki dalali; kumbe kesi sio ya rushwa ni ya kusema/kutoa taarifa za uongo...

Hapa naona kuna watu wanatafuta mahali pa kutokea, kwa ksingizio kuwa "serikali ilidanganywa" na kwamba mtuhumiwa amefikishwa mahakamani. PCCB wanafanya siasa badala ya kupiga vita rushwa.

Hivi Interpol watamtafuta mtu anayetuhumiwa kusema uongo?
 
Serikali yetu na mazingaombwe yake... kumbe mwenzenu kafunguliwa mashtaka ya kusema uongo...


Akili yangu haikubali kupokea ujumbe huu!!!

What? yaani hata uchunguzi ulio fanywa na wataalamu toka uingereza ni kwamba alisema uongo? TUMEKWISHA!!
 
hapana uongo wake ni kuwa hakuiambia serikali bei ya kweli ya rada hiyo...yeye aliongeza bei ili apate kitu kidogo. Tatizo walioagawana hizo 13 Bilioni wengine bado wapo serikalini.. na wengine "wamestaafu" siasa..
 
kama August alivyosema nadhani hiyo ni kesi ya polisi na siyo TAKUKURU.

Pia nadhani huyo jamaa akituhumiwa kuongopa na kusema uongo inakuwa rahisi kutomuuliza washirika wake, yaani muongo ni yeye tu, wakati ulaji au utoaji rushwa unakuwa na washiriki wawili au zaidi.
 
hapana uongo wake ni kuwa hakuiambia serikali bei ya kweli ya rada hiyo...yeye aliongeza bei ili apate kitu kidogo. Tatizo walioagawana hizo 13 Bilioni wengine bado wapo serikalini.. na wengine "wamestaafu" siasa..


Hahaaa sasa hiyo huku kwa ng'ambo wanasema ni Fraud na kesi hiyo inaweza kukuweka lupango kwa muda...hapo nyumbani Fraud ina jina gani kisheria; maana tunaweza kuwabeza hawa Takukuru kumbe wana plan kubwa iliyotulia. Wanaweza kuwa wanataka kufanya kama FBI, wanamshikilia mtu kwa Traffic au Immigration offence kumbe wanasubiri matokeo ya dna ili wamshitaki kwa murder....najaribu kuwa na matumaini kidogo.
 
hapana uongo wake ni kuwa hakuiambia serikali bei ya kweli ya rada hiyo...yeye aliongeza bei ili apate kitu kidogo. Tatizo walioagawana hizo 13 Bilioni wengine bado wapo serikalini.. na wengine "wamestaafu" siasa..

'Wamestaafu siasa' ili kukwepa kujibu tuhuma nzito dhidi yao, lakini inapokuja kwenye kuhudhuria mazingaombwe ya CCM yaliyomalizika hivi karibuni huko Dodoma bado 'wamo kwenye siasa.'
 
suala la rada is the biggest scandal in our history, na kama tungekuwa na mtu mwenye mabilinganya mawili, leo hii kuna watu wangekuwa wanalilia Keko.... siyo Magurumbasi kule gerezani!
 
suala la rada is the biggest scandal in our history, na kama tungekuwa na mtu mwenye mabilinganya mawili, leo hii kuna watu wangekuwa wanalilia Keko.... siyo Magurumbasi kule gerezani!

Mabilinganya mawili? kwani sasa hivi ana nini? ama hatuna mtu?
 
suala la rada is the biggest scandal in our history, na kama tungekuwa na mtu mwenye mabilinganya mawili, leo hii kuna watu wangekuwa wanalilia Keko.... siyo Magurumbasi kule gerezani!

Mzee naona sasa umeamua kumkoma mtu kwa tusi la reja2 :mad:
 
not really.. ni msemo tu wa kikwetu kama vile anayesema "nyege ni kunyegezana" hatukani...
 
not really.. ni msemo tu wa kikwetu kama vile anayesema "nyege ni kunyegezana" hatukani...

na sie pia kwetu tuna msemo "Akuchokonoae mwishowe hujichokonoa" lakini sijui una maana gani !

na msemo mwingie ni
"Ukiona mlango wa nyuma(wa uani) umefungwa, wee bwaga mzigo na uache atahangaika nao mwenyewe"

again, sijui hii misemo ina maana gani !

Kwaherini !
 
Kuna mtu kanitumia katika e-mail yangu ninayoitumia humu JF... Naiona kama imetulia.. Wana JF watakaobahatika kuwa na charge sheet waiweke humu ijadiliwe. ila hii Habari hapa chini inatoa mwanga kwanza.

MFANYABIASHARA mwenye asili ya Kiasia, Sailesh Vithlani, anayehusishwa na ufisadi katika ununuzi wa rada iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania, ameshitakiwa kwa kusema uongo mahakamani na kudanyanga makachero wa serikali.

Hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani Alhamisi iliyopita, haionyeshi kuwapo kwa kesi ya rushwa dhidi ya Vithlan na badala yake ameshitakiwa kwa kusema uongo pekee.

Hata hivyo Takukuru wanaelezwa kuandaa hati mpya ya mashitaka pindi watakapomkamata Vithlani na watuhumiwa wengine.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya mashitaka iliyowasilishwa kwa Hakimu Sivangilwa Mwangesi, Vithlan anadaiwa kwamba alitoa ushahidi wa uongo akiwa chini ya kiapo alipoitwa kutoa ushahidi mahakamani hapo Julai 25, mwaka jana.

Pamoja na kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilipewa hati ya kumkamata Vithlani Agosti 30, mwaka huu, hati ya mashitaka iliwasilishwa mahakamani hapo Alhamisi iliyopita ikiwa na makosa matatu yakiwamo mawili ya kusema uongo chini ya kiapo na moja la kumdanganya ofisa wa Takukuru.

Katika kesi hiyo namba 1474 ya 2007, Shailesh Pragji Vithlani anadaiwa kwamba alisema uongo mbele ya hakimu Katarina Revocati, wa mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, alikokua akitoa ushahidi chini ya kiapo.

Imedaiwa mahakamani hapo kwamba huku akijua kwamba anayoyasema ni uongo kuhusiana na ununuzi huo wa rada ulioigharimu serikali ya Tanzania kiasi cha Dola za Marekani 39, 972, 450 (sawa na Sh bilioni 70).

Vithlan anadaiwa kwamba aliidanganya mahakama kwamba kampuni ya Envers Trading Corporation inamilikiwa na Pablo J. Espino na Adelina M. Estriby akijua kwamba ni uongo kwa kuwa kampuni hiyo alikua akiimiliki yeye kama Mkurugenzi na alilipwa asilimia 31 ya mauzo ya rada kama kamisheni.

Vithlani anadaiwa kulipwa kiasi cha Dola za Marekani 12,391,459.50 kwa kile alichodai kwamba ni kuwa wakala wa akitumia mkataba kati ya kampuni ya Red Diamond Trading Company limited na Envers Trading Corporation.

Ilidaiwa mahakamani hapo kwamba Vithlan aliwasilisha taarifa za uongo kudai kwamba alilipwa Dola za Marekani 390, 000.00 tu sawa na asilimia moja ya bei ya rada iliyouzwa kwa serikali ya Tanzania na British Aero Space (BAe system) ya Uingereza kwa kuwa mshauri tu katika biashara hiyos.

Kwa mujibu wa Kanuni ya Adhabu, mtuhumiwa akipatikana na hatia atahukumiwa kwenda jela miaka saba kwa kusema uongo wakati makosa ya rushwa adhabu yake ni miaka 30 na huambatana na masharti magumu ya dhamana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom